Mangi wa Rombo
Senior Member
- Sep 25, 2014
- 172
- 104
Habari!
Kwa huzuni kubwa leo naomba kwa mara nyingine niwakilishe kadhia wanayopitia wakazi wa Mbopo kata ya Mabepwande kufuatia ubovu wa miundombinu kwenye kata hii iliyo kwenye jimbo la kawe!
Tangu mvua ya December 2023 mpaka January 2024 iliyoharibu kabisa barabara na miundombinu katika kata hii, nasikitika kusema 90% ya athari hizi hazijarekebishwa!
Leo nimeshuhudia namna watoto/wanafunzi wanavovushwa kwenye moja ya bonde ambalo kiunga/daraja lake lilisombwa na maji mwezi Januari! Aisee ni huruma na hatari! Watoto hawa wanabebwa migongoni na kuvushwa na vijana wanaojitolea!
Hili eneo ni moja ya eneo korofi, ubovu wake unafahamika na ofisi ya mbunge wa kawe, meneja TARURA mkoa, na hata ofisi ya wizara ya ujenzi lakini cha ajabu hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa!
Wananchi wa eneo hili wanadai walishawai kuchanga pesa ili kujenga karavati lakini wanadai mbunge alikuja akawambia serikali itajenga hivyo wakarudishiwa pesa zao, cha ajabu hakuna ujenzi wowote uliofanyika!
Swali langu, je serikali inasubiri mpaka watoto wasombwe na maji waje kuaga miili na makamera kama kawaida yao au? Hii ni aibu, mkoa wa Dar es salaam uko hivi, mkoani je?