Watanzania tukiiga mifumo ya familia za kihindi na kiarabu nusu ya ufukara/umaskini katika jamii zetu unatokomea

Kwa wanaokumbuka miaka ya 90 kulikua na usafiri wa mabasi ya bin kleb.
Mmiliki alipoanza kuzeeka kawakabidhi watoto magari waendeshe mradi wa usafiri.Mpaka kufikia miaka ya 2000 watoto wakaongeza maroli,vituo vya mafuta.
👆
Hayo ni mambo wanafanya waarabu na wahindi.Kwa wazawa ni adimu sana,sababu ni zilezile ubinafsi na roho mbaya.
Nilisoma na watoto wake forest Hil namkumbuka mmoja wa kike lanya qlifanyaga kituko kimoja hicho
 
Je, Waafrika Tungeweza Kujifunza Kutoka kwa Wahindi na Waarabu?

Jioni ya Jumapili, nilikuwa nikiwa miongoni mwa wazee wa jiji hili kwenye kikao cha kahawa, mahali ambapo akili hupata fursa ya kutafakari zaidi hali ya jamii kuliko vitabu vya darasani. Katika mazungumzo hayo, mada nyeti iliibuka – kusaidiana pale matatizo yanapojitokeza. Wazo hili lilitokana na ombi la mzee mmoja wa kikao kutaka michango kwa ajili ya rafiki yake aliyekuwa na maradhi. Nilipochunguza hali hii, nilijiuliza kwa nini jamii zetu za Kiafrika zinakumbana na changamoto kubwa za kifamilia na kifedha tunapopatwa na matatizo kama haya, ilhali wahindi na waarabu waliozaliwa hapa wanakabili matatizo kama haya kwa urahisi zaidi?

Mifumo ya Familia na Utajiri wa Pamoja

Moja ya siri kubwa ya mafanikio ya familia za kihindi na kiarabu ni mshikamano wa kifamilia na uzalishaji wa pamoja. Wahindi na waarabu huwekeza katika biashara za kifamilia kwa malengo ya muda mrefu. Mtoto anayesoma hujua elimu yake inatumikia familia na biashara zao. Shahada si tiketi ya kuanza maisha peke yake, bali ni nafasi ya kuchangia ukuaji wa biashara za kifamilia.

Kwa jamii za Kiafrika, hali ni tofauti. Watoto hupewa jukumu la kusoma na baada ya hapo kupambana kivyao. Familia nyingi zimepoteza msingi wa kuendeleza mali na utajiri wa kifamilia kwa sababu kila mmoja anajitahidi kujitegemea mara baada ya kufikia umri wa utu uzima. Hii inaleta changamoto kubwa ya kudumisha maendeleo na ustawi wa kifamilia kwa muda mrefu.

Ushirikiano wa Kaya Moja na Maadili ya Jamii

Familia za kihindi na kiarabu mara nyingi huishi katika makazi yanayowaunganisha wote – mababu, mabibi, wajomba, mashangazi, na hata binamu. Mfumo huu huimarisha maadili na utamaduni wa jamii, huku ukitoa fursa kwa vijana kuiga mifano mizuri ndani ya familia. Watoto hawaishi kutangatanga mitaani, bali wanajifunza kupitia mifano hai ya maisha ya familia zao.

Kwa Waafrika, muundo wa familia pana umekuwa ukipungua. Mifumo ya kijamii ambayo hapo zamani iliwapa watoto mwelekeo sahihi imekufa, na vijana wengi wanakosa maadili na mwongozo wa maisha. Hali hii imechangia kuongezeka kwa changamoto kama madawa ya kulevya na uhalifu, jambo ambalo ni nadra kwa familia za kihindi na kiarabu kwa sababu wanazingatia sana heshima ya familia.

Mafanikio ya Wahindi na Waarabu Ughaibuni

Mfumo huu wa mshikamano wa kifamilia na kibiashara hauishii katika nchi za Afrika pekee. Ukiangalia wahindi na waarabu wanaohamia nchi za Magharibi, utagundua kuwa wanaendelea kuwa na maendeleo makubwa hata huko. Hii ni kwa sababu ya utamaduni wao wa kusaidiana na kuwekeza katika familia. Mtu mmoja akifanikiwa kufika, hufanya kila juhudi kuwasaidia ndugu zake wengine kufika ili kusukuma gurudumu la maendeleo.

Kwa upande mwingine, Waafrika wengi wanapofika Ughaibuni, mafanikio yao huonekana kwa kusimamia masuala ya kifamilia kwa mbali, mara nyingi kupitia kutuma pesa za matumizi au ujenzi wa nyumba nyumbani. Hata hivyo, juhudi za kuwainua ndugu kiuchumi au kuwasaidia kujiendeleza hazipewi uzito unaostahili. Matokeo yake, maendeleo ya kifamilia na kijamii hubaki nyuma ukilinganisha na jamii za wahindi na waarabu.

Kutokomeza Aibu Ndogo Ndogo

Katika familia za Asia, mtu anayepoteza mwelekeo hupewa msaada na nafasi ya kuendelea kuishi bila kudhalilisha familia. Kwa mfano, mtu mwenye matatizo ya uteja anaweza kupewa kazi "geresha" ndani ya familia au biashara, lakini bado anatunzwa. Kwa upande wa Waafrika, mtu kama huyu mara nyingi hukataliwa na familia, akifukuzwa nyumbani na kuishia mitaani. Matokeo yake ni aibu ya kijamii inayowakumba familia nzima.

Je, Tungeweza Kubadilika?

Kwa Waafrika, kuna haja ya kurejesha mshikamano wa kifamilia kwa kushirikiana katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Familia zetu zinapaswa kuanza kuwekeza pamoja na kuondokana na fikra za kila mmoja kupambana kivyake. Tunapaswa kutambua kuwa maendeleo ya mtu mmoja hayatoshi – familia zenye mshikamano zina nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kwa ujumla.

Pia, tunapaswa kuanzisha mifumo ya kuwasaidia wanajamii wetu wenye changamoto, badala ya kuwatelekeza. Tukijifunza kutokana na mifumo ya familia za kihindi na kiarabu, tunaweza kuanza kupunguza ufukara katika jamii zetu na kurejesha heshima na mshikamano wa familia za Kiafrika.

Mwisho wa yote, umaskini si tu tatizo la kiuchumi; ni tatizo la kijamii linalotokana na kuyumba kwa mifumo ya familia. Hatujachelewa kujifunza na kubadilika – tukianza leo, tunaweza kujenga msingi bora kwa vizazi vijavyo.
Umetukosea sana waafrika. Sisi tuna mila na desturi zetu za kiafrika. Hatupaswi kucha tamaduni zetu kwa kigezo cha maendeleo. Waafrika ni waafrika na Wahindi na Waarabu watabaki hivyo hivyo. Kuna jamii za kuwaiga ila siyo waarabu na Wahindi. Wana roho mbaya na katili dhidi ya ngozi nyeusi. Waliwauza mababu zetu kama bidhaa sokoni na kuchukua mali zetu kwaajili ya kujinufaisha wao.
 
KWA

MBONA WACHAGA WANAFANYA HIVYO KITAAAAAAMBO HAINA HAJA KUTOLEA WAHINDI MFANO
 
Waafrika wapunguze warwa au pombe, kazi iwe ni ibada, uaminifu uwe mbele. Akili ziachane na kushangalia makalio badala yake zishughulike kujifuza mbinu za mafanikio kutoka kwa kuwa karibu na waliofanikiwa. Hapo mambo yatasonga mbele
 
Umetukosea sana waafrika. Sisi tuna mila na desturi zetu za kiafrika. Hatupaswi kucha tamaduni zetu kwa kigezo cha maendeleo. Waafrika ni waafrika na Wahindi na Waarabu watabaki hivyo hivyo. Kuna jamii za kuwaiga ila siyo waarabu na Wahindi. Wana roho mbaya na katili dhidi ya ngozi nyeusi. Waliwauza mababu zetu kama bidhaa sokoni na kuchukua mali zetu kwaajili ya kujinufaisha wao.
udhaifu wetu ndo ulifanya tukaingia mikononi mwao tuelewe point sio kila kitu chakuiga ila upendo wa kweli,masikilizano ,kushirikiana,tabia bora za utawala na nidhamu, niamini tungekuwa na quality hizi tokea awali tusingetumiwa vibaya vile
 
Umetukosea sana waafrika. Sisi tuna mila na desturi zetu za kiafrika. Hatupaswi kucha tamaduni zetu kwa kigezo cha maendeleo. Waafrika ni waafrika na Wahindi na Waarabu watabaki hivyo hivyo. Kuna jamii za kuwaiga ila siyo waarabu na Wahindi. Wana roho mbaya na katili dhidi ya ngozi nyeusi. Waliwauza mababu zetu kama bidhaa sokoni na kuchukua mali zetu kwaajili ya kujinufaisha wao.
2024 umeshindwa kabisa kumove on, dunia inaenda mbele wewe bado upo na story za utumwa. Mataifa makubwa yote unayoyajua yanashirikiana na kila race kutimiza malengo yao.

Wewe upo na anha huyu Muhindi, ah huyu Mwarabu alituuza utumwa.

Upo kwenye Comfort Zone.
 
Wafuate wewe na Familia yako. Mbadili na rangi uwe mweupeeee na nywele ndefuuuu alafu mkae pamoja kama waarabu na Wahindi wenu pendwa.
 
Umetukosea sana waafrika. Sisi tuna mila na desturi zetu za kiafrika. Hatupaswi kucha tamaduni zetu kwa kigezo cha maendeleo. Waafrika ni waafrika na Wahindi na Waarabu watabaki hivyo hivyo. Kuna jamii za kuwaiga ila siyo waarabu na Wahindi. Wana roho mbaya na katili dhidi ya ngozi nyeusi. Waliwauza mababu zetu kama bidhaa sokoni na kuchukua mali zetu kwaajili ya kujinufaisha wao.
Kuntu sana hilo.
Mwafrika ana mila na tamaduni zake.
 
Ni rahisi zaidi kuwa na umoja na ndugu yako ugenini kuliko kwenye mji wenu wenyewe isipokuwa mmekuwa na utamaduni wa kushikamana tangu awali
Na hii ndio secret iliyopo wanapendana hivyo wakiwa ugenini ila huko kwao wanafanyiana roho mbaya zaidi ya waswahili.
Waswahili pamoja na roho mbaya zetu huwezi ukamnyima mtu chakula au maji ukimuona yupo kwenye majanga,au kumsaidia ombaomba hela ni jambo la kawaida ila kwa upande wa wahindi hata wamuone mtu amezidiwa kwa kukosa maji na chakula wanampita tu
 
Mkuu narudia tena kusema mtu mweusi anaroho mbaya mimi pia ni mweusi ila jamani sisi waafrika tuna roho mbaya sana. Unakuta limtu limesomeshwa na wazazi na ndugu wameuza mashamba na mifugo yote, leo limeajiriwa limepata kazi limeoa, yeye na mke wake wanakula jasho la wazazi na nduguze waliomsomesha, mbaya zaidi mke anamtawala na ataki ndugu wa mume wakanyage kwao na lijamaa linaridhila tu kama msukule. Inakufaa nini kuwa na kazi nzuri nyumba na magari na watoto wako wasome International school huku wazazi wako na ndgu zako waliokufikisha hapo huwajali.

Jamani ukifanikiwa beba ndugu zako usomeshe au wape mtaji wajitegemee tuache roho mbaya ya kumjali zaidi mtu ambaye hakuwepo wakati wazazi na ndugu zako wanahenya, tena wengi wetu tulipokuwa tukikwama chuo tulipiga simu kwa kila ndugu kujaribu bahati
Ndugu wa kiswahili hawabebeki,narudia tena ndugu wa kiswahili hawabebeki,hawasaidiki.
Usione watu wamejitenga na ndugu ukadhani ni wajinga au ukadhani hawajui hizo hesabu za kuwafungulia biashara,ndugu unampa hela ya mtaji anakula hela baada ya mwezi anakuja tena na visingizio kibao umpe hela nyingine na ukimpa anaenda kuwaambia na wengine baada ya wiki mwingine anakuja kukusimulia shida zake watahakikisha wanakunyonya hadi ufilisike ili wote muwe sawa
 
Umetukosea sana waafrika. Sisi tuna mila na desturi zetu za kiafrika. Hatupaswi kucha tamaduni zetu kwa kigezo cha maendeleo. Waafrika ni waafrika na Wahindi na Waarabu watabaki hivyo hivyo. Kuna jamii za kuwaiga ila siyo waarabu na Wahindi. Wana roho mbaya na katili dhidi ya ngozi nyeusi. Waliwauza mababu zetu kama bidhaa sokoni na kuchukua mali zetu kwaajili ya kujinufaisha wao.
Hamna jamii ambayo haijajihusisha na shughuli za utumwa, hivi unadhani walivyokuwa wanakuja Afrika walikuwa wanakamata watu porini kama nyani? Tulikamatana sisi wenyewe na tukauzana kwa mwarabu na mzungu na huo ndio ukweli
 
Yaani nimewekeza nimenunua kiwanja,nimejenga nyumba ndogo pamoja na frem nikamfungulia duka ili litusaidie mimi na yeye lakini kapaacha akaondoka kwasasa eti nahangaika kutafuta mtu wa kusimamia.Can you imagine umewekeza sehemu milioni 10 halafu mama yako aliyekuzaa anakukwamisha?
Mkuu naomba kazi
 
sisi waafrika ni wajamaa, huo ndio mfumo tuliyokuzwa nao. haya unayosema ni ya mabepari. Hapo ndio utofauti unapoanzia. sasa ukichanganya na mila na desturi zetu ndio unatupata sisi wenyewe OG kabisa na rangi zetu zote. karibu.
 
Je, Waafrika Tungeweza Kujifunza Kutoka kwa Wahindi na Waarabu?

Jioni ya Jumapili, nilikuwa nikiwa miongoni mwa wazee wa jiji hili kwenye kikao cha kahawa, mahali ambapo akili hupata fursa ya kutafakari zaidi hali ya jamii kuliko vitabu vya darasani. Katika mazungumzo hayo, mada nyeti iliibuka – kusaidiana pale matatizo yanapojitokeza. Wazo hili lilitokana na ombi la mzee mmoja wa kikao kutaka michango kwa ajili ya rafiki yake aliyekuwa na maradhi. Nilipochunguza hali hii, nilijiuliza kwa nini jamii zetu za Kiafrika zinakumbana na changamoto kubwa za kifamilia na kifedha tunapopatwa na matatizo kama haya, ilhali wahindi na waarabu waliozaliwa hapa wanakabili matatizo kama haya kwa urahisi zaidi?

Mifumo ya Familia na Utajiri wa Pamoja

Moja ya siri kubwa ya mafanikio ya familia za kihindi na kiarabu ni mshikamano wa kifamilia na uzalishaji wa pamoja. Wahindi na waarabu huwekeza katika biashara za kifamilia kwa malengo ya muda mrefu. Mtoto anayesoma hujua elimu yake inatumikia familia na biashara zao. Shahada si tiketi ya kuanza maisha peke yake, bali ni nafasi ya kuchangia ukuaji wa biashara za kifamilia.

Kwa jamii za Kiafrika, hali ni tofauti. Watoto hupewa jukumu la kusoma na baada ya hapo kupambana kivyao. Familia nyingi zimepoteza msingi wa kuendeleza mali na utajiri wa kifamilia kwa sababu kila mmoja anajitahidi kujitegemea mara baada ya kufikia umri wa utu uzima. Hii inaleta changamoto kubwa ya kudumisha maendeleo na ustawi wa kifamilia kwa muda mrefu.

Ushirikiano wa Kaya Moja na Maadili ya Jamii

Familia za kihindi na kiarabu mara nyingi huishi katika makazi yanayowaunganisha wote – mababu, mabibi, wajomba, mashangazi, na hata binamu. Mfumo huu huimarisha maadili na utamaduni wa jamii, huku ukitoa fursa kwa vijana kuiga mifano mizuri ndani ya familia. Watoto hawaishi kutangatanga mitaani, bali wanajifunza kupitia mifano hai ya maisha ya familia zao.

Kwa Waafrika, muundo wa familia pana umekuwa ukipungua. Mifumo ya kijamii ambayo hapo zamani iliwapa watoto mwelekeo sahihi imekufa, na vijana wengi wanakosa maadili na mwongozo wa maisha. Hali hii imechangia kuongezeka kwa changamoto kama madawa ya kulevya na uhalifu, jambo ambalo ni nadra kwa familia za kihindi na kiarabu kwa sababu wanazingatia sana heshima ya familia.

Mafanikio ya Wahindi na Waarabu Ughaibuni

Mfumo huu wa mshikamano wa kifamilia na kibiashara hauishii katika nchi za Afrika pekee. Ukiangalia wahindi na waarabu wanaohamia nchi za Magharibi, utagundua kuwa wanaendelea kuwa na maendeleo makubwa hata huko. Hii ni kwa sababu ya utamaduni wao wa kusaidiana na kuwekeza katika familia. Mtu mmoja akifanikiwa kufika, hufanya kila juhudi kuwasaidia ndugu zake wengine kufika ili kusukuma gurudumu la maendeleo.

Kwa upande mwingine, Waafrika wengi wanapofika Ughaibuni, mafanikio yao huonekana kwa kusimamia masuala ya kifamilia kwa mbali, mara nyingi kupitia kutuma pesa za matumizi au ujenzi wa nyumba nyumbani. Hata hivyo, juhudi za kuwainua ndugu kiuchumi au kuwasaidia kujiendeleza hazipewi uzito unaostahili. Matokeo yake, maendeleo ya kifamilia na kijamii hubaki nyuma ukilinganisha na jamii za wahindi na waarabu.

Kutokomeza Aibu Ndogo Ndogo

Katika familia za Asia, mtu anayepoteza mwelekeo hupewa msaada na nafasi ya kuendelea kuishi bila kudhalilisha familia. Kwa mfano, mtu mwenye matatizo ya uteja anaweza kupewa kazi "geresha" ndani ya familia au biashara, lakini bado anatunzwa. Kwa upande wa Waafrika, mtu kama huyu mara nyingi hukataliwa na familia, akifukuzwa nyumbani na kuishia mitaani. Matokeo yake ni aibu ya kijamii inayowakumba familia nzima.

Je, Tungeweza Kubadilika?

Kwa Waafrika, kuna haja ya kurejesha mshikamano wa kifamilia kwa kushirikiana katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Familia zetu zinapaswa kuanza kuwekeza pamoja na kuondokana na fikra za kila mmoja kupambana kivyake. Tunapaswa kutambua kuwa maendeleo ya mtu mmoja hayatoshi – familia zenye mshikamano zina nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kwa ujumla.

Pia, tunapaswa kuanzisha mifumo ya kuwasaidia wanajamii wetu wenye changamoto, badala ya kuwatelekeza. Tukijifunza kutokana na mifumo ya familia za kihindi na kiarabu, tunaweza kuanza kupunguza ufukara katika jamii zetu na kurejesha heshima na mshikamano wa familia za Kiafrika.

Mwisho wa yote, umaskini si tu tatizo la kiuchumi; ni tatizo la kijamii linalotokana na kuyumba kwa mifumo ya familia. Hatujachelewa kujifunza na kubadilika – tukianza leo, tunaweza kujenga msingi bora kwa vizazi vijavyo.
Umefika India mkuu?.. Au unaongelea familia zipi za kihindi.

Hao waarabu gani unaongelea ww, maana huku mwembechai tupo nao kibao tu wanaungaunga.

#BlackboxThinking
 
Back
Top Bottom