mbongo_halisi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 6,911
- 5,326
habar wadau jf..
binafsi napenda kutoa haka ka kisa cha kupigwa kelubu(kibao)na mwenza wako a km ni wife or girlfriend ..ilikuwaje,kwa sabab gan na baada ya kupigwa ulifanyaje/ulimfanyaje km ni wife au girlfriend..
binafsi ilikuwa iv siku moja kulikuwa na shereh ya kampun yetu flan iv ya kuadhimisha miaka kadhaa toka kampun ianze kaz hapa tz. sasa c unajua tena siku ya shereh kila mfanyakaz anakuja na mwenza wake km ni wife au girlfriend tu..mi nilikuwa na girlfriend tu cz nilikuwa bdo cjaoa.
sasa wakat shereh kuanza na kuendelea ikafika muda wa kuruka debe(kucheza music) ..nashereh ilikuwa usiku sasa ulivofika muda wa kuruka debe. shemej yenu bhn alinikazia kucheza wote na alidai yy ayiuko interested na kuruka debe mbele ya hadhira ya watu sbb anajisikia aibu..na waka huo mm napenda kuruk debe toka utoto madisco yalikuwa hayanikosi..
sasa kil nikimladhimisha tukacheze hatak, hatak kabsa..mi c nikamuacha nikaingia kati kuruka debe bahat nzur bhn ple kazin kulikuwana wanawake weng na wazur sana..na nilikuwa mi ni mchesh kwao sa baada kuona naruka debe pekee yng walianza kusogea na kuanza kugombania kucheza na mm bhn.
mtt wakiume nikaona nishikilie tu ile mizigo ple sasa kosa iilikuja hapa mi wakati na cheza na wale wanawake tofaut tofaut shemeji yenu bhn roho ikawa inamuuma wivu ukamjaa bhn..akaanza kunisumbua bhn kupitia cm akawa ananitext kunizuwia niache kucheza nao sa akatuma text km mara nne iv mi nikampuzia bhn..
kilichofuata si akanifata ple nilikupokuwa na cheza mzika na kunipiga kelubi (vibao vya usoni) mbil heavy yan nilikuwa nimevaa miwan mpk ikaanguka na kuvunjika kabisa.hahaaaaaaa nilipatwa na hasira bt nikabid nizuie tu hasira zang na nikaomdoka ple ukumbin na kurud zang hom..sikuongea nae siku tatu bt aliniomba msamaha na yakaisha so nau tuko vizur tu..mapenz yanaendlea..
vp kwako ushawah pigwa vibao..na mwenza wako ..wife au girlfriend tu na ilikuwaje na kwa sabb gan..tuambie kisa chao..
Kwangu ilikuwa hivi; wakati natoka na mwana Mama mmoja wa kipare miaka ya nyuma, alikuwa na michezo ya kishirikina sana. Yeye alikuwa anapenda sana niende kula kwake kila mara hata nikimtoa out alikuwa anachukia na kuomba kile chakula akichukue akipeleke nyumbani. Mwanzoni nilifikiri ni kunijari mimi tu, kumbe yule Mama alikuwa na kamchezo fulani hivi. Yaani alikuwa anapenda kuwatega wanaume na madudu washa (ushirikina) kwenye vinywaji na vyakula. Mwenzie nilishapikwa toka kwetu (Tanga), kila aliponiwekea madudu washa niligundua na kujifanya nakula kumbe nilikuwa sili, navunga tu. Siku ya siku ya siku alifikiri dawa zimenikolea, akaniambia anataka milioni tano sasa hivi, nikamchunia huku machale yakaanza kunipanda. Akasema tena nikishampa milioni tano anataka pia nimnunulie kiwanja mwezi ujao kwani anaona viwanja vinahadimika sana....nikajifanya kulala na kumwambia sijisikii vizuri. Akaniletea na maji ya kunywa ambayo alikuwa katia madudu washa Zaidi, nikamwambia weka tu pembeni nitakunywa na dawa za kichwa ambazo nilikuwa nazo. Alipotoka chumbani nikamwaga yale maji na aliporudi aliona kama namalizia kunywa, alichekelea sana. Ghafla akawa na hasira akanikunja na kunichapa vibao eti ananidai milioni tano na kiwanja, na kutaka nimlipe kesho na kiwanja apate si chini ya wiki moja kwani kipo tayari. Story ni ndefu ila sikumtimizia mahitaji yake nikaachana naye. Baada kama wiki hivi nikaanza kupata mauzauza kazini na nyumbani, maana kile kichwa kilizidi kuniuma na hospitalini waliniambia sina ugonjwa wowote. Nikaenda mpaka Muhimbili kufanyiwa scan ya kichwa, holaaaaa. Rafiki yangu mmoja akawa concerned ndipo akanishawishi twende kwa Mze flani kule Kigamboni (Mji Mwema) kwa mtizamo Zaidi. Jamani wanawake wa Kipare ni nuksi kweli kama ndugu zao wachagga tu.....yule Mze akaangalia kwenye darubini na kuniuliza kuna mwanamke unatembea naye kijana? Akaniambia huyu mwanamke ni mshirikina na anapenda sana kutumia marijali kwa manufaa yake, hapo ulipo umeshakula nyama ya bundi, mjusi, nywele, na sindano....kakufanya hivi ili awe anakutumia wewe bila kujitambua, bahati uliyo nayo ni kwamba ulishatengenezwa toka kwenu na ndiyo maana alikasirika alipokuomba mahitaji yake wewe hukumpa kwani alidhania kakupata. Nikaduwaaa, Mze akanipa dozi ya kujizimua na sasa niko fiti na sina tena hamu na wanawake wa kipare wala wachagga.