Usisome mstari mmoja tu wa Biblia ukaishia hapo. Soma Maandiko haya kwa makini ujue ni kina nani walioambiwa wakiacha kumsifu Yesu MAWE yatapaza sauti(yatapiga kelele).
Luka 19:28-40
Na alipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akipanda kwenda Yerusalemu. Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi, akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa. Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji. Na wale waliotumwa wakaenda wakaona kama alivyowaambia. Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda? Wakasema, Bwana ana haja naye. Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda, wakampandisha Yesu. Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani. Hata alipokuwa amekaribia matelemko ya mlima wa Mizeituni, kundi zima la wanafunzi wake walianza kufurahi na kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya matendo yote ya uwezo waliyoyaona, wakasema, Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; amani mbinguni, na utukufu huko juu. Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, uwakanye wanafunzi wako. Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele."
Umeona? Waliokuwa wakimsifu Yesu katika tukio hilo ni kundi zima la Wanafunzi wa Yesu. Mafarisayo walipomwambia Yesu awakanye waache kumsifu ndipo alipowajibu "wakinyamaza hawa[wanafunzi], mawe yatapiga kelele."
Jiulize sasa, je hao wanafunzi wa Yesu wanaotajwa hapo walikuwa wazinzi? Walikuwa walevi?
Mungu hapendezwi na watu vuguvugu.
Ufunuo 3:16 SRUV
Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
TUBU LEO