Waswahili katika kupinga ukoloni wa Wabelgiji Burundi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,806
31,820
WASWAHILI KATIKA KUPINGA UKOLONI BURUNDI

Historia ya Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi inashangaza.

Hakuna Sheikh katika Afrika ya Mashariki aliyeweza kuingia Belgian Congo, Rwanda na Burundi kumpita Sheikh Hassan bin Ameir akieneza Uislam na wakati huo huo kwa ujanja mkubwa akiwafunza wanafunzi wake mbinu za siasa.

Waislam wa Congo, Rwanda na Burundi walikuwa wamebaguliwa na Wabelgiji wakawanyima elimu.
Wabelgiji waliweka elimu yote katika mikono ya Wamishionari.

Waislam wa Burundi wenyewe wakijiita Waswahili.

Ingawa Wamishionari walikuwapo Tanganyika na wakifanya shughuli zao kwa msaada mkubwa wa serikali, tofauti baina ya Nyasaland, Belgian Congo, Rwanda na Burundi ni kuwa Tanganyika Waislam walikuwa wengi na wingi huu kwa namna moja ulipunguza uzito wa matatizo yao.

Sheikh Hassan bin Ameir aliwashauri Waislam wa Burundi waunde jumuiya ya Waislam.

Waislam wa Burundi wakaunda taasisi iliyokuwa ikijulikana kama Association Scolaire Musulmane du Ruanda-Urundi kwa kifupi ASMARU.

Chama hiki kilijikita zaidi katika suala la elimu kwa Waislam na lilishughulika sana katika kupeleka serikalini madai ya Waislam kuhusu kupunjwa elimu wakidai wapewe ‘’subventions,’’ yaani ruzuku kama wafuasi wa dini nyingine ili na wao waweze kujenga shule zao.

Waislam walipoona juhudi zao zote hizi zinagonga ukuta wakaona waombe msaada kwa kutoka kwa ndugu zao Waislam wa Tanganyika kupitia kwa Sheikh Hassan bin Ameir kama walivyofanya Waislam wa Machame.

Waislam wa Burundi wakapata msaada na wakajenga shule moja ambayo hadi leo ipo Barabara ya Nane na ya Tisa, Buyenzi na inajulikana kwa jina la Jumuiyya.

Sheikh Hassan bin Ameir alialikwa aje Burundi kuifungua shule hii na ipo hadi leo.

Katika juhudi na harakati hizi taatifa za kikachero zikafikishwa serikalini kuwa Sheikh Hassan bin Ameir kutoka Tanganyika ndiye aliyekuwa akiwachochea Waislam wa Burundi dhidi ya Wabelgiji.

Haiyumkini kabisa kuwa Sheikh Hassan bin Ameir atakuwa kaingiliana na watu wa Burundi kwa kiasi ile ikawa yeye hawaelezi hali ya siasa ya Tanganyika na vipi Warundi kwa kiasi kile cha kuwawezesha kujenga shule asifunze na mbinu za siasa za mapambano.

Vyama vya siasa vilipoanza Burundi viongozi wa vyama hivi walikuja kuwa karibu sana na TANU kutokana na msingi huu alioweka Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam hawakusita kujiunga kwa wingi katika vyama hivi.

Viongozi wa vyama hivi wakawa wanaiangalia TANU na viongozi wake kama taa ya kuwaangazia kwenye kile kiza chao chini ya Wabelgiji na walihangaika sana kutaka na wao watiwe katika ‘’Panafricanisme,’’ kama Warundi walivyoita yaani, Pan African Freedom Movement in East and Central Africa (PAFMECA).

(Kutoka ''Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama'' (2020) na Mohamed Said)

 
Kwani waswahili ni waislam ? Mjomba acha kutudanganya bhana waswahili ni neno la dharau kuitwa mtu kwa mfano kama mtu mweupe (mzungu) kumuhita mtu mweusi nigger huko uraya na marekani . Hivyo mswahili hausiani neno sheikh . Sheikh ni cheo kwenye dini ya islam
 
Kwani waswahili ni waislam ? Mjomba acha kutudanganya bhana waswahili ni neno la dharau kuitwa mtu kwa mfano kama mtu mweupe (mzungu) kumuhita mtu mweusi nigger huko uraya na marekani . Hivyo mswahili hausiani neno sheikh . Sheikh ni cheo kwenye dini ya islam
Wamba...
Naomba kwanza kabisa tufahamiane.
Mimi napenda mjadala wa kiungwana na wa kistaarabu.

Tutumie lugha zinazopendeza.
Asiwe mtu anaingia katika mjadala kwa ajili ya kushambuliana.

Swali la kwanza umeliuliza vizuri.
Kwani Waswahili ni Waislam?

Neno, ''mjomba,'' hukustahili kuniita hivyo.

Kisha ukaendelea, ''Acha kutudanganya.''
Maneno kama haya hayapendezi.

Lugha za ''bhana,'' kwangu si mahali pake ikiwa ni lazima utumie maneno kama hayo basi isiwe kwangu mimi tumia kwa wengine.

''mzungu,'' Mzungu.
''muhita,'' muita.

''uraya,'' Ulaya.
''marekani,'' Marekani.

''dini ya islam,'' dini ya Kiislam.
Ukumbi huu ni mahali pazuri kwa mtu kujifunza na kupata elimu.

Tuutumie vyema ili tupate faida na maarifa.
 
Back
Top Bottom