GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,024
- 119,543
Nyie Watanzania wenzangu ambao kutwa napata taarifa za kujiua kwenu kwa kukata Tamaa ya Maisha au mnataka sasa na sisi (hasa mimi GENTAMYCINE) niwapeni Historia yangu kubwa ya mapito makubwa niliyoyapitia ya miaka saba mfululizo lakini nilijikaza na kuvumilia yote halafu hata wazo la kujiua (kujitoa uhai kama mfanyavyo) sikuwa nalo?
Au mnadhani kwa kutuona (kutusoma 24/7) hapa JamiiForums basi akina GENTAMYCINE hatuna shida na hatupitii au hatujapitia changamoto kubwa za kimaisha? Naandika huu Uzi kwa Uchungu mkubwa hadi Machozi yananilenga kwani mnakata Tamaa upesi sana huku mkidhani kuwa ni nyie pekee ndiyo mmeandikiwa kuteseka maishani. Naumia sana na maamuzi yenu ya kujiua.
Kitu pekee ambacho GENTAMYCINE nimejifunza na kukigundua pia Maishani ni kwamba kuna wakati Mwenyezi Mungu anaamua kukupa Shida makusudi ili kukupima Imani na Uvumilivu wako lakini pia tambueni ya kwamba kuna nyakati Mwenyezi Mungu anakunyima makusudi ili Kukuokoa na hatari zijazo. Ndiyo maana kila mara nikiwa hapa au hata Uraiani huwa nasema Mwenyezi Mungu ni Fundi.
Kwa mfano nijitolee tu mwenyewe kuwa kwa tabia yangu ya hasa kupenda chini (mbususu) nina uhakika katika miaka yangu saba ya mapito Mwenyezi Mungu angenipa Mafanikio ya Kiuchumi (kuwa na pesa) hakyanani kudadadeki hivi sasa ningeshakuwa marehemu. Hivyo namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniepusha na hilo kwa njia ya kunipa mateso ili akili itulie, nijifunze na anipe nikishakuwa nimebadlika.
Yaani natamani sana maisha yangu ya miaka saba yangu ya mapito ningejua ningekuwa nayarekodi ili nije kuwaonyesheni nyie Watanzania wenzangu ambao mnakata tamaa ya maisha haraka sana halafu mnakimbilia kujiua na wengine mnajiua huku mkiacha watoto wenu bado wadogo wakiwa wanawahitaji kwa ustawi wao mzima pamoja na wake zenu Warembo ambao mliwapenda wenyewe.
Naomba leo niwapeni Silaha zangu kuu ambazo zilinifanya GENTAMYCINE nikomae hivyo nikiwa Taabuni/Shidani na wala kamwe sikuwa na wazo la kujitanguliza mwenyewe kizembezembe kwa Baba Mola (Mwenyezi Mungu) pasipo ridhaa yake kwa kumtumia wakala wake ambaye huwa hana mzaha na hakosei akitumwa kuja kuitwaa roho yako iliyotukuka aitwae Israeli Mnoko.
1. Jikubali kuwa ulikuwa juu na sasa uko chini hivyo utaamka na kujipanga tena
2. Ukiwa na Shida (Msongo) shirikisha Kwanza Rafiki yako mkubwa na wa karibu kuna nafuu utaipata
3. Usiogope kuomba Msaada (hasa wa Pesa) kutoka kwa Mtu/Watu kuwa Utachekwa au Kudharaulika
4. Penda sana Kujichanganya na Wana (Marafiki) lakini pia tembelea Fukwe ule Upepo ni Tiba nzuri Akilini
5. Kama una Access na Internet tafadhali nakushauri tembelea mara kwa mara hapa JamiiForums utapona
6. Kubali Kukosolewa kama kuna mahala Wewe mwenyewe unajua Kibinadamu ulikosea ama kwa Utoto wako au Kiburi chako au Ujeuri wako na hasa Ujinga wako
7. Yote haya ya juu hapa hayatakamilika kama katika Ratiba yako ya kila Siku huwa HUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU kwa IBADA/KUOMBA. Kama kuna SILAHA ambayo inanipa JEURI zote Mimi GENTAMYCINE katika Maisha yangu ya kila Siku hapa duniani basi ni KUSALI SANA na KUJIAMINI pia.
Namalizia kwa kuwaombeni wale wengine ambao nanyi mmekata Tamaa ya Kimaisha tafadhali kabla ya kutaka Kuchukua hatua ya kujiua njoo hapa JamiiForums kisha Uusome huu Uzi wangu GENTAMYCINE uone nilikotoka na nina uhakika utacha hiyo nia na kuendelea kumtumainia Mwenyezi Mungu. Nimeyapitia mengi katika miaka yangu saba ya mapito huenda kuliko hata nyie ila sikuwa Mdhaifu wa kutaka KUJIUA sawa?
Poleni sana kwa CHANGAMOTO zenu zozote zile za KIMAISHA ambazo mnazipitia ila NIWAHAKIKISHIENI kuwa hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho. Mwenyezi Mungu anatujua wote na yale ambayo yako akilini mwetu ila anajua ni wakati gani sahihi wa kutupa na kutufungulia Milango yetu ya BARAKA na nawaomba Mwenyezi Mungu AKIWABARIKI tu tafadhali msiache Kutoa FUNGU LAKE LA KUMI na KUWASADIA na Wengine.
Nawapendeni nyote na ndiyo maana leo nimelazimika kuja na hili na huu USHUHUDA wangu. Mungu anaweza mno tu.
Mbarikiwe nyote kwa Jina la Bwana.