Wanasheria na wadau wa sheria naomba mnieleweshe kifungu hichi cha katiba

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
3,199
4,319
katiba ya jamhuri ya muungano ya mwaka 1977 yenye marekebisho madogo,nimeona katika kifungu namba 34 ibara ndogo ya sheria 4 na 5 yenye kipengele a na b,nimepata ugumu kufahamu naomba nifahamishwe.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa
ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu
madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii
hayatahesabiwa kwamba-
(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria
yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au
mamlaka yoyote ambayo si Rais; au
(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya
kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka

hapo kwenye sheria namba 5
 
Back
Top Bottom