Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,624
- 47,267
Umbea ni umbea tu, uwe na tija au usiwe na tija. Wote tu wambea, hata huu pia ni umbea.
Umbea ni umbea tu, uwe na tija au usiwe na tija. Wote tu wambea, hata huu pia ni umbea.
Tumekuelewa ila mazoea na waume zetu hatutakiHabari za jumapili wapendwa!
Kuna tukio lilinitokea na through that nikapata funzo kubwa tu.
Nina rafiki yangu(class mate) tulikuwa marafiki tangu shule, ila baada ya kuhitimu tukapotezana na hatukuwa na mawasiliano. Tukaja kuonana tena baada ya kama miaka 9 akiwa katika mchakato wa kuoa, urafiki ukarudi na tukawa na mawasilianao ya karibu tu. Baada ya kufunga ndoa nilianza kuweka kadistance maana mazoea sana na waume za watu sio mazuri.
Kuna kipindi alikuwa na wazo fulani kuhusu biashara na alinishirikisha tukashauriana vizuri na biashara ikafunguliwa na ikawa ikienda vyema.
Alipenda kunipa updates za hiyo biashara, na baadae akamuachia mkewe(wifi) aiendeshe then akawa na wazo lingine la project nyingine kubwa zaidi ambayo ingekwenda vizuri alikuwa na plan ya kuacha kazi ya kuajiriwa na kuiendesha mwenyewe.
Kutokana na kunishirikisha kwa karibu sana mambo yake, nikagundua mazoea yanakolea zaidi, nikaanza kumpotezea nikitambua yeye mtu mzima ataelewa tu. Alianza kulalamika sana maana mara nyingi nilikuwa sipokei call zake wala kujibu text zake, ikabidi nimwambie tu ukweli kuwa nisingependa hayo mawasiliano ya karibu namna hiyo. Japo kwa uchungu alinielewa ila aliomba sana nisipoteze mawasiliano nae kabisa.
Baada ya kama mwezi hivi nilipokea simu kutoka kwa mkewe akilalamika sana na kunilaumu akihisi nina mahusiano na mumewe, ilibidi nimtulize munkari then tulonge taratibu kiutu uzima.
Alilalamika kuwa kuna mambo mengi ambayo emekuta ktk mawasiliano baina yangu na mumewe ambayo yeye binafsi hayajui na hajawahi kushirikishwa. Hapo sasa ndio ikabidi niongee nae na kumuuliza vizuri kuhusu mawasiliano baina yake na mumewe, nikagundua sio supportive kwa mumewe na huwa hayaamini mawazo ya mumewe.
Sasa nilichojifunza ni kwamba mwanaume anapenda sana kusikilizwa,kuheshimiwa na kuaminiwa. Anaweza akaja na wazo lake ambalo ukiliangalia harakaharaka unaona kabisa hapa hakuna kitu, sasa sisi wanawake huwa tuna tabia ya kuwakatisha tamaa, unaweza kuguna mguno classic au kucheka kabisa kwa dharau kumuonyesha kuwa wazo lake ni la hovyo kabisa, ilihali hata wazo mbadala pia hauna.
Mpe nafasi ya kumsikiliza, then kama atakuomba ushauri mpe kama hauna bora umshauri atafute ushauri pahali sahihi, mtie moyo na umuamini kuwa anaweza, hata kama alikuwa na hofu na wazo lake kwa kumtia moyo na kumuamini itampa ari ya kulifanyia kazi vizuri zaidi.
Wakati mwingine tunaweza kuwa tunazima ndoto za akina Mengi wengi tu bila kujua kuwa kwa support yetu wangefika mbali sana. Hata akishindwa kwa mara ya kwanza mtie moyo na mwambie ajaribu tena na tena na atafanikiwa. Sio ndio unaanza na maneno kama "nilijua tu usingefika kokote"!!
Kama ulimuamini na kumchagua yeye kati ya wengi,basi hauna budi kuyaamini mawazo yake pia. Kuwa msaidizi ambae kila wakati atajivunia kuwa nae, hata akikengeuka akikumbuka mazuri yako mengi hakika atajirudi tu.
Biashara!!? Kwani lazima hiyo biashara mfanye na waume za watu? Hivi nyie mnajua kua mume anauma
Mazoea ya kibiashara hatuachi.