Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,515
- 10,828
Uzi mfupi tu kuhusu soko la sanaa Tanzania. Wasanii wetu wa muziki ni muda wa kutoka usingizini sasa na kufanya kazi zinazoenda Duniani kama Wanaija.
Nimeandika huu uzi baada ya kuona kazi mpya ya Asake - WHY LOVE hii imefuatana na kazi mpya ya Diamond Platnumz - Moyo. Ukisikiliza hizo kazi mbili unaweza kuhisi Asake yupo kwenye game la muziki kumshinda DP.
Wanaija walipotuacha ni kwa kufanya kazi za Kimataifa zaidi kwa kuzingatia ubora wa muziki: wimbo wenyewe, video production na promotion. Siku kadhaa Asake ali-trend kuwa anatoka na Inda Love, siku kadhaa mbele India Love yupo kwenye video ambayo imetendewa haki. Soko la muziki kwa sasa lipo sehemu moja tu "Ardhi ya D. Trump". Huwezi kuwa unafukuzia Grammy wakati upo Tandale.
Asake ndani ya miaka miwili baada ya kuachia video ya PBUY, jana ameachia video kali sana na hii inaonyesha ni kwa jinsi gani analitafuta soko la Marekani kwa kuboresha kazi zake. Huwezi kuonekana unafanya vitu serious kwa production team za hapa nyumbani na huu ndiyo ukweli. Huko Duniani watu wamenyooka sana: watu kama Cole Bennett, Gibson Hazard ukiangalia video zao ule muziki unajihisi kama vile na wewe uwe sehemu ya video hiyo.
Huku ndiyo Wanaija wanapotukimbiza, Wizkid, Asake, Tems wanaonyesha jinsi gani Marekani inawafungulia milango.
Kitu kingine muhimu, wasanii wetu hawajui jinsi ya kuji-brand. Ukifungua IG page ya Diamond Platnumz utakutana na ma-post kibao utasema ni Mwandishi wa Habari, uki-scroll unakutana na mambo ya chama, basi tu tafrani. Lakini ukifuatilia wasanii wa Kimataifa kutoka Naija wapo "straight to the point" utakutana na posts za kazi zao latest na picha kadhaa kwa mpangilio wa kuvutia.
Diamond Platnumz ana pesa, connections, potential. Inashangaza kuona anaanza kupotea taratibu, kile kipindi cha Hallelujah, African Beauty, Jeje ndiyo alikuwa peak sasa ameanza kurudi nyuma tena.
Hizi hapa chini ni YouTube za wasanii Diamond Platnumz na Asake, angalia uone utofauti katika uwasilishaji wa kazi.
1. Diamond Platnumz
2. Asake