Wanawake jifunzeni mapishi, mnatia aibu

MFALME WETU

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
3,426
8,517
Wanawake wa siku hizi sijui mmekuja kuwaje kwenye suala la mapishi ya jikoni. Ivi mnajua kwanini mwanaume akioa waswahili tunasema Kavuta Jiko?

Unakuta kijana umeopoa dem au mchumba wako kabisa yupo geto ila unalazimika kwenda restaurant kutafuta msosi ili upeleke mle pamoja kisa mpenzi wako hajui kupika. Unaweza kuta foleni ya vijana wa kiume kwenye vibanda vya chips ukazani ni wao wanakula kumbe wameagizwa na wale wa kuitwa pisi kali uko magetoni.

Kitu pekee mnachojitaidi kupika ni wali [kwenye rice cooker] na kuchemsha chai kwenye jagi.

Kuna wengine baadhi wapo kwenye ndoa ila linapokuja suala la kupika kwao ni kipengele, wanawapakazia wafanyakazi wa ndani.

Tatizo ni kubwa sana hususani kwa hawa wanawake waliofika chuo, tena usiombe ukute kabandika tips kwenye kucha.!!

Basi kama huwezi kupika ugali jitaidi kabla hujaolewa angalau uwe unajua kupika chapati laini za kusukuma.!! na pakujifunzia ni ukuku magetoni maana uko majumbani kwenu kila kazi mmewatelekezea wadada wa kazi.!!

Mnafanya baadhi ya wanaume tunaojielewa na waowaji kuwa hit & run.

Screenshot_20231022_183653.jpg

Mada za kuwadhalilisha mama na dada zetu ifike mahali zikomeshwe .. Si kila kitu akiweze vingine ni kusaidiana.. Swala la mapishi hata mwanaume anaweza kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaili kaka umekosea kwaiyo unataka kusema tuwekeane zamu na mwanamke kuhusu kupika na kama sina uwezo wa kuweka house girl inakuaje tena unakuta maali yenyewe wamekomaa millioni 3 hawajapunguza hata mia alafu jitu lenyewe box kupika zero
 
Kwanza: Kama hujamuoa usimpe majukumu ya mke, kupika ikiwemo si ndivyo tulivyojadili katika nyuzi kibao humu?

Pili: Kama ni mke na umemuoa umegundua hajui kupika mrudishe kwao akajifunze.

Tatu: Wanawake wote wa JF tunajua kupika, kwa reference zaidi kaangalie uzi wa vyakula. Hivyo hii mada haituhusu na kwa heshima na taadhima tunaomba muwaambie watu wenu huko huko.

Nne, wanaume wa JF wengi wenu mnafanya Online gender based violence (OGBV) as if hao wanawake zenu hawana jema hata moja.

Mwisho siku nikigundua shemeji yenu yupo humu, ntampa likizo ya miezi 6, agghr wanaume humu mna gubu bwana!
 
Kaa chini kwanza utulie uandike polepole

Jifunzeni kupika, iyo ni sunnah kwa mwanamke.!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom