Wasanii wetu na mtego wa tuzo za kimataifa

Mkuu unazunguka sana .... we sema tu "Ni kwanini mashabiki wa Kiba sasahivi wanazikodolea tuzo''. Basi
 
Katika tuzo zote anayepata kihalali ni platnumz peke yake. Sababu ndo tunaona rotation ya nyimbo zake mpaka nje ya africa na anafanya show kibao africa hii. Lakini hawa wengine tuzo wanazopata ni kutokana na ulimbukeni wa watz kupenda kukesha 24/7 wanapiga kura. Tena kwa mtu ambae hastahili.
Chuki mbaya mkuu .Fanya research usije na fact za za tandale kwa tumbo.
 
Pole sana naona ile ya sound city aliyoshinda kiba imekuuma sana?? Mbona mondi kashinda sana na hamkutoa tathmini hzo??
Watanzania tu wanafiki sana,miaka miwili ilopita tulikua tukiomba tuwe na wasanii wengi wa kutuwakilisha kimataifa baada ya diamond kuwa peke yake,amekuja kiba anajitahidi anashinda tunzo mbalimbali lakini cha kushangaza kuanzia media,blogs na watanzania tumemsusa utadhania Ali kiba ni mkenya ndo kwanza tunaendesha kampeni za kumvunja moyo
Swali langu,Mlitaka diamond pekee ndiye ashinde hizo tunzo??
Safi sana ndugu yangu Watz ni wanafiki sana .Ali kiba anatoboa wanajifanya hawaoni wanaanza majungu
 
Ali Kiba ashaimba na R Kelly sasa wewe unataka nini tena?
 
Safi sana ndugu yangu Watz ni wanafiki sana .Ali kiba anatoboa wanajifanya hawaoni wanaanza majungu

Ali Kiba anatoboa wapi? Acheni kumjaza ujinga huyu mswahili wenu ni heri ungesema navy kenzo au vanessa. Huyo kiba ata rwanda tu hapo hakuna mwenye time nae nyie mnafikiri kura zenu zitampa show
 
Team kariakoo shimoni 24/7 simu mikononi cjui wanakula saa ngapi kipya kinyemi
 
Tomaso akasema "sitaamini mpaka niyashike makovu take".

"Emanicipate yourself from mental enslavement. Non but ourselves can free our mind" Robert Nesta Marley.
 
Huu ndiyo ukweli, Alikiba ameshinda Tuzo nyingi sana mwaka 2016, Wapinzani hawajakubali kabisa au hawajaamini kama jamaa anadeserve.. Mara waseme analilia Tuzo, Mara za Mchangani, Mara hastahili, Mara wengine EATV AWARDS hawakushiriki kwa vile za kujiandikisha, Mara Ben Pol alistahili!

Kama umewahi kusoma hesabu za probability: Ni kwamba kuwa tu nominee katika Awards inamaanisha wewe una nafasi sawa ya kushinda, ishu ni nani ana vigezo zaidi! Kwa hiyo kama ALIKIBA alishinda Tuzo MTVEMA, BEFFTA, WANAcorp, SOUNDCITYMVP, ASFA n.k na bado amepata nafasi ya kuperfom MTV MAMA, KENYA NA CHRISS BROWN, UGANDA, NIGERIA. HUwezi kufanikiwa siku moja! Yaani huyo huyo Alikiba ametoa Collabo na Sauti sol, Ommy, mziwanda, Baraka, Blue, Mauzo na Bado ana Mengine ya kumstress! Ifike kipindi anayeshinda tumheshimu.

swali la kujiuliza ukimtoa Alikiba, Vanessa na Diamond kwa 2016, Ni Msanii gani ambaye wewe unadhani anastahili kupata Tuzo za kimataifa??????

Issue siyo kwamba jamaa wanataka kutangaza Tuzo zao, hapana ni kawaida kabisa! Sema unayemfahamu toka mdogo huwezi kumthamini kama yule aliyemjua akiwa staa.

kwa kifupi Tujitahidi kusapoti wasanii wetu wote
 
Kwa kuwa kapata KIBA imekufanya uone zinapatikana kirahisi eeh? Hamna tuzo inayopatikana kirahisi ila anayeipata anastahili kuipata.
 
Kwa kuwa kapata KIBA imekufanya uone zinapatikana kirahisi eeh? Hamna tuzo inayopatikana kirahisi ila anayeipata anastahili kuipata.

Mkuu, tatizo Kiba alijiharibia mwenyewe kwa kujifanya supastaa na mjuaji. unakumbuka wakati Diamond anazipata tuzo, yeye alikuwa anaziponda. alikuwa anajitapa kuwa yeye ni mkubwa kuliko tuzo.

hii maana yake nini, maana yake ni kwamba kiba alionyesha dharau kuwa tuzo si lolote. kwa hiyo haishangazi hata inapotokea leo anapata yeye wengine tunamshangaa, kulikoni leo na yeye naona tuzo ni tamu wakati mwenzie anazipata yeye alizipondea.

afterall, Mi linapokuja suala la tuzo, kwa Diamond ndo huwa nafuatilia na kutilia maanani zaidi, kwa sababu Diamond yeye alionyesha kuzijali tangia mwanzo.

ndo ushangae sasa, kiba pamoja na kuziponda tuzo na kujiona yeye ni mkubwa kuliko tuzo, leo anadiriki kwenda kujaza fomu ili apate tuzo. sasa hayo majigambo yake leo kiko wapi.?

binafsi nikisikia kiba kapata tuzo hata huwa sifuatilii kwa sababu ya jeuri yake, ila akipata Diamond hata kama ni uchochoroni lazima niishadadie.
 
Hoja ya kupata mialiko sio kigezo pekee cha mwanamuziki kukubalika sehemu Fulani. Kuna baadhi ya nchi watu wake ni wanunuzi wazuri wa kazi za wasanii kuoitia mitandao kama iTunes, tidal n.k na huko tunao wasanii wa tz wanaofanya vizuri kwenye mauzo ya kazi zao.
 
Back
Top Bottom