Mkuu Rufiji,
Mimi binafsi nimeshitushwa na hiii theory, ambayo niliambiwa na kiongozi mmoja mzito sana kwamba katika siasa za Kenya, the bottom line ni M-Kikuyu, hawezi kubali kutawaliwa na Mjaluo,
Meaning kwamba hii kupiga kura na the rst of the story ilikuwa geresha tu, wao huko Kenya wanajua ukweli toka enzi za baba yake Odinga, sasa kama huuu ndio ukweli wenyewe sisi bongo tunafanya nao nini hawa wakabila?
FMES,
Tukiwashambulia Wakenya kwa ukabila wao, lazima tujiulize na sisi je tuko salama?
Ukweli ni kwamba hayo wanayofanya Kenya, sisi tulishayaanza toka mwaka 1995 kule Zanzibar.
Tunasema Mpemba hata siku moja hawezi kuongoza Zanzibar.
Tatizo hapo sio ukabila tu, tatizo ni wanasiasa kutumia ukabila ili wabaki kwenye power.
Japo inaonekana TZ bara hatuna ukabila mkubwa lakini nakumbuka mwaka 1995 maeneo mbalimbali ya nchi, CCM walikuwa wanasema mkichagua Mchaga Mrema mtaibiwa maana wote ni wezi. Sasa kama huo si ukabila ni nini?
CCM kama watakaribiwa sana na Mbowe mwaka 2010, tegemea kusikia mambo ya ukabila na Uchaga.