Waraka maalum kwa Prodyuza DONCHA na Maprodyuza wote Tanzania ili kuboresha Muziki wa Tanzania

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
WARAKA MAALUM KWA PRODYUZA DONCHA.

NILIJIIMARISHA KIMUZIKI NA UIMBAJI ULIO BORA KWA KUTUMIA BEAT YA AINA YOYOTE ILE MWAKA2014 KWA PRODYUZA "DONCHA" WA MWANZA.(DJ. DON NALIMISON)

Producer DONCHA nilimfahamu kupitia Gabriel Samalu(Mlapa) wa Global Publisher mwaka 2014 nanikafanya Albam yangu iliyoitwa "AGANO JIPYA" ikiwa ni albam ya Pili 2014 kwani ie ya kwanza iliyoitwa "USIUNYANYAPAE MOYO WANGU (Bongofleva) niliitoa mwaka 2003)2004 chini ya JAPANTECH-DAR ES SALAAM.

Bw. DONCHA nitofauti na Producer Marijani aliyenigongea beat ya NIMEPATA DEMU mwaka 2003 studio za Backyard Namanga Kona, vocal na mixing zilifanywa na Producer Hingi. Hata hivyo DONCHA nitofauti na Producer Seiblast wa Sei Record ya Kinondoni studio-Dar ambaye ndiye alinitengenezea beat na mixing ya nyimbo kadhaa 2004/2005 ikiwemo USIUNYANYAPAE MOYO WANGU, lakini pia DONCHA anakuwa tofauti na Prodyuza KGT ambaye 2004/2005 studio za Flex record Kinondoni studio-Dar alikuwa akifurahia uimbaji wangu tu baada ya kufanya kazi moja nikishirikiana na Msanii TOMMY GADUI aliyekuwa best yangu Sana wakati huo. Lakini DONCHA anakuwa tofauti Sana na Prodyuza Sam wa Njenje Studio za Morocco-Dar aliyenitengenezea beat na mixing 2005 ya wimbo wangu PESA UKO WAPI(Marimbastyle) na kukimbia na wimbo wangu katika studio za Fabric record zilizokuwa Kinondoni pia. Lakini DONCHA anakuwa tofauti kabisa na Maprodyuza wa kilokole walionitengenezea beat kwa kinanda na mixing katika wimbo wangu NIA NINAYO mwaka 2005 Kariakoo-Dar kwenye jengo la jeshi.

Mimi DJ. DON NALIMISON Japo Mwanza2016 nilikutana pia na Prodyuza Nelly wa Mapango studio, Mkuyuni Magorofani na kufanya naye kazi ya Vocal tu kwa beat yangu binafsi. Hata hivyo Bw. DONCHA alikuwa studio moja na Prodyuza D.Class baadae walitengana na DONCHA akiwa nyamanoro nikiendelea kufanya naye kazi mpaka 2017. Nilipofungwa mwaka2018 na nilipotoka gerezani Juni2020 nilimtafuta Sana bila mafanikio ili tuanze kusuka Album yangu mpya ya kwanza katika lugha ya Kiingereza (HipHop/RnB) lakini hakupatikana kabisa. Nilikutana na Prodyuza Ghost wa Action studio Kahama-Shinyanga mwezi July2020 nikafanya naye nyimbo moja(Goodbye) ambayo niliirudia upya baadae jijini Mwanza katika studio za City of Studio. Baada ya kumsaka Sana DONCHA bila mafanikio nikaingia Mkataba na Prodyuza HPal wa City of Sound Mwanza Julai2020 na kufanya kazi 6 za awali. Ikiwemo Congratulation, Innocent, African Prison, Dear Mama n.k ambazo Sasa nimezirekodi upya kwa studio yangu binafsi(DJ. DON NALIMISON STUDIOS ambapo zamani ilikuwa MUSICPRESS). Hii Ni kutokana na uvurugaji uliofanywa na Maafisa wa Serikali kuingilia Mambo yangu binafsi ya KIMUZIKI na Maisha yangu wakishirikiana na Maaskari magereza Fulani na Mwanajeshi Fulani hivi, hivyo Nili block kila kitu mwaka huu 2021 na kuanza upya baada ya binafsi kujiimarisha Kiproduction kwa audio na video na graphics.

DONCHA aliniweka sawa Sana katika kufuata beat lakini besi yangu bado ilikuwa tatizo kwake maana alitaka niimbe Kama kina Mondi, Mo Music yaani sauti zile zilizozoeleka za kubana pua. Nilimkatalia Sana, ilibidi anifuate ninavyotaka kwa besi yangu, tulielewana Sana na hata nilipokosea au kuvuruga aliniweka Sana na wakati mwingine hata kurekebisha Melody(tune) ili Muziki uwe vizuri. Nilimfurahia Sana Bw. DONCHA kipindi hicho. Lakini ilifikia hatua akigonga beat anashangaa Melody naibadilisha kwenye kuingiza vocal na wimbo bado unakuwa Bora Sana. Siku kwa siku nakijiona naimarika zaidi kuliko Maprodyuza wote niliowahi kufanya nao kazi.

Kutokana na style yangu ya Muziki kutokubalika katika lugha ya Kiswahili ndipo nikaanza kuimba kwa Kiingereza kuanzia mwak 2016 nikijifua zaidi binafsi kwani style yangu kwa Kiswahili Haina ladha Ila kwa Kiingereza au kifaransa au Kifilipino au Kiitaliano lugha ambazo pia najua kuzungumza ndizo style yangu ya Muziki inakubalika Sana.

Pamoja na kwamba Sasa Mimi DJ. DON NALIMISON ni Prodyuza wa Muziki na pia Prodyuza wa Filamu na kazi zangu zote nafanya mwenyewe hapahapa nyumbani Kahama-Shinyanga (Shunu) lakini bado namkubali Sana Bw. DONCHA. Mimi Sina Mke Wala Sina mtoto hata mmoja nipo nyumbani naishi na mama yangu mzazi na ndipo napofanyia kazi zangu zote.

Kimsingi lazima umkubali mtu aliyekuonesha njia nzuri japo Bw. DONCHA alikuwa hafurahii uimbaji wa besi. Bw. DONCHA popote ulipo Mungu akubariki Sana. Shakira ni Mwanamke aliyesumbuka Sana kukubalika kutokana na kubuni style yake binafsi lakini Leo style yake imemuokoa.

Ndimi DJ. DON NALIMISON
KAHAMA-SHINYANGA
20 OKTOBA,2021.
Call +255 689 16 55 22.

InShot_20211017_130746751.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom