Polisi jamii
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 2,604
- 1,381
Onyo: Usisome Post hii kama umewahi kutendwa na Mwanamke, utaugua Presha na stress usijue la kufanya
Nazungumza na wanawake wote bila kujali umri
Nasema hivi, ninyi ni Mama zetu, ni wake zetu pia. Vilevile ni dada zetu na shangazi zetu kwa upande mwingine Lakini wanawake Mungu anawaona mjue
Jamaa yamemkuta, yamemkuta ndivyo unavyoweza kusema, Siri ya Mtungi kweli ajuae Kata, Hakika Moyo wa mtu ni kichaka. Kikulacho ki-nguoni mwako kweli, Wanasema “Usiusemee moyo” eti unapendwa... Zaidi ya yote naweza tu kusema kuwa Wanawake Mungu anawaona. Japo naamini si wote wa aina hii.
Wacha nianze hivi nifuate hapa Tirirka:
Jamaa yetu mmoja anazo pesa nyingi sana, alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe alioa mwanamke aliyeamini ni mzuri sana, Wakati wakiwa wachumba kama ilivyo ada kwa wadada wengi huwaambia wenza wao kuwa “Tusishiriki tendo la ngono hadi tuoane” Kumbe wakati huo huyo mdada anako kajamaa kamoja sehemu nyingine anakokaamini na kukapenda sana tena kwa dhati. anachokifanya ni kutafuta Maslahi kwa huyu mkaka.
Jamaa akavumilia, mwanzo mwisho, huku akisema moyoni kuwa “Kuku wako utamshikiaje Manati?” Alijitahidi sana kuonesha kuwa anajali, lakini yule dada asivyo na adabu, aliendelea kufanya Ngono na rafiki yake anayehisi kumpenda huku mipango ya Ndoa Ikipangwa kwa huyu anayeitwa “Mchumba”, Mipango ikakamilika, ikawa Mwezi, Ikawa wiki, mara ikawa siku na hata saa na baadae dakika na sekunde halisi ya kufunga ndoa ikafika. Ndoa ikafungwa John na Jane (Si majina halisi) wakawa mke na mme. Lakini ujue na kukumbuka Jane alikuwa na Mpenzi aitwae Joseph, (Si jina halisi)
Kumbe kipindi kile siku ilipokwisha kukaribia kuoana, Jane akahakikisha anabeba Mimba ya Joseph, kwahiyo Jane alifunga Ndoa akiwa na Mimba ya wiki moja 'aliyopachikwa' na Joseph. Kipindi cha Fungate (Honey moon) John akajitahidi kufanya alichokiweza akijiaminisha kidume cha mbegu, kumbe Ukweli aliujua vema Jane kuwa tayari anacho Kiumbe. Ikawa wiki, hata mwezi, Jane akaonekana ni Mjamzito, naye John akamshukuru Mungu sana. Ikafika Miezi Tisa ambayo hata hivyo John asingeweza kugundua lolote. Basi Mtoto akazaliwa wa Kiume, akafanana na yule jamaa (Joseph) ambaye hata hivyo John hamjui.....
Jane na Joseph waliendelea na mawasiliano, Jane alihakikisha wakipanga kuzaa na Mmewe, siku za hatari anamfuata Joseph, anatimiza lengo la Jane, mara mimba ya Pili ya Joseph ikilelewa na John ambaye naye alijiaminisha ni ya kwake. Mara Mtoto wa Pili akazaliwa akifanana na mtoto wa kwanza naye alikuwa wa kike. John akiamini ni wanae, vile vile Joseph akijua fika kuwa Jane amezaa watoto wake wawili (Judicar na Judith), ikawa hivyo, John alijitahidi kuwahudumia watoto wale akiamini ni wake. Mara wakapanga tena kuzaa mtoto wa tatu. Kama kawaida yake Jane akamfuata Joseph, wakafanya walichokikusudia
John akalea Mimba akiamini ni yake, Akazaliwa Mtoto wa tatu wa kike aliyeitwa jina Justina. watoto wakaendelea na maisha, huku Jane akiendelea kumpa taarifa za kukua kwa watoto wale ndugu Joseph, akawa anawapiga picha kila hatua, Wakaendelea kuchati na Joseph, wakipanga mpango mzuri wa kuwakutanisha watoto wale watatu na mmoja ambaye Joseph alizaa na mkewe halali wa ndoa. John wala hajui lolote, Kilichomshangaza John ni ukali wa mwanamke kwa mmewe kushika Simu.
Ndipo siku moja Mkewe Jane alipojisahau na kuacha simu Mezani, akiwa bize kufanya Usafi, na tayari alishaaga kwa mmewe kuwa baadae angetoka kwenda sehemu na kuruhusiwa. Sasa wakati akiwa bize, Joseph akatuma meseji kwa Jane, bahati njema siku hiyo John aliisoma Meseji "Hakikisha unawapiga picha wakiwa pamoja wote watatu.” John akashangaa, ikambidi ajibu “Hapana kwa leo ni ngumu” Joseph akajibu tena “Jitahidi bwana si unajua nataka nizweke picha pamoja nataka wanangu wafahamiane…”
John aka-MUTE, wala hakuonesha ghadhabu yoyote kwa mkewe, alipomaliza kazi akamwambia mkewe, “Mama Judicar, Andaa watoto tutoke mara moja” Wakaenda straight hadi Hospital Jane akashangaa John anataka kupima DNA, Maajibu yalikuja watoto wote watatu si wa kwake, Ndipo John akamwambia Mkewe, “Jane tafadhali soma hizo meseji zako zilizotoka kwa Lizzie…” Kumbe Jane alimsave Joseph kama Lizzie, Ebhana eeeee wadada Mungu anawaona.
Jane ikabidi akiri, na kumweleza ukweli Mmewe, kuwa “Nilishindwa, sikutaka kabisa kuchanganya watoto kuwa na baba tofauti” John alipofika home, akamwambia Jane ampigie simu Joseph, kuwa aje kumchukua waelekee kwenye miadi yake na amwambie Mmewe hayupo. Akafanya hivyo, Joseph alipokuja, Jane alimkaribisha Ndani, Ndipo John akatoka chumbani kuja sebureni, na kusema maneno yafuatayo:
“Ndugu yangu umenikosea sana, yaani umenivua nguo kabisa, lakini nashukuru kuwa haya mambo yamejulikana mapema, sasa Mchukue huyu mwanamke, na watoto wako nenda kwa Amani….”
Joseph hakuamini aise, kweli wakaondoka, na wala Jane hakuonesha kuomba Msamaha, wakaondoka, John hakupata usingizi kabisa siku mbili mfululizo, akaona njia pekee ya kupata Usingizi, ni kukandamiza Mvinyo kwa wingi, na kwakuwa alikuwa na Mali nyingi basi alifanya hivyo na kuwa Mlevi wa kupindukia, Lakini Mali zake zikaonekana kuanza kutapakanywa, ndipo Rafiki zake na nduguze wakaamua kumshauri atulie ikiwezekana Aoe mke mwingine, Weee jamaa hataki, nduguze wakamkumbusha kuhusu kufilisika hilo la kuacha Pombe akalikubali lakini chini ya usimamizi mkali.
Now ametulia, akili imerudi na sasa amekuwa mtulivu sana wa akili na mali zake zimerudi mahala pake, Lakini hataki kusikia kiumbe aitwae “Mwanamke” ameathirika kisaikolojia kabisa. Hadi sasa ana Miaka Mitano tangu kimkute kisanga hiko. Lakini wanawake ninyi ambao mnafanya aliyoyafanya Jane, Mungu anawaona, yaani hiki kisa kimeniuma sana kwa kweli, Jamaa ukimwambia habari za Wanawake hataki kabisa, anashangaa kabisa akisikia kuna watu wameoa wake Zaidi ya mmoja.
Maswali:
a) Je umejifunza nini katika story hii ya ukweli kabisa?
b) Je Unahisi Jane na Joseph waifanya vema kuondoka pale
c) Je Ingekuwa wewe Ungefanyaje?
d) Je unadhani John alikuwa sahihi kumfukuza Jane na watoto?
e) Je Wewe unashika simu ya mke/mme wako muda wowote upendao?
f) Ni kwa kiasi gani mn
ashirikiana ki uwazi katika matumizi ya simu na mwenza wako?