Wanaosali Jumuiya vs wacheza pool table, kuna tofauti?

Uzuri ni kuwa jumuiya nyingi hukutana WEEKEND!
Au unataka WEEKEND ziwe siku za kazi?
Yaani Wasabato wasiende kanisani Jumamosi ili kuokoa muda au wakafaye mikutano ya mtaa/kijiji?
Na wale wa Pengo,Dr.Shayo na akina Kakobe nao wasiende kanisani ili kuokoa muda,wakafanye kazi za kipato?
Let this be your worst thread ever!
I pray to Allah that you resume your normal health reasoning.
 
Utetezi wenu wengi ni zero.Sijaona sababu ya msingi ya watu kukutana nyumbani kwa mtu mmoja mmoja tena kila week-end kujadili mambo yale yale kwa kisingizio cha kufanya ibada.Ni wangapi kati yenu mnaotetea utaratibu huu mmetumia mikusanyiko hii kuchukua namba za simu za mabinti kwa lengo la kukiuka amri ya saba?

Ni lini tumewahi kutumia Jumuiya zetu hizi kukusanya michango ya kwenda kusaidi yatima au kuhudumia wagonjwa mahospitalini?
 
Inawezekana una mawazo mazuri lakini sidhani kama utaeleweka, kiujumla una point labda jaribu kulekebisha baadhi ya vipengele kwenye hoja yako, Mh spika naomba kuwasilisha
 
watu wengine hua wanajiandikia tu ili wapate comments nyingi. maswala ya Mungu acha masihara nayo mkuu usilete siasa katika imani. kwahiyo na wanaoswali swala tano kila siku wana iq ndogo na ni wavivu? hii mada iache unazidi kujiaibisha.
 
Fahamu kuwa maisha yanahitaji vitu vingi na siyo uchumi tu. Sina muda wa kutosha kuandika ili nikuelimishe vizuri ila ninahakika ningekuonesha ulivyopotoka na baadae ukajiona wewe ni KIAZI tu.
 
Hivi hatuwezi kuishi pasipo kuwa na huu utaratibu wa kusali kwa jumuiya huku mitaani.Kusali makanisani hakutoshi mpaka tukutane kwenye majumba yetu siku za week-end na hata kila siku kwa baadhi ya maeneo kwa lengo tu la kusali kwa utaratibu huu wa Jumuiya?

Wanaocheza pool table wanatakiwa kukamatwa kwani wanapoteza muda wa kufanya kazi,je hawa wanaokutana saa 12 kila Jumamosi na kwa baadhi ya maeneo nasikia ni kila siku,huku si kupoteza muda wa kufanya kazi?

Hivi lengo la kusali Jumuiya si kukusanya sadaka tu?Nini kipya kinachofanyika katika hizi Jumuiya tofauti na makanisani kwetu?

Alafu hivi mtu unawezaje kushiriki kwenye Jumuiya hizi lakini ukashindwa kushiriki mikutano ya kijiji/mtaa kwa maendeleo ya kijiji/mtaa wako?

Kama hizi Jumuiya ni muhimu sana,kwanini adhabu hizi za kijamii tunazozitoa kwa watu wasioshiriki Jumuiya hizi pia tusizitoe kwa wale wasioshiriki mikutano ya maendeleo ya mitaa au vijiji vyetu kwani hata hii mikutano nayo ni muhimu pia?

Utaratibu huu nimeuona hapa Dar leo hii nikakumbuka na huko mikoani hali ni hiyo hiyo hivyo nikajikuta najiuliza haya maswali.Alafu katika nchi za wenzetu mambo haya yanafanyika?Nina hakika miaka ijayo haya mambo yatakuja tu kutoweka maana sioni ulazima wake.

Duh, huyu Ndugu sijamwelewa kabisa. Kwani Jumuiya zinatumia muda gani kusali?! Nivyofahamu mimi Jumuiya za kikatoliki hukutana Jumamosi, nadhani kuanzia au kati ya saa 12.00 asubuhi hadi saa 1.00 hivi asubuhi yaani muda wa karibu saa moja. Sasa utahusishaje Jumuiya na Pool table ambao kila siku huchezwa tena basi saa zote?

Sijamwelewa huyu Ndugu, au unataka kuleta suala la udini hapa?
 
Mwataka kuwaambia watu wasisali swala tano eeh! Eti wanapoteza muda wa kufanya kazi sio? Ganja bana.
 
Fahamu kuwa maisha yanahitaji vitu vingi na siyo uchumi tu. Sina muda wa kutosha kuandika ili nikuelimishe vizuri ila ninahakika ningekuonesha ulivyopotoka na baadae ukajiona wewe ni KIAZI tu.
Ni lini Jumuiya zenu hizi zimewahi kukutana hiyo asubuhi na mkakusanya sadaka zenu na kwenda kusaidia wagonjwa/yatima na wengine wenye matatizo kama mungu anavyotaka?
 
Mkuu, haya ni matokeo ya kuuvuruga mfumo uliokuwepo wa nyumba kumi kumi ambapo kila mkaazi, bila kujali dini yake alihusika kwenye shughuli za kitaifa kwa siku maalumu ya wiki. Tulipojichukulia huo utaratibu wa kitaifa na kuufanya wa kichama tukavuruga. Sasa hata ki-chama umekufa.

Muendelezo huu unaingiza udini ambao kitaifa tuliukemea kwa nguvu zote. Naona siku hizi kila dhehebu wanasali peke yao na hata mnapokutana kwenye mtaa kwa shughuli za kitaifa, unaweza kujua haya makundi kwani mijadala inaungwa mkono au kupingwa kufuatana na makundi hayo. Wengine wanasahau kuwa sio mkutano wa jumuia wanaanza kikao kwa kusali sala ya dhehebu lao.

Ki-ufupi ni kuwa huku mitaani nchi imegawanyika ki-madhehebu. Huku mitaani, madhehebu yamejiundia utawala wao sambamba na wa sarikali ambao ni mdhaifu na unadhoofika kila siku. Miaka michache ijayo tutakuwa na serikali za mitaa zinazoundwa na madhehebu ya dini. Hapo ndipo, ukatoliki, u-lutheran, usabato, u-answar sunna, ubakwata, upentekoste, etc utakapovunja U-Tanzania rasmi.

Asante
 
Ni lini Jumuiya zenu hizi zimewahi kukutana hiyo asubuhi na mkakusanya sadaka zenu na kwenda kusaidia wagonjwa/yatima na wengine wenye matatizo kama mungu anavyotaka?

Ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Nahisi kama unataka serikali ipange na kusimamia utaratibu wa watu kuabudu!
Hizi ni athari za kuzungusha mikono hewani. Hapo bado hamjaanza kulala chali na kuzungusha miguu hapo 2020.
 
Mwataka kuwaambia watu wasisali swala tano eeh! Eti wanapoteza muda wa kufanya kazi sio? Ganja bana.
Kusali kwenyewe mnasali kama fashion tu na mazoe ila matendo yenu ni bora hata wapagani!

Tumejijengea imani ya kipuuzi sana eti kuwa kusali swala tano na kwenda Kanisani ndio tumemaliza kila kitu wakati kitakachotuhukumu ni matendo yetu.

Unatoka Kanisani au Msikitini na gari lako una mkutana kilema njiani huku mvua ikimnyeshea unampita kama humuomi?

Unatoka kwenye sala yako dakika mbili baadae unaenda kuzini!

Sisi binadamu ni wanafiki wakubwa bora hata wanyama wasiomjua mungu kuliko sisi tuliopewa akili na mungu.

Watu ni mabingwa wa kutetea imani zao lakini ni mabingwa wakubwa wa kutenda dhambi kila kikicha tena pasipo hata kujutia dhambi zao!
 
Inakubidi uwe mwehu Fulani ndio unaweza ukakaa kuandika alichoandika mleta bandiko. Au hii ni laana? Maana mleta bandiko hakuwa hivi huko nyuma.
 
Nakubaliana na mtoa MADA kwa mara ya kwanza 100% kamata like mkuu
 
Mkuu, haya ni matokeo ya kuuvuruga mfumo uliokuwepo wa nyumba kumi kumi ambapo kila mkaazi, bila kujali dini yake alihusika kwenye shughuli za kitaifa kwa siku maalumu ya wiki. Tulipojichukulia huo utaratibu wa kitaifa na kuufanya wa kichama tukavuruga. Sasa hata ki-chama umekufa.

Muendelezo huu unaingiza udini ambao kitaifa tuliukemea kwa nguvu zote. Naona siku hizi kila dhehebu wanasali peke yao na hata mnapokutana kwenye mtaa kwa shughuli za kitaifa, unaweza kujua haya makundi kwani mijadala inaungwa mkono au kupingwa kufuatana na makundi hayo. Wengine wanasahau kuwa sio mkutano wa jumuia wanaanza kikao kwa kusali sala ya dhehebu lao.

Ki-ufupi ni kuwa huku mitaani nchi imegawanyika ki-madhehebu. Huku mitaani, madhehebu yamejiundia utawala wao sambambamba na wa sarikali ambao ni mdhaifu na unadhoofika kila siku. Miaka michache ijayo tutakuwa na serikali za mitaa zinazoundwa na madhehebu ya dini. Hapo ndipo, ukatoliki, u-lutheran, usabato, u-answar sunna, ubakwata, upentekoste, etc utakapovunja U-Tanzania rasmi.

Asante
Ubarikiwe sana.Umeitendea haki mada hii.
 
Jumuiya za Katoliki zilianzishwa miongo michache tu iliyopita. lengo kubwa lilikuwa kuimarisha kanisa hasa baada waumini wengi kuhamia madhehebu ya kiprotestant.
Kwa hiyo zitaendelea. Wahudhuriaji wakubwa ni wamama wazee na watoto. wababa wengi hawahudhurii. Ni kwa nini? labda wana mawazo kama ya mtoa mada.
Jumuia ziendelee. ila mbele ya safari zitakabiliwa na tatizo la mahudhurio kama ilivyo ulaya ambapo hata makanisa hayana waumini. waafrika wanabadilika pia.
kitu kimoja nimekipata kwa mtoa mada mada ni kuwa sio lazima wahudhuriaji wakawa watu weme. kwa bahati mbaya kuna wengi ambo hujitokeza kama waumini wema lakini maovu yamewajaa. si kila aliitaye jina la bwana ataingia mbinguni. Chunguzeni kwaya za makanisa mtagundua kitu.
Watu wanaweza kuwa wema na waadilifu bila ya kwenda jumuiya ingawa wakienda pia watakuwa wema zaidi.
 
Halafu huyu huyu utamkuta uwanjani anabwata na kjiita kamanda huku akililia katiba ya warioba kipengele cha maadili...unadhani maadili yanakuja kwa kuandikwa kwenye katiba??
 
Back
Top Bottom