Wapinzani wa Rais Samia waanza kutumia silaha ya Uzushi na uongo kumshambulia baada ya njia zao kushindwa.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
25,989
19,051
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia ni mtu anayeishi mbele ya wakati na muda na kiongozi Mwenye akili na upeo wa hali ya juu sana,ni mtu Mwenye jicho la tatu nje na haya mawili ya kibinadamu.ni kiongozi aliyejaliwa macho ya Rohoni yenye uwezo wa kuona asipoweza kuona Mwenye macho ya kawaida.

Ni kiongozi mwenye ufunuo wa kiroho wa kutambua masuala mbalimbali.ndio maana huwezi ukaona akikurupuka wala kuhemuka wala kuzungumza jambo hadharani bila staha. Ni mtu mtulivu,makini na mwenye kuchunga ulimi wake kabla na wakati wa kuzungumza.huwezi ukaona akijikwaa hovyo ulimi wake na kuleta taharuki au mgawanyiko ndani ya Taifa.

Alipokuwa anaingia na kutwaa madaraka ya urais kuna watu hawakuamini mioyoni mwao kama anaweza kuongoza Taifa letu kwa hata mwezi mmoja tu.walitamani kama wangekuwa na mamlaka au uwezo basi wangemuweka pembeni na kumuacha na Umakamu wake na wao kuweka mtu wao.waliona ni kama hastahili wala hafai wala hana huo uwezo wala hakuandaliwa kwa nafasi hiyo.

Lakini Mungu katika ulimwengu wake wa kiroho tayari alikuwa amemuandikia kwa wino usiofutika kuwa Mama Samia atainuliwa na kuwa Rais wa Taifa letu.Ndio maana pamoja na watu kuleta habari za ubaguzi kwa misingi ya jinsia na ukanda. Kumzushia mambo ya uongo, uchonganishi,fitina na chuki binafsi.bado Rais wetu ameendelea kuaminika ,kuungwa mkono ,kupendwa na kukubalika sana machoni pa watanzania ,huku Taifa likiendelea kutamalaki kwa amani na utulivu mkubwa sana.

Jambo ambalo linawaumiza sana waliokuwa hawana Imani na Rais wetu na waliokuwa wakitamani kutokuona akiwa Rais wetu.Lakini kubwa na linalowapa homa ni kuona namna watanzania wanavyohitaji kwa kiu kubwa sana kuona Mama huyu mzalendo na kipenzi cha watanzania akiendelea na muhula wa pili kama Rais.

Sasa ili kumkwamisha ,kumkatisha tamaa,kumchonganisha na wananchi,kumvunja moyo,kumchafua na kumpunguza kasi .sasa wabaya na wapinzani wa Mama yetu wameona watumie silaha yao ya mwisho ambayo nayo imeonekana kutokuwa na nguvu kabisa, ya kuzusha mambo ya uongo, uchonganishi na maneno ya fitina na chuki binafsi.na ndio mwisho wao mbaya sana utakaowapoteza kabisa katika ramani ,kwa sababu watanzania wameshatambua njia hiyo ya kumchafua Rais wetu mpendwa. Hakuna silaha ya aina yoyote ile itakayoinuka na kufanikiwa mbele ya Rais wetu mpendwa.kila kitu kitashindwa na mwisho Rais wetu itaendelea kuwa shujaa wetu na jasiri Muongoza Njia.

Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
1718963337489.png
 
MAELEZO MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) AKIWASILISHA USHAHIDI WA VIELELEZO KWA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. TULIA ACKSON (MB) KUHUSU WAZIRI WA KILIMO MHE. HUSSEIN MOHAMED BASHE (MB) KUSEMA UONGO BUNGENI LEO TAREHE 14 JUNI 2024.

MHE. SPIKA,

MANENO YA UTANGULIZI

Itakumbukwa kuwa Mnamo Tarehe 4 Juni 2024, wakati wa mjadala wa kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2024/2025, uliniagiza nilete ushahidi wa kuonyesha namna ambavyo Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe (Mb) amelidanganya Bunge wakati akichangia hoja hiyo kuhusu suala la sukari. Nanukuu sehemu ya maagizo ya Mheshimiwa Spika Dk. Tulia Ackson (Mb).

“Kwa hiyo, Mheshimiwa Mpina wewe ulikuwa unasema Waziri alete ushahidi, sasa mimi nitauhitaji ushahidi kutoka kwako wa kuonyesha namna ambavyo Waziri anadanganya……..jambo

lingine nilikuwa nimemuelekeza Mheshimiwa Mpina kwa mujibu wa Kanuni ya 70 kwamba yeye athibitishe yale aliyosema Waziri amesema uongo, Kanuni ya 70 (6) inataka apewe muda na mimi nampa mpaka tarehe 14 Juni 2024 ” mwisho wa Kunukuu.

Kufuatia maagizo ya Kiti nalazimika kuandaa Maelezo na kuwasilisha kwa Mheshimiwa Spika leo Tarehe 14 Juni 2024 nikiwasilisha ushahidi wa vielelezo vya kuthibitisha uongo wa Waziri Bashe aliousema Bungeni tarehe 4 Juni 2024.

Hotuba ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe (Mb) katika Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2024/2025 alisema Wizara kupitia NFRA ilitoa idhini ya uingizaji wa sukari tani 410,000 ambapo uingizaji wa sukari umeanza Januari 2024 na utakamilika ifikapo Disemba 2024.

WAZIRI WA KILIMO MHE. HUSSEIN MOHAMED BASHE (MB) KUSEMA UONGO BUNGENI

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe wakati akichangia hoja ya Waziri wa Fedha kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Bungeni alisema uongo mara 18, kama ilivyoainishwa katika maelezo na ushahidi wa vielelezo. Pia Maelezo hayo ya uongo yanaweza kufanyiwa rejea kwenye Hansard ya Bunge ya tarehe 4 Juni 2024 (Kiambatisho Na. 1).

2.1 Maelezo ya Waziri kwamba mwaka jana (2022/2023) nchi hii ilikuwa na Gap Sugar ya tani 60,000 walimpa Kagera Sugar, walimpa Mtibwa, walimpa Bagamoyo, walimpa TPC hakuna aliyeagiza hata Kilo 1. Hii sio kweli amesema uongo.

Maelezo na uthibitisho: Uongo wa Waziri uko katika maeneo yafuatayo:

Gap Sugar iliyoidhinishwa kwa msimu wa mwaka 2022/2023 ni Tani 30,000 tu na si tani 60,000 kama alivyosema Waziri wa Kilimo. Rejea Barua ya Bodi ya Sukari Tanzania yenye Kumb.Ref.No.SBT/DGO/26-38 ya tarehe 29 Machi 2023 iliyoandikwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari, Prof. Bengesi kwenda kwa Katibu Mtendaji wa TCS SADC (Kiambatisho No.2)

Viwanda vya wazalishaji wa sukari nchini na wafanyabishara waliingiza nchini tani 6,801 na hivyo si kweli kwamba hakuna kilo hata moja iliyoingia mwaka 2022/2023 kama alivyosema Waziri wa Kilimo. Rejea Ripoti ya CAG (Mashirika ya Umma) ya mwaka 2022/2023 ukurasa wa 174 (Kiambatisho
Na. 3)

Wenye viwanda walipewa vibali vya kuagiza tani 2,500 kwa kila mmoja ambapo ni sawa na tani 12,500 ambapo vibali vyake vilitoka Tarehe 3 Mei 2023 na kuishia tarehe 30 Juni 2023, hivyo viwanda vingi vilishindwa kuagiza sukari kutokana na muda mfupi wa vibali na kwamba uzalishaji viwandani ulikuwa umekaribia kuanza. Hivyo sio kweli kwamba wenye viwanda walipewa vibali vya tani 60,000 na wakashindwa kuingiza sukari. Rejea kibali SR No. 3153403174 (Kiambatisho Na. 4)

2.2 Maelezo ya Waziri kwamba wameenda kubadili Kanuni za National Food Reserve Agency kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuagiza Sukari. Hayo ni Maelezo ya uongo.

Maelezo na uthibitisho: Hadi sasa hakuna GN yoyote ya Serikali inayoonyesha kutungwa kwa Kanuni mpya za NFRA kuruhusu shirika hilo kuagiza, kusambaza na kuuza sukari nchini. Kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2024 Kanuni hizi ndiyo zinapendekezwa kurekebishwa.

2.3 Malalamiko ya Waziri kwamba waliwapatia wazalishaji wa sukari wa ndani walete Tani 50,000 mpaka mwezi Februari walikuwa hawajaleta hata kilo moja ya sukari.

Maelezo na uthibitisho: Si sahihi kulalamikia kutoingizwa kwa sukari kufikia mwezi Februari wakati Waziri anajua vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi vilitolewa na Bodi ya Sukari kati ya tarehe 4 hadi 8 Januari 2024 ambapo wenye viwanda walipewa kibali cha kuagiza tani 10,000 kila mmoja, hivyo isingewezekana ndani ya wiki 2 sukari iwe imeshaagizwa na kuingizwa nchini kwani huhitajika wastani wa zaidi ya siku 60 hadi siku 90 kuagiza na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi. Hivyo malalamiko ya Waziri yalikuwa ni ya uongo rejea vibali SR No. 6568448093 na 9178437615 (Kiambatisho Na. 5)

Hata hivyo hadi kufikia tarehe 31 Mei 2024 jumla ya tani 49,884 zimeshaingizwa nchini na wazalishaji sukari kutokana na vibali vya kuingiza tani 50,000 walivyopewa mwezi Januari 2024 ambapo sukari hiyo imesambazwa sehemu mbalimbali nchini.

2.4 Maelezo ya Waziri kwamba Viwanda 7 vya sukari vya nchi hii viliweka Taifa la watanzania milioni 61 kwenye mikono yao, na walivyowapa kibali cha kuingiza sukari wamekaa Disemba hakuna kilo 1 iliyoingia, Januari hakuna kilo 1 iliyoingia mwishoni mwa Januari wameingiza tani 250 wakati wakifahamu Sugar na buffer stock ya mwaka wa nyuma wa uzalishaji hawakuingiza hata kilo 1 kwa hiyo taifa lilikuwa halina sukari.

Maelezo na uthibitisho: Waziri amesema uongo katika

maeneo yafuatayo:-

Haiwezekani Disemba na Januari kuingiza sukari wakati vibali kuingiza sukari kwa wenye viwanda vya sukari na wafanyabishara wasio na viwanda vilitolewa na Bodi ya Sukari kati ya tarehe 4 hadi 30 Januari 2024.

Katika Msimu wa 2022/2023 wenye viwanda na wafanyabishara waliingiza sukari tani 6,801 kati ya Gap Sugar ya tani 30,000 iliyokuwa inahitajika hivyo sio kweli kwamba mwaka anaoutaja Waziri kwamba makampuni hayakuingiza hata kilo 1 na taifa lilikosa sukari kwa sababu Gap sugar ya kutosha haikuingia nchini ni maelezo ya uongo.

2.5 Maelezo ya Waziri kwamba, hivi sasa (tarehe 4 Juni 2024) viwanda vilikuwa havijaanza uzalishaji sasa projected Gap Sugar mwanzo wa uzalishaji mwaka jana mwezi wa tatu, tuli project kwamba tutakuwa na Gap Sugar tani 140,000 na 150,000.

Maelezo na uthibitisho: Sio kweli kwamba hadi tarehe 4 Juni 2024 viwanda vilikuwa havijaanza uzalishaji kwani Kiwanda cha Kagera Sugar kilianza tarehe 27 Mei 2024, Kiwanda cha TPC kilianza uzalishaji tarehe 1 Juni 2024 na Kilombero Sugar kilianza tarehe 3 Juni 2024.

2.6 Maelezo ya Waziri kwamba, uzalishaji ukashindikana katika nchi yetu kuanzia Oktoba, Novemba, Disemba, Januari, Februari na Machi ambayo ni hali ya kawaida ya uzalishaji lakini leo (Juni 4, 2024) tunavyoongea Aprili hakuna uzalishaji, Mei hakuna uzalishaji kwa hiyo taifa letu halina uzalishaji wa sukari kwa miezi 8.

Maelezo na uthibitisho: Maelezo hayo ni ya uongo kwani miezi aliyoitaja Waziri wa Kilimo, viwanda vingi vilikuwa vinazalisha sukari isipokuwa miezi ya mvua nyingi za El Nino ambapo uzalishaji ulipungua na baadhi ya viwanda vilisimamisha uzalishaji mwezi Disemba na Januari tu na sio miezi 8 anayosema Waziri. Rejea Taarifa ya TSPA inayoonyesha uzalishaji wa Sukari mwaka 2023/2024 ambapo uzalishaji ulifikia tani 394,829 (Kiambatisho No.6)

2.7 Maelezo ya Waziri kwamba, Wastani wa matumizi ya sukari katika nchi yetu tunakula tani 1,500 kwa mwezi tunakula tani 45,000 simple mathematics tani 45,000 mara 8 ni zaidi ya tani 350,000 karibu tani 360,000 sasa kwanini tumeidhinisha ziada kufikia tani 410,000 kawaida tunapofika mwezi wa 3 mwakani always ni lazima tunaposimamisha uzalishaji tuwe na buffer ya miezi 2 hivi ndivyo hesabu zinavyofanyika.

Maelezo na uthibitisho: Waziri alidanganya katika maeneo yafuatayo:

Kwa vielelezo vya Bodi ya Sukari na TSPA zinaonyesha kuwa mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 490,000 na hivyo kwa mwezi ni kati ya tani 38,000 hadi 41,000 na sio tani 45,000 alizosema Waziri.

Kuanzia mwezi Mei 2023 mpaka mwezi Aprili 2024 viwanda vilikuwa vinafanya kazi isipokuwa baadhi ya miezi uzalishaji ulipungua, baadhi ya viwanda vilifungwa kutokana na mvua za El Nino na kupisha ukarabati.

2.8 Maelezo ya Waziri kwamba anataka atoe mfano kidogo wa Kagera, Kiwanda cha Kagera Sugar kiko Kagera pale Bukoba wilaya ya Misenyi nini kinatokea, mlaji aliyeko Missenyi anakula almost the same na mlaji aliyeko Nzega.

Maelezo na uthibitisho: Waziri amesema uongo na anakinzana na bei elekezi iliyotangazwa na Ofisi yake, kwani haijazingatia hicho alichosema, kupitia Tangazo la Serikali Na. 40B la tarehe 23 Januari 2024 ambapo wananchi wa Missenyi bei ya rejareja ya sukari kati ya Tsh. 2,800 hadi 3,200 huku wananchi wa Nzega wakipewa unafuu zaidi wa bei kati ya Tsh 2,800 hadi Tsh. 3,000 kwa kilo. Hivyo madai ya Waziri wa Kilimo alipaswa ayazingatie katika kuandaa Bei elekezi (Kiambatisho Na. 7)

2.9 Maelezo ya Waziri kwamba mfumo wote wa distribution ni cartel system msambazaji mmoja tu yuko Mwanza anahudumia mikoa 11.

Maelezo na uthibitisho: Haya maelezo hayana ukweli wowote kwa kuwa uzalishaji na usambazaji wa sukari nchini hufanyika katika misingi ya ushindani na kila kiwanda kinao wasambazaji wake na sio mmoja kama alivyodai Waziri. Kagera Sugar inao wasambazaji 24 katika wilaya na mikoa mbalimbali nchini (Kiambatisho No. 8), Hata hivyo kama kuna matatizo ya usambazaji Waziri alipaswa kukaa na viwanda kuyatatua na sio kulalamika katika majukwaa ambayo hayahusiki.

2.10 Maelezo ya Waziri kwamba, Serikali ya Chama cha Mapinduzi italinda walaji, Wakulima, viwanda na wafanyabiashara.

Maelezo na uthibitisho: Ni kweli kabisa hilo ndilo lengo la Chama cha Mapinduzi na imewekwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020. Hata hivyo, matendo na kauli za Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe haziendani na azma hiyo ya Chama na Serikali.

2.11 Maelezo ya Waziri kwamba ni lazima Serikali ifanye intervention na sisi tumefanya intervention na wao nimewaambia njooni mezani tuongee tukubaliane, tuheshimu Taifa hili.

Maelezo na uthibitisho:

Waziri hakusema ukweli, kwani hajawaita wazalishaji wa sukari ili akae nao kujadili changamoto zinazowakabili, badala yake ni wazalishaji wa sukari waliomba kuonana na Waziri. Kupitia barua yenye Kumb Na. Ref:TSPA/SI-Gen/27/01/2024 ya Tarehe 14 Februari 2024 iliyoandikwa na Katibu Mtendaji wa TSPA, Deo Lyatto kwenda kwa Waziri wa Kilimo. (Kiambatisho Na. 9)

Kupitia Bodi ya Sukari Waziri wa Kilimo aliwajibu wazalishaji wa sukari nchini kwamba atakutana nao pale tu wazalishaji sukari watakapokuwa wamekamilisha kutekeleza masharti waliyopewa na Wizara ya kujenga maghala kila mkoa na wasambazaji kuwatangaza hadharani na Kampuni ya Kagera Sugar kumfuta Uwakala Ndugu VH Shah.

Rejea barua yenye Kumb. Na. Ref. No.SBT/DGO/01/33-33 ya Tarehe 20 Machi 2024. Iliyoandikwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari, Prof. Bengesi kwenda kwa TSPA (Kiambatisho

Na.10)

Baada ya Wazalishaji kuona Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe hana utayari wa kukutana nao kujadili changamoto zao wamelazimika kuomba kuonana na

Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kumwelezea changamoto walizonazo katika tasnia ya sukari, kupitia barua yao yenye Kumb. TSPA/SI-Gen/27/02/2024 ya Tarehe 22 Mei 2024 iliyosaniwa na Wakurugenzi Watendaji wa Viwanda 5 vya Sukari nchini (Kagera, Kilombero, TPC, Bagamoyo na Mtibwa). (Kiambatisho Na.11)

2.12 Maelezo ya Waziri kwamba mwezi Januari na Februari nchi hii sukari ilifika Shilingi 10,000 sio ya kweli kwani,

Katika uchunguzi wangu hakuna soko wala kijiji wananchi walinunua sukari kwa shilingi 10,000 kwa kilo, isipokuwa bei ilipanda na kufikia kati ya shilingi 4,000 mpaka 6,000 kwa kilo kwa baadhi ya maeneo nchini, kutoka bei iliyokuwepo ya wastani wa shilingi 2,800 mpaka shilingi 3,000 kwa kilo. Bodi ya Sukari hadi sasa imeshindwa kuthibitisha bei hiyo ya Shilingi 10,000 kwa kilo iliuzwa wapi. Hivyo Waziri kusema bei ya sukari ilifika shilingi 10,000 ni uongo.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA KATIKA UAGIZAJI WA SUKARI NJE YA NCHI

Kama nilivyosema awali kuwa uagizaji holela wa sukari nje ya nchi ulidhibitiwa tangu mwaka 2017 na baada ya marekebisho ya Sheria ya Sukari mwaka 2020 ambapo ni wenye viwanda vya sukari pekee waliruhusiwa kuagiza Gap Sugar na kiasi kinachoagizwa ni nakisi ya sukari pekee (Gap Sugar) na kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa sukari na kupunguza kwa kiasi kikubwa nakisi ya sukari kutoka tani 144,000 mwaka 2017 hadi tani 30,000 tu mwaka 2023 na inatarajiwa kuondoka kabisa nakisi ya sukari kufikia mwaka 2025. Rejea taarifa ya TSPA ya uzalishaji wa sukari na Gap Sugar ya 2015/2016 hadi 2023/2024 (Kiambatisho Na. 12)

Hatua anazozichukua Waziri wa Kilimo tangu ateuliwe zinalenga kuua tasnia ya sukari na hatua nyingine anazochukua ni kinyume cha Sheria, kinyume na Mpango wa Taifa ya Maendeleo na Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kwamba inaleta hofu kwa uwekezaji unaoendelea wa uzalishaji wa sukari na Wakulima wa miwa.

Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-

3.1 Wizara ya Kilimo imetoa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi tani 410,000 ambapo Tani 50,000 wamepewa wenye viwanda vya kuzalisha sukari nchini na tani 360,000 wamepewa wafanyabishara wasio na viwanda vya sukari nchini wakati nakisi ya sukari (Gap Sugar) iliyopendekezwa na Timu ya Kiufundi ya Bodi ya Sukari (TAC) na kupitishwa Bodi ya Sukari (SBT) mwaka 2023/2024 ni tani 100,000 tu kwa ajili ya mwezi Januari hadi Juni 2024. Hii ziada ya sukari ya tani 310,000 imeagizwa kwa ajili ya nini? sukari hiyo itapelekwa wapi wakati viwanda vimeshaanza uzalishaji katika msimu wa mwaka 2024/2025. Mhe. Waziri wa Kilimo aliongozwa na nini hadi kuruhusu vibali vinavyozidi viwango vya mahitaji kutolewa? Maamuzi haya yanaleta mashaka makubwa juu ya kukosekana kwa uzalendo, uadilifu na uhalali wa ugizaji wa sukari nje ya nchi.

Hata hivyo uzalishaji wa sukari wa ndani mwaka 2023/2024 ulifikia tani 394,829 sawa na upungufu wa tani 95,171 ikilinganishwa na mahitaji ya sukari ya nchi ya tani 490,000 kwa mwaka. Hivyo hakuna sababu za msingi Wizara na Bodi ya Sukari kutoa vibali vya ziada ya sukari tani 310,000. Pia uzalishaji wa sukari katika viwanda vya ndani mwaka 2024/2025 ulishaanza tangu tarehe 27 Mei 2024.

Maamuzi haya ya Waziri wa Kilimo ni kinyume cha Sheria ya Sukari Na 6 ya Mwaka 2001 na marekebisho yake ya mwaka 2020 yaliyofanyia marekebisho kifungu cha 14 cha Sheria ya Sukari na Kanuni zake ambazo zinataka sukari inayoagizwa kutoka nje ya nchi iwe ni ile ya nakisi ya sukari (Gap Sugar) tu na si vinginevyo (Kiambatisho Na. 13) na kiasi hicho kiwe kimethibitishwa na kamati ya ushauri wa kiufundi (TAC) ya Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) baada ya kupitia mahitaji na uzalishaji wa sukari nchini.

3.2 Wizara ya Kilimo na Bodi ya Sukari kutoa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi tani 360,000 kwa wafanyabiashara wasio na viwanda nchini ni kinyume na Kifungu cha 14 cha Sheria Sukari Na 6 ya mwaka 2001 na marekebisho yake ya mwaka 2020, Waziri wa Kilimo na Bodi ya Sukari hawana mamlaka ya kutoa vibali nje ya utaratibu uliowekwa kisheria.

3.3 Bodi ya Sukari ilisajili Makampuni kuingiza sukari ambayo hayakuwa na sifa kisheria na Makampuni hayo hayakuwa na rekodi yoyote ya kujihusisha na biashara ya sukari na pia uwezo wao wa kifedha ni wa kutiliwa mashaka jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Sukari.

Baadhi ya Makampuni machache yaliyopewa vibali vya kuingiza sukari nchini ambayo hayana viwanda vya kuzalisha sukari nchini ni kama ifuatavyo:-

3.3.1 ITEL EAST AFRICA LIMITED ambaye Bodi ya Sukari ilimuandikia barua yenye Kumb. Ref. No. SBT/DGO/09/VOL.II/2-10 ya tarehe 2 Januari 2024 iliyosainiwa na Lusomyo Buzingo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi wa Sukari ikiitarifu kampuni hiyo kuwa Serikali imeidhinisha kuingiza tani 50,000 za sukari (Kiambatisho Na. 14).

Lakini tarehe 9 Januari 2024 na tarehe 30 Januari 2024 Kampuni ya ITEL ilipewa vibali vya kuingiza tani 60,000 za sukari zaidi ya kiwango ya kiwango kilichoidhinishwa kwenye barua rejea kibali SR Na. 8652445335 na 944600548 (Kiambatisho Na. 15)

Pia vibali alivyopewa ITEL ni zaidi ya viwanda vyote vitano ambavyo jumla vimepewa tani 50,000 tu kwa maana ya tani 10,000 kila kiwanda.

Baada ya kufanya upekuzi wa BRELA tarehe 10 Juni 2024 (Kiambatisho Na. 16) ilibainika kuwa:-

Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED imesajiliwa Tarehe 15 Februari 2013 yenye ofisi zake Ilala, Dar es Salaam, Kwa ajili ya biashara za kuuza rejareja simu, komputa, TEHAMA na vifaa vingine vya mawasiliano na sio biashara ya sukari.

Wizara ya Kilimo na Bodi ya Sukari wameipa kampuni ya ITEL kuagiza sukari wakati ni kampuni ya kuuza simu na Kampuni hiyo haina uwezo, ujuzi na weledi wa masuala ya sukari na hivyo inaweza kupelekea kuingiza sukari isiyo na ubora, kufanya udanganyifu, kukwepa kodi na kuliingiza taifa katika migogoro ya Kibiashara kimataifa.

Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED 49% ya hisa zinamilikiwa na raia wa India

Viwanda vya ndani vinavyolipa kodi, soko la Wakulima wa miwa na kutoa ajira kwa watanzania wengi vimeachwa na kipaumbele kupewa Makampuni binafsi.

Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED ina hisa za kawaida 1000 zenye thamani ya Tsh. 50,000,000

Kampuni hii ina mtaji mdogo na sijaona ushahidi wa kuongeza mtaji na hivyo haiwezekani kupewa kazi ya zaidi ya Tsh. Bilioni 160 kwa mara moja, nimefuatilia Financial Statements za mwaka 2020, 2021, 2022, 2023 inaonyesha Kampuni inafanya biashara ndogo na haina uwezo mkubwa kifedha. Kitendo cha kupewa vibali vya kuagiza sukari kwa mara moja zenye thamani ya Tsh. Bilioni 160 kupitia Kampuni hii inaweza ikawa ni utakasishaji wa fedha haramu, kufanya udanganyifu na kukwepa kodi.

Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED ilihuisha taarifa zake Tarehe 19 Februari 2024 siku chache baada ya kupewa barua na vibali vya kuingiza sukari nje ya nchi kati ya tarehe 9 na 30 Januari 2024. Pengine ilikuwa kutafuta sifa za ziada.

Barua ya Bodi ya Sukari yenye Kumb. Ref. No. SBT/DGO/09/VOL.II/2-10 ya tarehe 2 Januari 2024 iliyoijulisha Kampuni ya ITEL kuruhusiwa kuagiza sukari nje ya nchi haionyeshi kama Kampuni hiyo iliwahi kuomba kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi. Haya ni matumizi mabaya ya madaraka na inaweza kuwa kula njama kuiibia Serikali (organized crime).

Hata hivyo zipo taarifa kuwa Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LTD inatumiwa na Kampuni ya MOHAMMED ENTERPRISES (T) LTD. kwa mgongo wa nyuma kuagiza sukari nje ya nchi kwa niaba yake. Taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonyesha kuwa mzigo wa sukari wa Kampuni ya ITEL ukifika bandarini unatolewa na Kampuni ya METL rejea nyaraka za kuondoa mzigo Bandarini za TRA (Kiambatisho Na.17), pia ziko taarifa za uhakika kuwa baada ya mzigo kutolewa Bandarini unapelekwa kwenye ICD ya Mohamed Enterprises na kutoka ICD sukari inapelekwa kwenye Godown za Mohamed Enterprises na baadaye kuuzwa rejareja na jumla rejea risiti ya TRA ya EFD Na. 32 ya tarehe 22 Februari 2024 na risiti yenye verification code na.28630946606 ya tarehe 23 Februari 2024. Iliyotolewa na Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) LIMITED (Kiambatisho Na.18)

Mahusiano ya kibishara baina ya Kampuni ya MOHAMMED ENTERPRISES (T) LTD na ITEL EAST AFRICA LTD hayako wazi na yanaweza ikawa ni mkakati wa kutakatisha fedha haramu na kukwepa kodi za Serikali.

3.3.2 Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED ambaye amepewa Kibali cha kuagiza sukari Tani 2,500 cha tarehe 22 Juni 2023 (Kiambatisho 19), na kibali hiki kilitolewa wakati uzalishaji wa viwanda vya ndani ulikuwa umeshaanza.

Baada ya kufanya upekuzi wa BRELA (Kiambatisho Na. 20) tarehe 10 Juni 2024 ilibainika yafuatayo:-

Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED ilisajiliwa Tarehe 28 Oktoba 2010 yenye ofisi zake Ilala, Dar es Salaam inayojishughulisha biashara za stationary, huduma za upishi wa vyakula (event catering) na usafi wa mazingira na sio biashara ya kuagiza sukari nje ya nchi.

Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED ina hisa za kawaida 1000 zenye thamani ya Tsh. 1,000,000

Kwa mapungufu haya usingetarajia Bodi ya Sukari itoe kibali na Kampuni hii ambayo suala la kuagiza sukari sio sehemu ya biashara zake na hata hisa inazomiliki zenye thamani ya Tsh. 1,000,000 kwa hali ya kawaida Kampuni hii haina uwezo wa kuagiza tani 2,500 kwa mara moja zenye thamani ya USD 2,500,000 sawa na Tsh. Bilioni 6.6. maamuzi haya ni matumizi mabaya ya madaraka na unaweza ukawa ni utakasishaji wa fedha haramu.

3.3.3 Kampuni ya Yasser Provision Store

Kampuni hii imepewa kibali Na. 9043487787 cha tarehe 2 Aprili 2024 kuingiza sukari nchini tani 10,000 nchini (Kiambatisho Na.21) na kibali kimetolewa kwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo na sio kwa sababu nchi ina upungufu wa sukari. Rejea barua ya Bodi ya Sukari yenye Kumb. Na. SBT/DGO/C/13-23 ya Tarehe 29 Aprili 2024 iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari, Prof. Bengesi kwenda kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato.
(Kiambatisho Na.22)

Baada ya kufanya upekuzi wa ZBPRA na BRELA (Kiambatisho Na. 23) tarehe 13 Juni 2024 ilibainika yafuatayo:-

Kampuni hii imesajiliwa Wakala wa Usajili Biashara na Mali Zanzibar (ZBPRA) Tarehe 5 Januari 2016 na baadaye ilisajiliwa na BRELA na tarehe 4 Januari 2024 na kufungua Ofisi Mtaa wa Nyasubi, Kahama, Shinyanga.

Baada ya kupata usajili wa BRELA tarehe 4 Januari 2024, tarehe 29 Aprili 2024 akapewa kibali cha kuingiza tani 10,000 za sukari.

3.3.4 Kampuni ya ZENJ GENERAL MERCHANDISE COMPANY LIMITED

Kampuni hii ilipewa kibali No. SR No. 3925349484 cha kuingiza sukari nchini tani 60,000 tarehe 30 Aprili 2024 (Kiambatisho 24)

Baada ya kufanya upekuzi wa BRELA (Kiambatisho Na. 25) tarehe 10 Juni 2024 ilibainika yafuatayo:-

Kampuni hii haijawasilisha BRELA Financial Statements tangu mwaka 2016 hadi 2023 miaka 8 sasa. Kiufupi kampuni hili haliko hai na haliwezi kufanya biashara na Serikali.

Kampuni hii imesajiliwa Zanzibar lakini haijahuisha taarifa zake katika Mfumo wa Online Registration System (ORS) wa BRELA.

Kampuni hii imepewa vibali zaidi ya viwanda vyote 5 vinavyozalisha sukari nchini ambavyo vilipewa tani 10,000 kila kiwanda. Lakini pia uwezo wa kifedha wa kampuni hii ni wa kutilia mashaka kupewa kazi ya zaidi ya Bilioni 160.

3.3.5 Mohamed Enterprises (T) Limited

Upekuzi ulifanyika BRELA (Kiambatisho Na. 26) tarehe 11 Juni 2024 Kampuni hii hisa zilizotolewa hadi sasa ni 300,000 tu kati hisa 2,500,000 sawa na 12% tu ingawa taarifa za fedha (Financial Statements) za mwaka 2018 hadi 2023 zinaonyesha kuwa Kampuni ina mtaji mkubwa na kutosha kuendesha biashara kubwa.

3.4 Kusamehe kodi ya Import Duty 35% na VAT 18% kwa sukari inayoagizwa kutoka nje ya nchi tani 410,000 wakati viwanda vya ndani havijapata msamaha huo wa kodi hali itakayopelekea kuzorota na kufungwa kwa viwanda vya ndani kutokana na kutokuwepo ushindani wa haki na usawa. Pia msamaha wa VAT unaharibu utaratibu wa ulipaji wa kodi na kuvifanya viwanda vya ndani kulipa kodi zaidi.

Kusamehe 53% ya kodi katika tani 410,000 za sukari zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, Serikali itapoteza mapato wastani wa Dola za Marekani Milioni 217.3 sawa na Tsh. Bilioni 580. Hivyo kwa msamaha huu Serikali itapoteza mapato ya Tsh. Bilioni 580.

Kwa vibali vya tani 410,000 vilivyotolewa wafanyabishara watapata faifa kubwa (Super Abnormal Profit) ya jumla ya Bilioni 465. Mfano sukari iliyonunuliwa na kuingizwa nchini kwa bei ya USD 575 kwa tani na kuuza nchini kwa wastani wa USD 1000 kwa tani na kwa kuwa hakuna kodi yoyote wafanyabishara walipata faida ya USD 425 kwa kila tani 1 ya sukari.

Changamoto katika maamuzi haya ni kama ifuatavyo:-

Waziri wa Fedha na Waziri wa Kilimo hawana mamlaka kisheria kusamehe kodi iliyowekwa na Sheria zilizotungwa na Bunge. Haya ni matumizi mabaya ya madaraka na ni uhujumu uchumi wa nchi.

Hapakuwa na sababu za msingi za kusamehe kodi, kwani bei ya sukari nje ya nchi haikuwa kubwa kiasi cha kuhitaji msamaha. Hivyo msamaha huu uliombwa kuwanufaisha wafanyabiashara na sio wananchi.

Sukari ya nje imefutiwa kodi ya VAT, lakini viwanda vya ndani vya sukari vinatozwa VAT na kwa kuwa sukari inayoagizwa ni zaidi ya mahitaji, viwanda vya ndani havitaweza kushindana na hivyo kupelekea kuzorota na kufungwa na nchi kupata hasara kubwa.

Hapakuwa na usimamizi wa bei nchini kwani hata pale sukari ilipopatikana kwa bei ndogo nje ya nchi bado iliuzwa kwa kubwa hapa nchini ambapo mfuko wa Kilo 50 uliuzwa Tsh. 145,000. Rejea risiti Na. ya TRA ya EFD Na. 32 ya tarehe 22 Februari 2024 na risiti yenye verification code Na.28630946606 ya tarehe 23 Februari 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Limited katika ofisi za Dar es Salaam.

Mawaziri hawa walitengeneza uhaba wa sukari, kutoa vibali vya kuagiza sukari zaidi ya mahitaji, kuruhusu sukari inayoingizwa kwa msamaha wa kodi kuuzwa kwa bei kubwa kinyume cha sheria. Pia msamaha huo wa kodi unapelekea Serikali kupoteza mapato ya Tsh. Bilioni 580 na kuwawezesha wafanyabiashara kupata faida ya ziada zaidi ya Tsh. Bilioni 465. Kwa maoni yangu hizi ni njama zilizosukwa na baadhi ya Viongozi na watendaji wa Serikali kuiba mapato ya nchi.

3.5 Kuandaa na kutangaza bei elekezi ya sukari mwaka

2024, hatua hii imekuwa na changamoto zifuatazo:-

Bodi ya Sukari ilitangaza bei elekezi kupitia Tangazo la Serikali 40B la Tarehe 23 Januari 2024 toleo Na. 3, lakini katika Hotuba ya Waziri wa Kilimo ya Bajeti ya Mwaka 2024/2025 anaripoti kuwa Wizara ilitangaza bei elekezi ya Sukari nchi nzima kupitia Gazeti la Serikali Na. 3 Toleo la 105 la Tarehe 23 Januari 2024. GN ambayo haipo mahala popote kwenye vitabu vya Serikali.

Wizara na Bodi ya Sukari hazikuwashirikisha wenye viwanda na Wakulima wa miwa katika mchakato wa kuandaa bei elekezi ya sukari iliyotangazwa na Bodi ya Sukari kupitia Tangazo la Serikali (GN) Na. 4OB ya Tarehe 23 Januari 2024 Toleo Na 3. Hii ni kinyume na Kifungu cha 11 A cha Sheria ya Sukari kinachotaka kabla ya kutangaza Bei elekezi Bodi ya Sukari itawashirikisha wenye viwanda vya sukari na Wakulima wa miwa ili kupata gharama sahihi za uzalishaji zitakazosaidia kutengeneza mjengeko wa bei na kujenga msingi wa kupata bei elekezi. (Kiambatisho Na. 27)

Pia Wizara na Bodi ya Sukari walishindwa kusimamia bei elekezi waliyoitangaza wenyewe ambapo wafanyabishara hawakuizingatia bei elekezi hiyo. Licha ya misamaha ya kodi 53% ya sukari kutoka nje ya nchi bado wananchi waliuziwa sukari kwa bei kubwa na wanaendelea kuuziwa sukari kwa bei ya rejareja kubwa kati 3,500 mpaka 4,000 kwa kilo kwa baadhi ya maeneo kinyume na bei elekezi iliyowekwa.

Wizara na Bodi ya Sukari kuchelewesha vibali vya kuagiza Gap Sugar nje ya nchi na kusababisha uhaba wa sukari na kuchochea kupanda kwa bei ya sukari.

Kwa muda mrefu kumekuwa na utulivu wa bei ya sukari na sukari kupatikana muda wote, Bei ya rejareja ya sukari katika kipindi cha miaka 7 iliyopita (2017-Novemba 2023) kumekuwa na utulivu wa bei ya sukari ikiwa ni kati ya Tsh 2,600 hadi Tsh 3,200 kwa kilo na hii ilitokana na Serikali kudhibiti uhaba na uagizaji holela wa sukari.

Baada ya Wazalishaji wa sukari kuona mvua nyingi za El Nino zilizoathiri miundombinu ya mashamba na kushuka uzalishaji waliomba kupitia barua yenye Kumb. Ref. TSPA/SBT/SI&C/03/2023 ya Tarehe 23 Novemba 2023 iliyosainiwa Mwenyekiti wa TSPA kwenda kwa Bodi ya Sukari na nakala kwa Wizara ya Kilimo kuomba kupitia upya kiwango cha Gap Sugar ili kiongezwe kufikia Tani 60,000 katika msimu wa 2023/2024 na kwamba vibali vitolewe mapema kabla ya tarehe 10 Disemba 2023 lakini vibali vilikuja kutolewa kuanzia Tarehe 4 Januari 2024. Katika hali hiyo nani aliyesababisha upungufu wa sukari nchini kama si Waziri wa Kilimo. (Kiambitisho Na. 28)

Pia wazalishaji wa sukari wa ndani waliindikia Bodi yaSukari barua yenye Kumb. Na. Ref. TSPA/SBT/SI&C/04/2023 ya Tarehe 8 Disemba 2023 kukumbusha barua yao ya tarehe 23 Novemba 2023.

(Kiambatisho Na. 29)

3.6 Wizara kufanya marekebisho ya Sheria ya Sukari Na. 6 ya mwaka 2001 kwenye Sheria ya Fedha ya Mwaka 2024 ili kuiwezesha NFRA kununua sukari na kuhifadhi sukari kwenye hifadhi ya chakula ya taifa pamoja na kufanya marekebisho ya Kanuni za NFRA. Hapa kuna mkanganyiko ufuatao:-

Mkanganyiko wa Maelezo ya Waziri wa Kilimo, kwamba NFRA amepewa idhini ya kuagiza tani 410,000 za sukari lakini Bodi ya Sukari imetoa vibali kwa Makampuni binafsi na sio NFRA. Hata barua za uteuzi zilizotolewa na Bodi ya Sukari kwa Makampuni hayo hazionyeshi kama mchakato ulianzia NFRA.

Mawasiliano ya Bodi ya Sukari na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haionyeshi kama Kampuni zinazopewa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi zinapitia NFRA.

Mkanganyiko mwingine Wizara ya Kilimo inafanya marekesho ya kanuni za NFRA na mapendekezo ya kufanya marekebisho ya Sheria ya sukari Na. 6 ya 2001 kupitia Sheria ya Fedha ya 2024 ili kuiwezesha NFRA kununua sukari na kuhifadhi sukari kwenye hifadhi ya chakula ya Taifa. Huku Wizara tayari imeshatoa idhini kwa NFRA kuagiza sukari Tani 410,000 tangu Januari 2024 na bila kusubiri hayo marekebisho ya Sheria Juni 2024. Hapa

Waziri anakiri mwenyewe kutoa vibali kwa wafanyabishara wasio na viwanda vya sukari kinyume cha Sheria.

Mwaka 2022/2023 Gap Sugar iliyotangazwa ilikuwa tani 30,000 ambapo wenye viwanda walipewa vibali vya kuagiza tani 12,500 na wafanyabishara wasio na viwanda vya sukari walipewa vibali vya kiasi kilichobaki kinyume cha sheria na hapakuwa na mvua za El Nino wala utaratibu wa kupitia NFRA. Lakini vibali vilitolewa. Hii inaonyesha kuwa suala la kuagiza sukari nje ya nchi kupitia Makampuni binafsi ni utashi wa Waziri kwa maslahi binafsi kwani mwaka 2022/2023 uzalishaji wa ndani ulikuwa umefikia zaidi 93%.

Marekebisho ya Sheria yanayopendekezwa na Waziri yanakinzana na Sera ya ulinzi wa viwanda vya ndani. Waziri anaruhusu uagizaji holela wa sukari kuua soko na viwanda vya ndani, pia ni kinyume na Makubaliano ya kukuza uzalishaji wa sukari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC) na pia maazimio ya Mkutano wa AGRF (Africa Food Syestem Forum 2023) ya kuzalisha chakula cha kujitosheleza Afrika na kuilisha dunia. Waziri anataka tuue viwanda, tuue mashamba ya miwa ili tuagize sukari kutoka nje ya nchi.

3.7 Wizara ya Kilimo na Bodi ya Sukari wameshindwa kusimamia kikamilifu ubora wa sukari inayoagizwa kutoka nje ya nchi.

Changamoto ya Usimamizi wa ubora wa sukari inayoingizwa kutoka nje ya nchi ni kama ifuatavyo:-

Sukari inaagizwa kutoka nchi tofauti tofauti na baadhi ya nyaraka zinaonyesha kuwa Sukari ilinunuliwa kutoka Dubai na kupakiliwa Maputo Msumbiji, sukari nyingine imenunuliwa nchini Thailand, Brazili na maeneo mengine na kushushwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam na hivyo ufuatiliaji na usimamizi wa ubora una changamoto.

Kutumia njia ya kufungasha upya (repackaging) ili kufanikisha kuingiza sukari isiyo na ubora na iliyokwisha muda wa matumizi, mfano Sukari iliyozalishwa mwezi Februari 2024 nchini Brazili ilifika na kuuzwa nchini Tarehe 23 Februari 2024. Muda wa kusafirisha kawaida huwa ni wiki 14 sawa na miezi 3, sukari hiyo kutoka Brazili imewezaje kufika nchini kwa kutumia mwezi 1? Rejea kifungashio na Tax Invoice iliyotolewa tarehe 23 Februari 2024 na Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Limited

(Kiambatisho 30)

Nimefuatilia kwa waagizaji wa sukari nje ya nchi hasa inayotoka Dubai hawana cheti cha ubora (Health Certificate) lakini wameruhusiwa kuingiza sukari na kuiuza kwa wananchi.

Utofauti wa bei ya sukari kwa kiwango kikubwa huko inakoagizwa kunaleta mashaka makubwa ya ubora wa sukari hiyo. Mfano Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED tarehe 29 Januari 2024 ilinunua sukari nchini Thailand kwa Dola za Marekani 575 kwa tani na siku hiyo hiyo ikanunua sukari Dubai kwa Dola za Marekani 797 kwa tani. Tarehe 7 Februari 2024 ikanunua sukari nchini Brazil kwa Dola za Marekani 820 kwa tani.

3.8 Waziri wa Kilimo kukataa kuonana na wazalishaji wa sukari nchini Katika dhana ya ushirikishwaji katika misingi ya utawala bora haikuwa sahihi kwa Waziri wa Kilimo kuweka masharti ya kukutana na wenye viwanda vya sukari kwani hakujua dharura waliyokuwa nayo wawekezaji hao na kikao chao kisingeondoa maelekezo yake ya awali, lakini pia ilikuwa fursa kwa Serikali kupokea ushauri na maoni kutoka kwa wazalishaji wa sukari nchini.

Mbaya zaidi Waziri anaingilia hadi masuala ya uendeshaji wa ndani ya viwanda vya sukari na kufikia hatua ya kuwakataa baadhi ya wasambazaji walioingia mikataba na viwanda akishinikiza wafutiwe mikataba jambo ambalo liko nje ya majukumu ya Waziri wa Kilimo ya kusimamia sera na sheria. Lakini pia Waziri wa Kilimo amekuwa akiwatupia lawama wenye viwanda na kuwasingizia mambo mengi ya uongo badala ya kufanya kikao nao hali inayovunja moyo wawekezaji wa ndani na kuhujumu jitihada za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kufungua nchi na kuvutia uwekezaji nchini.

MADHARA YA MAAMUZI YA WAZIRI WA

KILIMO

Madhara yatakayopatikana kufuatia maamuzi Waziri Bashe ni Viwanda vyote 7 vya sukari vilivyopo nchini vitazorota uzalishaji na vitafungwa na hivyo taifa letu kutegemea sukari ya kutoka nje ya nchi zaidi ya Tani 490,000 kwa mwaka ambayo itahitaji fedha za kigeni zaidi ya Dola za Marekani Milioni 490 sawa Tsh Trilioni 1.3 kwa kila mwaka kuagiza sukari nje ya nchi. Pia maamuzi hayo yataleta changamoto zifuatazo:-

Kukosekana kwa ushindani ulio sawa kutokana na misamaha ya kodi, Usimamizi dhaifu wa bei itasababisha viwanda vya ndani kusuasua na kutakuwa na mlundikano mkubwa wa sukari nchini iliyoanza kuzalishwa na viwanda vya ndani na hivyo kukosa soko na kutouzika kirahisi kutokana na ushindani mkubwa wa sukari ya kutoka nje ya nchi iliyoingizwa.

Kuua ajira za moja kwa moja zaidi ya 25,000 na ajira zingine nyingi za watoa huduma, wasafirishaji na Wakulima wanaozunguka viwanda zaidi ya 12,000 na wanafunzi wa vyuo kukosa maeneo ya kufanya mafunzo kwa vitendo. Pia kuathiri huduma zingine za kijamii ikiwemo afya, elimu na michezo ya timu za Mpira za Miguu.

Wakulima wa miwa (Cane growers) kupoteza soko la mazao yao. Itavuruga mfumo wa maisha ya Wakulima wa miwa kwa kuwakosesha mapato ya uhakika yanayozidi Tsh. Bilioni 100 kila mwaka na hivyo kutumbukia kwenye lindi kubwa la umasikini.

Wananchi wetu na Wakulima wetu wa wilaya na maeneo ya Mvomero (Turiani), Ifakara, Kilombero, Kilosa, Misenyi ambao kwa sehemu kubwa wanategemea kipato chao kupitia kilimo cha miwa ambapo wameingia gharama kubwa kuendeleza mashamba na wana mikopo badala ya kuwaunga mkono tunaua nguvu kubwa waliowekeza.

Serikali kukosa mapato yatokanayo na kodi na ushuru mbalimbali wa viwanda na mnyororo mzima wa uzalishaji na usambazaji wa sukari unalokadiriwa kufikia zaidi ya Tsh. Bilioni 700 kwa mwaka.

Uwekezaji wa zaidi ya Tsh Trilioni 1.8 uliowekezwa katika viwanda katika kipindi cha miaka 5 iliyopita kupotea na nchi kupata kubwa.

Nchi kugeuzwa kuwa jalala la sukari feki na iliyokwisha muda wa matumizi na kuleta madhara makubwa ya kiafya kwa wananchi.

Kushindwa kurejesha mikopo na ugumu wa kupata mikopo katika taasisi za fedha za ndani na nje ya nchi

Kuzorota kwa uzalishaji wa sukari au kufungwa kwa viwanda kutapelekea Makampuni, Wakulima wa miwa na watoa huduma wengine na wafanyakazi kushindwa kurejesha mikopo kwenye mabenki yaliyowakopesha na hivyo kusababisha mabenki hayo kupata changamoto za ukwasi na hivyo kuathiri uchumi wa nchi.

Viwanda na Wakulima kutokuamiwa katika taasisi za fedha kwa kukosa kinga kutokana na kuruhusu uingizaji holela wa sukari kutoka nje ya nchi. Na hivyo kukwamisha jitihada za nchi za kuifanya nchi yetu kujitosheleza mahitaji ya sukari ifikapo mwaka 2025.

UZOEFU WA NCHI NYINGINE KUHUSU BIASHARA YA SUKARI

Nchi ya Kenya iliporuhusu uingizaji holela wa sukari mwaka 2017 takribani tani 989,619 ilipelekea viwanda 6 kufungwa kikiwemo kiwanda cha Serikali cha Mumias Sugar. Na uzalishaji wa Sukari Kenya kushuka kutoka Tani 639,741 mwaka 2016 hadi tani 376,111 mwaka 2017 anguko la 41% rejea ripoti Mamlaka ya Kilimo na Chakula (AFA) Kenya ya 2011-2022 (Kiambatisho 31)

Nchi zote zinazolima miwa na kuzalisha sukari Duniani kama Thailand, India na Brazili zimeweka utaratibu wa kutoruhusu hata sukari ya kwao ikitoka kwenda nchi nyingine haiwezi tena kurudi nchini mwao kutokana na viwango vikubwa vya ushuru na kodi vinavyozidi 35% mpaka 65% ili visishindane na sukari iliyopo na inayozalishwa ndani ya nchi zao.

Tunaagiza sukari kutoka Brazil, Thailand, India nk nchi hizo zilifanya jitihada kubwa za kuongeza uzalishaji wa sukari kutosheleza mahitaji na kuuza nje ya nchi, kutoa ruzuku kwa wenye viwanda na Wakulima wa miwa, kuweka kodi kubwa kwa sukari kutoka nje ya nchi na kuzuia uingizaji holela wa sukari katika nchi zao.

Leo sisi Tanzania, Waziri tuliyempa dhamana ya Kilimo anaona fahari kuagiza sukari nje ya nchi na kuhujumu mipango na mikakati ya kitaifa iliyowekwa ya kuongeza uzalishaji wa sukari na nchi kujitosheleza mahitaji.

MAMBO YASIYO YA KAWAIDA KATIKA BIASHARA YA SUKARI

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Taarifa za CAG za miaka ya nyuma kabla ya mwaka 2017 zililalamikia uagizaji holela wa sukari kutoka nje ya nchi zaidi ya mahitaji au nakisi ya sukari (Gap Sugar). Pia katika ukaguzi wa mwaka 2022/2023 ukaguzi umethibitisha kuwa moja ya sababu ya kuwa na uhaba wa sukari ni Usimamizi na udhibiti hafifu wa Bodi ya Sukari, kuchelewa kutolewa vibali na kutokuagiza Gap Sugar kwa wakati. Pia ripoti hiyo inaonyesha kuwa Gap Sugar ilikuwa tani 29,951 tu kwa sukari ya majumbani mwaka 2022/2023.

Maagizo ya Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli

Rais wa awamu ya Tano, Hayati Dk. John Pombe Magufuli alipiga marufuku uingizaji holela wa sukari kutoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani na kukuza ajira kwa vijana wa kitanzania. Nanukuu.

“Unakuta Serikali ni moja lakini ndani ya coordination yuko mwingine aidha kwa makusudi yake kwa sababu amepewa virushwa kidogo yeye nikutoa vibali tu vya kuingiza sukari na inawezekana hata hiyo sukari inaingia nchini ambayo ni sukari ambayo ni very inferior, nyingine labda kwenye nchi nyingine ilikuwa Iexpire katika mwezi mmoja au wiki mbili inaletwa huku alafu wana I re berg, hii ni mifano kwa hiyo huku tunazungumza tuwe na viwanda vingi, mmoja tu labda hata mkurugenzi ndiye anaye mamlaka ya kutoa vibali hivyo anatuambia tusitengeneze sukari, tumeshajipanga serikalini na bahati nzuri mheshimiwa Waziri Mkuu uko hapa, hakuna vibali vya namna hiyo kutoka bila idhini yako, tunataka sukari ya hapa izalishwe sana ili watu tuwape motisha ya kufungua viwanda vingi ili vijana wengi wapate ajira, na Wakulima wauze mazao yao” Magufuli tarehe 18 Februari 2016. (Kiambatisho Video Clip)

Maelezo ya aliyekuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Faustine Mkenda (Mb)

Msimamo wa Wizara ya Kilimo uliotolewa Agosti 30 2021 na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Profesa Adolf Faustine Mkenda (Mb) wakati Waziri wa sasa Mheshimiwa Bashe akiwa Naibu

Waziri wa Wizara ya Kilimo, Profesa Mkenda alisema nanukuu.

“Suala la kuingiza sukari nchini ni suala la rushwa, la ufisadi mkubwa kwa sababu tamaa yake kubwa mno, tamaa ya kunufaisha wachache kunyima watanzania ajira kubwa mno, tamaa ya kunufaisha wafanyabiashara wachache, kunyima Wakulima fursa ya kuuza miwa kubwa mno, sukari ni kama madawa ya kulevya. Pesa nyingi sana nalisema hili kwa sababu hizi takwimu zinatupa picha I have to say this, Vinginevyo nyongo itaniua. Tamaa ya kuwapa watu wachache fursa ya kuleta sukari kuua ajira ya watanzania, kunyima wakulima fursa ya kuuza miwa na kuinyima Serikali kodi kubwa mno, huko nyuma wako mawaziri waliondoka sitowataja hilo hilo kwa kutoa vibali vya kuingiza sukari hapa wakati hali ndio hivyo, lakini serikali imejipanga sasa kwa wale wanaoleta shinikizo kuingiza sukari, wafanyabiashara wanasumbua sana Bodi ya Sukari, wanasumbua sana, wanasumbua kweli kweli, wewe ni mfanyabiashara huzalishi sukari, Sheria inasema ni mzalishaji wa sukari peke yake ataruhusiwa kuingiza sukari hapa nchini na ataingiza sukari hiyo kulingana na pengo lililopo.

Halafu unazunguka na kuanza kutoa tuhuma kwenda kumshitaki Mtendaji Mkuu ooh sisi tunanyimwa fursa, waache ndiyo maana napenda niseme hadharani hili hicho kibali cha sukari kitapitia mezani kwangu mimi Adolf Mkenda, Waziri wa Kilimo na hakitapita bora niachie ngazi, hakitapita bora niachie ngazi. Tunamnufaisha nani wanaopeleka majungu wapeleke na wafanyabishara acheni kutuzunguka kutuharibia, huyu mwekezaji akiacha expansion atatusaidia nini sisi, inafurahisha nini kuendelea kuagiza sukari kutoka nje, inawasaidia nini, haitusaidii chochote tunaweza tukajitegemea tukiacha tamaa. Kwa hiyo la sukari ni hilo nilitaka niliseme kibali kitapita kwa Waziri wa Kilimo sikitoi ng’o, hakina maslahi kwa nchi yetu na tutaichafua sana Serikali kama tukitoa kitachafua sana, kitachafua sana Serikali inaenda vizuri mpaka hapa hatutoi kibali ng’oo” Mwisho wa Kunukuu, Prof Mkenda Agosti 30 2021 (Kiambatisho Video Clip)

Kama huu ndiyo ulikuwa msimamo wa Serikali, msimamo wa Wizara ya Kilimo, Msimamo wa Bodi ya Sukari kuwa uagizaji wa sukari nje ya nchi umejaa kila aina ya madili, rushwa na ufisadi na leo hii mimi Mpina nikisema kampeni kubwa ya uagizaji sukari nje ya nchi anayoifanya Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Bashe inasukumwa na rushwa na ufisadi kosa langu ni nini.

Maelezo ya Waziri wa Kilimo wa sasa Mhe. Hussein Mohamed Bashe (Mb)

Wenye viwanda wana option mbili wafuate utaratibu wa Serikali hawawezi waache. Hii kazi na tumewapelekea waraka wa kubadilisha mfumo wa usambazaji haiwezekani mfano Kagera Sugar ana Distributor mmoja yuko Mwanza anahudumia mikoa 11.

Serikali haiwezi kuruhusu, tumewaprotect vya kutosha kama nchi lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mwezi wa 6 kwenye Bunge la Bajeti kama Waziri mwenye dhamana ninapeleka mabadiliko ya Sheria kwa ajili ya liberalize biashara ya sukari.

Wata compete na competing company za kutoka nje na wenyewe watapata incentive zilizomo ndani ili kuwa protect lakini hatuwezi kuendelea kuwaprotect hawa watu tumewaprotect over 20 years is enough kama kukua wameshakuwa na kuanzia baada ya mabadiliko ya sheria hiyo Sugar Gap haitoagizwa na wao kwa sababu tutakuwa tumebadilisha sheria watapata incentive kama strategic investors, Teri anafanya kazi nzuri na Kitila watawapa package wanavivutio vingi vya kodi wataruhusiwa ku compete na watu wengine sokoni kwa sababu hatuwezi kuendelea na

Irresponsible Private Sectors kwenye nchi.

Kwa hali hii inayoendelea ili wajue ni position, Wakulima wa miwa wako 12,500 nchi hii tutasota mwaka huu mmoja, mabonde yale tutayageuza ya mpunga, there is no problem ziko nchi ambazo zimeacha kulima sukari.” Mwisho wa kunukuu, Mhe. Bashe 22 Februari 2024, Ikulu Dar es Salaam. (Kiambatisho Video Clips)

Haitegemewi kauli chafu kama hizi kutolewa na Waziri aliyepewa dhamana ya Kilimo nchini badala ya kuhamasisha ukuaji wa kilimo yeye anafanya kampeni kubwa ya kuua kilimo nchini kwa maslahi binafsi na tena kauli hizo chafu amezitoa akiwa Ikulu.

Kauli za Waziri Bashe akiwa Ikulu zinachangamoto zifuatazo:-

Waziri hana mamlaka ya kukashifu sekta binafsi na badala yake anapaswa kusimamia sera na sheria lakini pia huwezi kuwaita wazalishaji wa sukari kuwa ni Irresponsible Private Sector, viwanda ambavyo vinahakikisha sukari inapatikana nchini, kutoa ajira na kulipa kodi, vimeongeza uzalishaji na kuifanya nchi kujitosheleza kwa sukari 94% na Gap Sugar kubakia 6% tu ambapo tusingekuwa na mvua za El Nino mwaka 2023/2024 kusingekuwa na Gap Sugar nchini.

Waziri Bashe kuona kazi ya kulinda viwanda vya sukari vya ndani kama hisani wakati ndiyo jukumu la msingi la Serikali na kudanganya kuwa viwanda hivyo vimelindwa kwa zaidi ya miaka 20 huku akijua marekebisho ya kulinda viwanda vya sukari tuliyafanywa mwaka 2020 kipindi ambacho yeye alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo.

Waziri ameonyesha dhamira ya wazi ya kuua viwanda vya sukari na mashamba ya miwa kuyageuza kuwa ya mpunga ili nchi itegemee sukari ya kutoka nje ya nchi, kupoteza mapato, ajira, fedha za kigeni

Kauli za dharau na kejeli kwa sekta binafsi na wakulima wa miwa zinakwenda kinyume na dhana ya utawala bora, kupunguza ari ya kuwekeza na kufukuza wawekezaji nchini.

HITIMISHO

Katika mapitio ya mahojiano na vielelezo nilivyopokea pamoja na Ripoti ya CAG nimejiridhisha kwamba:-

Wizara ya Kilimo na Bodi ya Sukari wametoa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi zaidi ya mahitaji (Gap Sugar) jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Wizara ya Kilimo na Bodi ya Sukari waliandaa mkakati kutengeneza uhaba wa sukari nchini na ndiyo maana vibali vya kuagiza sukari ya nakisi havikutolewa mapema hata baada ya tahadhari ya mvua kubwa za El Nino ili kufanikisha lengo la kuwapa vibali wafanyabiashara wasio na viwanda kuagiza sukari nje ya nchi kinyume cha Sheria.

Hapakuwa na sababu za msingi za kusamahe kodi ya Import Duty na VAT bali ilikuwa ni kuwaongezea faida kubwa wafanyabishara wanaoingiza sukari kutoka nje ya nchi na kujinufaisha binafsi.

Kuna kampeni kubwa inayoendeshwa na Waziri wa Kilimo ya kuua kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari nchini, kusema uongo na hata kupendekeza marekebisho ya Sheria ya Sukari ili kufanikisha biashara ya uagizaji holela wa sukari nje ya nchi.

Nashauri yafuatayo:-

Mchakato wa kubadilisha Sheria ya Sukari katika Bunge hili la Bajeti la mwaka 2024 kama alivyosema Waziri wa Kilimo usitishwe kwani hauna maslahi kwa taifa na umelenga kuua kilimo cha miwa na viwanda vya sukari nchini.

Serikali ifute vibali vyote vya kuingiza sukari vilivyotolewa na kuzuia sukari kuingia nchini, kufanya ukaguzi na kuiondoa sukari isiyo na ubora kwenye matumizi ya binadamu.

Bunge liunde tume maalum kuchunguza kashfa ya uagizaji holela wa sukari na misamaha holela ya kodi iliyotolewa na kupendekeza hatua za kuchukua, Pia Kanuni ya 70 ya Kanuni za Kudumu za Bunge ichukue nafasi yake katika kumwajibisha Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe kwa kusema uongo Bungeni.

Vyombo vya uchunguzi vichukue hatua za kisheria kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe na mtandao mzima uliohusika kwenye kashfa ya sukari ikiwemo kushtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi wa nchi.

Ninaamini kuwa kusema uongo mara 18 bungeni haikuwa kwa bahati mbaya bali Waziri huyo kwa makusudi alilenga kulipotosha Bunge ili lifanye maamuzi ya kufanikisha malengo yake binafsi kupitia chombo hicho kikubwa cha uwakilishi wa wananchi. Waziri wa Kilimo ameliyumbisha Bunge kwa kiwango kikubwa hivyo kunilazimu kutoa maelezo yenye kurasa 41 na viambatisho 40 vya vyaraka na Flash Disk 1 (Video Clips).

Kipekee namshukuru sana Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Tulia Ackon (Mb) kwa agizo lake la kunitaka mimi Luhaga Joelson Mpina, Mbunge wa Jimbo la Kisesa kutoa maelezo na ushahidi wa vielelezo bungeni ili kuthibitisha uongo uliosemwa Bungeni na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe Mnamo tarehe 4 Juni 2024. Lakini pia kuweka wazi ukweli uliofichwa na Waziri huyo kwa
1718698248748.png
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia ni mtu anayeishi mbele ya wakati na muda na kiongozi Mwenye akili na upeo wa hali ya juu sana,ni mtu Mwenye jicho la tatu nje na haya mawili ya kibinadamu.ni kiongozi aliyejaliwa macho ya Rohoni yenye uwezo wa kuona asipoweza kuona Mwenye macho ya kawaida.

Ni kiongozi mwenye ufunuo wa kiroho wa kutambua masuala mbalimbali.ndio maana huwezi ukaona akikurupuka wala kuhemuka wala kuzungumza jambo hadharani bila staha. Ni mtu mtulivu,makini na mwenye kuchunga ulimi wake kabla na wakati wa kuzungumza.huwezi ukaona akijikwaa hovyo ulimi wake na kuleta taharuki au mgawanyiko ndani ya Taifa.

Alipokuwa anaingia na kutwaa madaraka ya urais kuna watu hawakuamini mioyoni mwao kama anaweza kuongoza Taifa letu kwa hata mwezi mmoja tu.walitamani kama wangekuwa na mamlaka au uwezo basi wangemuweka pembeni na kumuacha na Umakamu wake na wao kuweka mtu wao.waliona ni kama hastahili wala hafai wala hana huo uwezo wala hakuandaliwa kwa nafasi hiyo.

Lakini Mungu katika ulimwengu wake wa kiroho tayari alikuwa amemuandikia kwa wino usiofutika kuwa Mama Samia atainuliwa na kuwa Rais wa Taifa letu.Ndio maana pamoja na watu kuleta habari za ubaguzi kwa misingi ya jinsia na ukanda. Kumzushia mambo ya uongo, uchonganishi,fitina na chuki binafsi.bado Rais wetu ameendelea kuaminika ,kuungwa mkono ,kupendwa na kukubalika sana machoni pa watanzania ,huku Taifa likiendelea kutamalaki kwa amani na utulivu mkubwa sana.

Jambo ambalo linawaumiza sana waliokuwa hawana Imani na Rais wetu na waliokuwa wakitamani kutokuona akiwa Rais wetu.Lakini kubwa na linalowapa homa ni kuona namna watanzania wanavyohitaji kwa kiu kubwa sana kuona Mama huyu mzalendo na kipenzi cha watanzania akiendelea na muhula wa pili kama Rais.

Sasa ili kumkwamisha ,kumkatisha tamaa,kumchonganisha na wananchi,kumvunja moyo,kumchafua na kumpunguza kasi .sasa wabaya na wapinzani wa Mama yetu wameona watumie silaha yao ya mwisho ambayo nayo imeonekana kutokuwa na nguvu kabisa, ya kuzusha mambo ya uongo, uchonganishi na maneno ya fitina na chuki binafsi.na ndio mwisho wao mbaya sana utakaowapoteza kabisa katika ramani ,kwa sababu watanzania wameshatambua njia hiyo ya kumchafua Rais wetu mpendwa. Hakuna silaha ya aina yoyote ile itakayoinuka na kufanikiwa mbele ya Rais wetu mpendwa.kila kitu kitashindwa na mwisho Rais wetu itaendelea kuwa shujaa wetu na jasiri Muongoza Njia.

Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Watu wa DCEA tafadhali lile Zoezi lenu la Kupambana na Matahaira kama mmelipumzisha hebu lirejeeni kuna Wengine.
 
Unafahamu mmiliki wa gazeti hili? Unafahamu historia yake na uadilifu wake?
Kwann watu wajinga, Huwa wanakawaida ya Kumshambulia mtu na sio uhalisia?.

Usiwe kipofu sababu ya uchawa mpaka ushindwe kuona uhalisia.

Nyeupe ni nyeupe, nyeusi ni nyeusi haijalishi Nani kasema.

Je History ya Mmiliki wa gazeti, inaondoa ukweli wa Madudu ya Bashe ??.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia ni mtu anayeishi mbele ya wakati na muda na kiongozi Mwenye akili na upeo wa hali ya juu sana,ni mtu Mwenye jicho la tatu nje na haya mawili ya kibinadamu.ni kiongozi aliyejaliwa macho ya Rohoni yenye uwezo wa kuona asipoweza kuona Mwenye macho ya kawaida.

Ni kiongozi mwenye ufunuo wa kiroho wa kutambua masuala mbalimbali.ndio maana huwezi ukaona akikurupuka wala kuhemuka wala kuzungumza jambo hadharani bila staha. Ni mtu mtulivu,makini na mwenye kuchunga ulimi wake kabla na wakati wa kuzungumza.huwezi ukaona akijikwaa hovyo ulimi wake na kuleta taharuki au mgawanyiko ndani ya Taifa.

Alipokuwa anaingia na kutwaa madaraka ya urais kuna watu hawakuamini mioyoni mwao kama anaweza kuongoza Taifa letu kwa hata mwezi mmoja tu.walitamani kama wangekuwa na mamlaka au uwezo basi wangemuweka pembeni na kumuacha na Umakamu wake na wao kuweka mtu wao.waliona ni kama hastahili wala hafai wala hana huo uwezo wala hakuandaliwa kwa nafasi hiyo.

Lakini Mungu katika ulimwengu wake wa kiroho tayari alikuwa amemuandikia kwa wino usiofutika kuwa Mama Samia atainuliwa na kuwa Rais wa Taifa letu.Ndio maana pamoja na watu kuleta habari za ubaguzi kwa misingi ya jinsia na ukanda. Kumzushia mambo ya uongo, uchonganishi,fitina na chuki binafsi.bado Rais wetu ameendelea kuaminika ,kuungwa mkono ,kupendwa na kukubalika sana machoni pa watanzania ,huku Taifa likiendelea kutamalaki kwa amani na utulivu mkubwa sana.

Jambo ambalo linawaumiza sana waliokuwa hawana Imani na Rais wetu na waliokuwa wakitamani kutokuona akiwa Rais wetu.Lakini kubwa na linalowapa homa ni kuona namna watanzania wanavyohitaji kwa kiu kubwa sana kuona Mama huyu mzalendo na kipenzi cha watanzania akiendelea na muhula wa pili kama Rais.

Sasa ili kumkwamisha ,kumkatisha tamaa,kumchonganisha na wananchi,kumvunja moyo,kumchafua na kumpunguza kasi .sasa wabaya na wapinzani wa Mama yetu wameona watumie silaha yao ya mwisho ambayo nayo imeonekana kutokuwa na nguvu kabisa, ya kuzusha mambo ya uongo, uchonganishi na maneno ya fitina na chuki binafsi.na ndio mwisho wao mbaya sana utakaowapoteza kabisa katika ramani ,kwa sababu watanzania wameshatambua njia hiyo ya kumchafua Rais wetu mpendwa. Hakuna silaha ya aina yoyote ile itakayoinuka na kufanikiwa mbele ya Rais wetu mpendwa.kila kitu kitashindwa na mwisho Rais wetu itaendelea kuwa shujaa wetu na jasiri Muongoza Njia.

Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Wewe ungejikita kwenye ile biashara yenu ya ukoo ya kuchuna watu ngozi tu, huku unajidhalilisha tu.
 
Sasa wabaya na wapinzani wa Mama yetu wameona watumie silaha yao ya mwisho ambayo nayo imeonekana kutokuwa na nguvu kabisa, ya kuzusha mambo ya uongo, uchonganishi na maneno ya fitina na chuki binafsi.na ndio mwisho wao mbaya sana utakaowapoteza kabisa katika ramani ,kwa sababu watanzania wameshatambua njia hiyo ya kumchafua Rais wetu mpendwa. Hakuna silaha ya aina yoyote ile itakayoinuka na kufanikiwa mbele ya Rais wetu mpendwa.kila kitu kitashindwa na mwisho Rais wetu itaendelea kuwa shujaa wetu na jasiri Muongoza Njia.
Watu wangekuona una akili na busara kama ungetaja baadhi ya mambo ambayo wewe unaona wanamzushia na kumsingizia, na kuyakanusha kwa hoja. Kwa mfano, tuhuma kwamba Abdul, mtoto wa Samia, nae alipewa vibali vya sukari, zikanushe kwa hoja ukijua watu wanaweza kukuletea ushahidi.

Bila hivyo watakuona wewe ni vuvuzela tu lenye kelele nyingi bila kuwa na ubongo wala kujua kinachoendelea.
 
Wewe si ndio walewale waongo na wazushi? Unaweza vipi zusha habari ya uongo pasipo ushahidi halafu useme mtu akanushe kwa vithibitisho? Huoni huo unakuwa ni uwendawazimu na ukichaa?
 
Wewe chawa umeona hiyo silaha moja , kwenye ghala la silaha la Chadema kuna silaha nyingi nzito nzito na kali zitatumiwa 2025 . Kuna silaha maalumu kali kuliko zote itatumika dakika ya 89 kwenye uchaguzi wa rais 2025 na upinzani wataibuka na ushindi kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.
 
Wewe chawa umeona hiyo silaha moja , kwenye ghala la silaha la Chadema kuna silaha nyingi nzito nzito na kali zitatumiwa 2025 . Kuna silaha moja kali kuliko zote itatumika dakika ya 90 kwenye uchaguzi wa rais 2025 na upinzani wataibuka na ushindi kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.
CHADEMA haina uwezo wala ubavu wala nguvu ya kuweza kushindana na CCM katika sanduku la kura.iwa sasa inaendelea kusambaratika na kupasuka vipande vipande kama kioo
 
Wewe chawa umeona hiyo silaha moja , kwenye ghala la silaha la Chadema kuna silaha nyingi nzito nzito na kali zitatumiwa 2025 . Kuna silaha moja kali kuliko zote itatumika dakika ya 90 kwenye uchaguzi wa rais 2025 na upinzani wataibuka na ushindi kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.
CHADEMA haina uwezo wala ubavu wala nguvu ya kuweza kushindana na CCM katika sanduku la kura.kwa sasa inaendelea kusambaratika na kupasuka vipande vipande kama kioo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom