Wasiobadili umiliki wa vyombo vya moto wapewa siku 13

Mowwo

JF-Expert Member
Aug 15, 2015
1,043
1,583
Wakuu
Walee tunaonunua ndinga mikononi mwa watu bila kubadili umiliki tumefikiwa.
TRA imesema kuanzia January 20 itaanza kutumia mfumo unaoitwa IRAS ambao hautaruhusu alieuziwa chombo cha moto kubadili umiliki, badala yake alieuza chombo hicho ndiye atakua na uwezo wa kubadili umiliki pekee
Maswali
Siku 13 pekee zinatosha?
Walio mbali na access za TRA watabadili vipi kwa haraka?

Source; Mwananchi
 

Attachments

  • Screenshot_20250107_193225_Instagram.jpg
    Screenshot_20250107_193225_Instagram.jpg
    405.6 KB · Views: 11
Wakuu
Walee tunaonunua ndinga mikononi mwa watu bila kubadili umiliki tumefikiwa.
TRA imesema kuanzia January 20 itaanza kutumia mfumo unaoitwa IRAS ambao hautaruhusu alieuziwa chombo cha moto kubadili umiliki, badala yake alieuziwa chombo hicho ndiye atakua na uwezo wa kubadili umiliki pekee
Maswali
Siku 13 pekee zinatosha?
Walio mbali na access za TRA watabadili vipi kwa haraka?

Source; Mwananchi
Screenshot_20250107-221456.jpg

Unakielewa ulichoandika hapa??
 
Ni sh ngapi kubadili?
KWA GHARAMA TU

1. Swali: Chombo cha moto ni nini?
Jibu : Ni chombo kinachotumika katika usafirishaji ardhini, ambavyo ni pamoja na Magari, pikipiki na bajaji.

2. Swali: Nikitaka kununua gari kwa mtu taratibu zipoje?
Jibu : Unapaswa ufike ofisi ya TRA na picha ya pasipoti ya muuzaji, ripoti ya ukaguzi kutoka kwa trafiki, barua ya muuzaji kuhusu mabadiliko ya umiliki wa gari, picha yako ya pasipoti, kadi halisi ya gari, hati ya kiapo ya muuzaji, gari kufika TRA kwa ajili ya ukaguzi, mkataba wa mauziano uliothibitishwa na mwanasheria na upewe risiti ya EFD kutokana na huduma ya kisheria.

3. Swali: kumwakilisha mtu kwenye taarifa za uhamishaji wa chombo unaruhusiwa?
Jibu : Ndiyo kwa kampuni au taasisi unaruhusiwa kwa mwakilishi kuleta idhini maalum ya kisheria (Power of Artoney) ya kuthibitisha uwakilishi wake lakini kwa mtu binafsi anapaswa awepo mhusika mwenyewe.

4. Swali: Gharama ya kuhamisha umiliki wa gari ni shilingi ngapi?
Jibu : Ada ni shilingi 50,000 + ada ya nakala ya kadi ni shilingi 50,000 +ushuru wa stempu ambayo ni 1% ya bei ya gari.

5. Swali: Gharama ya kuhamisha umiliki wa bajaji, Je?
Jibu : Ada ni shilingi 27,000 + ada ya nakala ya kadi shilingi 30,000 , ambapo jumla ni shilingi 57,000.

6. Swali: Gharama ya kuhamisha umiliki wa pikipiki nao upoje?
Jibu : Ada ya uhamisho ni shilingi 27,000 + ada ya nakala ya kadi shilingi 20,000, ambapo jumla ni shilingi 47,000.

7. Swali: Kuna ulazima wa kubadilisha taarifa za umiliki TRA?
Jibu : Ndiyo, unapaswa kubadili taarifa za chombo TRA ili umiliki uhame kutoka kwako kwenda kwa mtu mwingine la sivyo kuna athari zinaweza kutokea.

8. Swali: Athari za kutobadili umiliki au taarifa ya chombo cha moto ni zipi?
Jibu : Athari zinazoweza kutokea ni
(i) Mmiliki wa awali anaweza kuwajibishwa endapo chombo kitatumika kwenye uhalifu.
(ii) Mmiliki mpya atakosa malipo ya fidia kutoka bima.
(iii) Mmiliki mpya atakosa uhalali wa kutumia chombo hicho kama dhamana ya kukopa.
(iv) Mmiliki awali atawajibika endapo mmiliki mpya atakopa kwa kutumia chombo hicho.

C & P
 
Back
Top Bottom