Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 2,651
- 3,607
Naongea na nyinyi mnaojiita wasanii wa nyimbo za Injili (Gospel Artists), vikundi vya kwaya na bendi. Nyinyi mnaotunga na kuimba nyimbo za Injili, nyimbo za sifa na kuabudu lakini maisha yenu ni ya mchanganyo! Maisha ya uvuguvugu. Nyinyi mnaopenda kumwimbia Mungu lakini dhambi hamtaki kuziacha. Mnaimba sana kwenye matamasha ya Injili, kanisani na kwenye mikutano ya Injili, lakini hamtaki kuacha matendo haya ya kidunia yaliyoandikwa katika Wagalatia 5:19-26 BHN
Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: Uzinzi, uasherati, ufisadi; kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano; husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo.
Kwa kufanya hayo mnasababisha Jina la Mungu linatukanwa. Kwa kutenda hayo, tambueni leo kwamba nyimbo zenu ni kelele mbele za Mungu, na wala hataki kusikia sauti za vinanda vyenu.
Amosi 5:23 SRUV
Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu.
Basi, tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kutoka kwake Bwana(Matendo 3:19).
Mkitubu na kurejea kikamilifu, nyimbo zenu zitapata kibali mbele za Mungu.
Yeyote anayesikia maneno haya bila kuyazingatia na kuyafanya, anafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa(Mathayo 7:24-27)
Blessed and wise is the one who receives the message of this thread with discernment and applies it with diligence.