siku moja tulikuwa na mdahalo wa maendeleo chuoni hapa europe na nikawauliza hao facilitators ambao wanatoka mashirika makubwa ya misaada ya ulaya (wazungu) , niliwauliza kwanini nchi zenu za ulaya zinatoa misaada ambayo viongozi wengi wa Afrika wanaitumia kununua mahekalu Paris na kudeposit Swiss na mnajua na mnawaona? je mnatenda haki kwa tax payers wenu kwa pesa yenu kuishia matumbo ya viongozi wa Afrika na mnawaona huku ulaya wakiranda randa 5 stars hotels na convoys zao? na je kuendelea kusaidia Afrika hamuoni kama mnaua jitihada binafsi za Afrika kujikwamua yenyewe bila misaada? manake ukisaidiwa kila siku akili inadumaa na unakuwa tegemezi? wakanijibu hivi: wazungu hawataacha kutoa misaada sababu ni sera yao ya kideplomasia na pia ni kurudisha asilimia moja ya mamilioni ya rasilimali wanazovuna Afrika! this means viongozi wa Afrika ndo wanatukuza wazungu na uzungu zaidi ya wananchi wa kawaida! hawa jamaa walinijibu black and white mbele ya mdahalo! kweli Afrika ni bara la giza! siku itapata viongozi bora watakaokataa utumwa wa mzungu labda miaka 500 ijayo vitukuu wetu wataendelea!
cheki hapa chini mwananchi wa Cameroon akimponda Rais wake anaekula raha Geneva , Switzerland kwenye 5 star hotel juzikati!