Watanzania mbona hamjahoji uuzwaji wa nyumba za Serikali kwa bei ya kutupwa?

Kwa sasa watanzania (walio wengi) wanasherehekea kutumbua majipu. Naomba niwakumbushe nyumba za serikali ziliuzwa bei ya kutupwa mbona hampigi kelele jipu hilo likatumbuliwa?

2f324d6dd11ff849227a8b6c3cd43cc2.jpg
 
Bavicha mbona hamueleweki, mnasema nyumba zimeuzwa kwa bei ya rahisi, wakati huo huo mnakesha mitandaoni mkiandika kuwa national housing na nssf wanauza nyumba kwa bei hgali sana kiasi ambacho mtanzania wa hali ya chini hawezi kununua. Sasa tuwaelewe kwa lipi?
 
Kwa sasa watanzania (walio wengi) wanasherehekea kutumbua majipu. Naomba niwakumbushe nyumba za serikali ziliuzwa bei ya kutupwa mbona hampigi kelele jipu hilo likatumbuliwa?
Nyumba za Serikali ziliuzwa na Serikali ya Mkapa si mtu wala aliyekuwa waziri mwenye dhamana husika. Maamuzi yote yanayofanywa na Serikali hukubalika kisheria ingawa mass action (negative consensus principle) inaweza ku-overturn maamuzi yoyote ya serikali. Kama hakukuwa na upraising yoyote kupinga maamuzi ya Serikali kuuza nyumba zake inatafsiriwa kuwa wananchi walilidhika (endorsed the policy). Tusipoteze muda kwenye fitna, tusonge mbele.
 
Kwa sasa watanzania (walio wengi) wanasherehekea kutumbua majipu. Naomba niwakumbushe nyumba za serikali ziliuzwa bei ya kutupwa mbona hampigi kelele jipu hilo likatumbuliwa?

Ziliuzwa na Rais wa awamu ya ngapi na leo tuko awamu ya ngapi? na kwa nini hukuhoji kwa rais aliyeuza au aliyefuatia? huna hoja. Na chadema mwaka huu mtarukia kila tawi na hamponi.
 
Mtu akishakuwa kiongozi wa nchi tunatakiwa tumheshimu na kumheshimu ni pamoja na kutokuanza kufungua mabaya yake hata kama tunayajua.Huyu ni kiongozi mkuu mapungufu yake madogo madogo yawekwe kando kwanza,tumkosoe kwa haya ya sasa.Umenielewa???

kwani ziliuzwa kwa amri ya nani? na lini? achana nao hao.
 
Sioni tatizo kwa serikali kuuza hizo nyumba na ni kweli nyumba hizo nyingi ni zile zilizotaifishwa na serikali kutokana na azimio la arusha....bei ya kutupwa maana yake nini?kama zingeuzwa kwa bei ya juu..mtanzania gani unaelalamika ungepata fursa ya kumiliki?lazima tukubali kuwa uuzaji wa mali za serikali una taratibu zake cha muhimu ni kujiuliza kuwa Taratibu zilifuatwa?mamlaka husika zilikubaliana na kushirikishwa?vinginevyo hizi taarifa tunaweza kuzifasiri kama figisu za kuzuia kasi ya utendaji wa serikali ya awmu ya tano
 
Sheria ya manunuzi inaonesha juu ya taratibu za kufuatwa katika procurement and disposal of govt assets. So kama sheria inaruhusu kudispose gvt assets na nyumba ni moja ya hizo assets, sidhani kama kuna watu watachukuliwa hatua...
 
WEWE NDIO WALE WALE WA NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO, KWA HERI
 
Sheria ya manunuzi inaonesha juu ya taratibu za kufuatwa katika procurement and disposal of govt assets. So kama sheria inaruhusu kudispose gvt assets na nyumba ni moja ya hizo assets, sidhani kama kuna watu watachukuliwa hatua...
Kufikiri kwa ni finyu sana. Unalinganisha nyumba na kuuza gari lililotumika miaka 10, nyumba iliyopo Posta mpya for example, kwa milioni mbili eti taratibu zimefuatwa. Jinga we
 
Kwa sasa watanzania (walio wengi) wanasherehekea kutumbua majipu. Naomba niwakumbushe nyumba za serikali ziliuzwa bei ya kutupwa mbona hampigi kelele jipu hilo likatumbuliwa?
Kwani kelele uliyoipiga wewe katika hili bandiko lako haikuridhishi mpaka ualike watu wengine wakusaidie? Kila mtu atajikuna pahala anapoona panamwasa. Ukiona watu hawaongei lolote kuhusu suala hilo maana yake siyo agenda yao kwa sasa. Hata hivyo kuna baadhi ya mambo huchuja baada ya muda na ukumbuke pia ajenda ya nyumba ilitumika kuanzia kitambo baadaye kwenye mchujo wa ccm na hatimaye uchaguzi mkuu lakini haikuonekana lolote na jamaa kakalia kiti. Basi fanya watu wapige kelele, kwa hiyo nani atazifanyia kazi hizo kelele zenu? Rais?
 
Zilishajengwa maelfu kibao , hakuna kuhoji hapo, mbona huoji kwa nini serikali imejenga nyumba kibao ?
 
Kwa sasa watanzania (walio wengi) wanasherehekea kutumbua majipu. Naomba niwakumbushe nyumba za serikali ziliuzwa bei ya kutupwa mbona hampigi kelele jipu hilo likatumbuliwa?

Kijana, wakati mzee Sumaye anatangaza nia ya kugombea urais, Mbunge wa sasa wa Ubungo kupitia Chadema, Said Kubenea alimuuliza swali kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali. Unataka kujua Kamanda Sumaye alijibu nini? Mtazame hapa;

Kuna swali lingine?!
 
Lowasa na Sumaye nao walinunua, umeshawauliza nani aliwauzia?
We ndio wale wale wa Ndioooooooooooooooooooooooooooooooooooooo, ishu siyo hawo uliowataja, ishu ni kuuza nyumba iliyopo Sea View kwa milioni mbili, for example!
 
Kijana, wakati mzee Sumaye anatangaza nia ya kugombea urais, Mbunge wa sasa wa Ubungo kupitia Chadema, Said Kubenea alimuuliza swali kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali. Unataka kujua Kamanda Sumaye alijibu nini? Mtazame hapa;

Kuna swali lingine?!

Sijafungua clip, whatever the answer he gave that time, ishu unawezaje kuuza nyumba, say, iliyo posta mpya kwa milioni 10 for example eti serikali imeruhusu. The whole government is corrupt and should not exists
 
Back
Top Bottom