The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 2,264
- 4,142
Imepita takribani zaidi ya miaka 60 tangu uhuru, lakini maisha ya Mwafrika hayana tofauti na ya mbwa Koko, ambaye hajui ale nini au avae nini.
Ukitumia akili ya ndani, utagundua kuwa kabla ya uhuru, Waafrika walikuwa na maisha bora, ikiwemo uhakika wa lishe, ajira tele mashambani na viwandani, biashara tele, na elimu bora. Ni tamaa tu ya wapigania uhuru kuwahadaa Waafrika wengi ili wawape sapoti ya kuwafurusha wakoloni, wakiwa na lengo lililo nyuma ya pazia wao – na vizazi vyao pekee – ili waje kurithi mema ya nchi baada ya wakoloni kuondoka. Leo ni ushahidi usio na shaka kabisa kuwa vizazi vya wapigania uhuru bandia ndivyo vimeshika madaraka, au vipo kwenye mfumo wa wizi wa raslimali za umma, huku mamilioni ya Waafrika wakitopea kwenye lindi la umasikini. Huu ni uthibitisho kuwa Waafrika walidanganywa.
Na hata baada ya uhuru, wapigania uhuru waligeuka kuwa wakoloni weusi, huku wakiwatendea mabaya sana Waafrika, ikiwemo ukatili, mauji, matumizi mabaya ya raslimali za wananchi, na kuua chumi za nchi zao, tofauti na alivyofanya mkoloni mweupe. Waligeuka kuwa madikteta, mafedhuli, na wang’ang’anizi madarakani, ingawa wao wenyewe hawakutaka wakoloni wang’ang’anie madarakani.
Baada ya kushindwa kuwaletea maendeleo, Waafrika walipanda sumu na chuki mashuleni, kwa kuwaaminisha wananchi kuwa mabaya wanayopatayo ni matokeo ya ukoloni, kitu ambacho ni uongo mkubwa. Hakuna uhusiano wa kutoendelea na kutawaliwa; hata mataifa yote makubwa yamewahi kutawaliwa, lakini baada ya uhuru au mapinduzi wamepiga hatua.
USA ilitawaliwa na Muingereza, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa zilitawaliwa na Rumi (Italy), China ilitawaliwa na Japan, na India na Muingereza. Kama kutawaliwa ni kikwazo cha maendeleo, mbona Ethiopia na Liberia hazikuwahi kutawaliwa?
Shida ya Afrika sio chaguzi, katiba bora, au tume bora za chaguzi; Kenya, Ghana, Malawi, Zambia, nk wanazo kitambo, lakini nini kimebadilika kutuzidi sisi? Wanasiasa wote, iwe ni upinzani au tawala, wote ni njaa tu ndo zinawasukuma kutafuta shibe sawa na tumbili. Wanapopigia kelele ngedere wakiwa nje ya shamba, lakini wakiwa ndani ya shamba, wao ni wale wale, hawana jipya.
Mambo ya chaguzi ni matumizi mabaya ya kodi na raslimali za nchi, kwa maana hazibadili chochote. Afrika inahitaji mfumo mpya wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo na sio hizi mambo ya chaguzi na vyama vingi. Vyama vingi vimeshapitwa na wakati; miaka sasa havina tija yeyote zaidi ya kufaidisha wajanja wachache.
Nini kifanye?
Hitimisho: Wapigania uhuru walipigania maslahi yao binafsi kwa kuwahadaa Waafrika, na si maslahi ya Waafrika wote.
Nachokoza mada.

- Kazi ya urais iwe ni kazi ya kuajiriwa watu. Maombi ya urais yafanyike, na kama haujafanya vizuri, mkataba usitishwe.
- Bunge lisiwe la vyama, bali liwe na makundi ya wakilishi yote, ambapo kila kundi litaingia bungeni kwa nafasi maalumu kama wawakilishi: vijana, watoto, walemavu, kina mama, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wafugaji, wavuvi, wasanii, machinga, wanachuo, wanamichezo, na makundi mengine ya wakilishi.
- Waziri asiwe mbunge, na uwaziri uwe ni kazi ya kuajiriwa, na sio kuteuliwa.