Wasifu wa Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Mhandisi John William Kijazi

hana lolote zaidi yakuiba CCM hawawezi hata dakika moja kufanya jambo lenye faida zaidi ya wizi tu
 
Kijazi1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 6 Machi 2016, akichukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue.

Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mhandisi Kijazi alikuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.

Vilevile, hadi uteuzi wake, Balozi Kijazi amekuwa Mkuu wa Mabalozi wa Afrika nchini India ambaye amekuwa mtetezi mkuu wa wanafunzi wenye asili ya Kiafrika nchini India.

Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India. Kati ya mwaka 1996 hadi 2002.

Mhandisi Kijazi alikuwa Mhandisi Mwandamizi wa Ujenzi wa Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa Barabara za Mikoa ndani ya Wizara hiyo hiyo.

Balozi Mhandisi Kijazi alipata Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Umma mwaka 1982 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Barabara Kuu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza mwaka 1992.

Balozi Mhandisi John Kijazi amemuoa Fransiscar Kijazi na pamoja wamejaliwa watoto watatu, David, Emmanuel na Richard Kijazi.

Balozi Mhandisi John Kijazi ameapishwa leo tarehe 7 Machi 2016 na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es salaam.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, 07 Machi 2016.
 
Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mhandisi Kijazi alikuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.
Vilevile, hadi uteuzi wake, Balozi Kijazi amekuwa Mkuu wa Mabalozi wa Afrika nchini India ambaye amekuwa mtetezi mkuu wa wanafunzi wenye asili ya Kiafrika nchini India.
Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India. Kati ya mwaka 1996 hadi 2002.
Mhandisi Kijazi alikuwa Mhandisi Mwandamizi wa Ujenzi wa Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa Barabara za Mikoa ndani ya Wizara hiyo hiyo.
Balozi Mhandisi Kijazi alipata Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Umma mwaka 1982 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Barabara Kuu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza mwaka 1992.
Balozi Mhandisi John Kijazi amemuoa Fransiscar Kijazi na pamoja wamejaliwa watoto watatu, David, Emmanuel na Richard Kijazi.
Balozi Mhandisi John Kijazi ataapishwa leo tarehe 7 Machi 2016 na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es salaam.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa, 07 Machi 2016.
 
Tuna imani naye.... ila CCM ni ile ileeeee awe makini sana...
 
Umesahau amezaliwa tarehe 18 Novemba, 1956. Hivyo tarehe 18 Novemba, 2016 atafikisha miaka 60.
 
CURRICULUM VITAE

NAME:
John William Herbert Kijazi
BORN: 18 November 1956
AGE: 59
MARITAL STATUS: Married
CHILDREN: Has three sons

EDUCATION
  • Bachelor of Science (Honours) in Civil Engineering, University of Dar es Salaam, Tanzania
  • Masters of Science in Highway Engineering, Birmingham University, UK
CAREER
  • 1982 – 1986 Assistant Executiver Engineer, Ministry of Public Works, Tanzania
  • 1986 – 1996 Regional Engineer, Ministry of Public Works, Tanzania
  • 1996 – 1999 Senior Road Maintenance Engineer, Ministry of Public Works, Tanzania
  • 1999 – 2002 Director of Regional Roads, Ministry of Public Works, Tanzania
  • 2002 – 2005 Permanent Secretary, Ministry of Public Works, Tanzania
  • Jan – Nov 2006 Permanent Secretary, Ministry of Infrastructure Development, Tanzania
  • Dec 2006 – Jun 2007 Special Duties, Minstry of Foreign Affairs and International Cooperation HQTS, Tanzania
  • Jun 2007 High Commissioner to India
  • 27 May 2013 High Commissioner to Singapore
LANGUAGES
English, Swahili

Vs

Chief Secretary Roles
As Parmanent Secretary of the President
Chief Secretary is the Permanent Secretary of the President. In that position, he is the CEO of the Office of the President. In addition, he is the head of the Public Service and Secretary to the Cabinet of Ministers.Duties of the Chief Secretary include:

  1. Advise the President on matters relating to discipline and employment in the Public Service..
  2. Receive and deal appropriately with reports from various committees of the Commission and the President as well as the Public Service Commission.
  3. Address the operational issues of TISS and PCCB.
  4. Provide a link between the President and the MDAs on all matters pertaining to the implementation of various issues concerning the Government and the country in general.
  5. Advise the President on all matters pertaining to the operation of government and the country in general.
  6. Undertake any work that the President shall assign.

Kuelekea 2020 na gurudumu la Maendeleo.
 
Huyu bwana ukiangalia record yake....amekuwa mtusmishi wa umma kwa mda mrefu na hakubebwa popote. Kila lakheri ndugu Kijazi. Na ukiangalia kwa umakini sidhani kama Huyu bwana ni mtu wa "system". Ni outsider kabisa.
Hawezi kukosa kuwa mtu wa system.
 
Ngosha hana utani ni lazima atakuwa anafahamu utendaji wake wa kazi ndiyo maana. Kassim Majaliwa hakuna mtu alitarajia atachaguliwa lakini Ngosha anafahamu utendaji wake wa kazi. Ule muda wa kuleana umepita mjomba.

Ni wewe kweli
 
Mbona historia ya Kijazi haikamiliki . Haionyeshi alizaliwa wapi na alisoma wapi msingi na secondary?
 
Back
Top Bottom