Habari wana JF,
Moja kwa moja niende kwenye Mada,
Husika katika miaka ya hivi karibuni kumetokea wimbi kubwa la wanaume kuanza kujipodoa sana ili tuu kuweza kuwavutia wanawake yani wamekosa kabisa mbinu za kuwafuata wanawake na kuona njia inayofaa ni kuanza kujipodoa sana ili tuu walete mvuto kwa wanawake.
Kiukweli jambo hili linanisikitisha sana coz kadri miaka inavyozidi kwenda ndivyo idadi kubwa ya wanaume wanaodumbukia kwenye mambo ya ajabu inaongezeka. Mwanaume unapaswa kuwa msafi na nadhifu tuu inatosha lakini mambo ya kujipodoa sana hayo ni ya kike.
Wanawake ndio wanapaswa kujipodoa ili kutuvuta lakini mvulana unapojipodoa ili kuwavutia wa kina dada unakuwa unafeli sana.
Nimalizie kwa kusema
..*hawawavuti wanawavutia*