Uchaguzi 2025 Wanaodaiwa kuwa ni polisi Dodoma wafanya upekuzi nyumba ya Honesty Msacky Mwanachama wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watu wanaodaiwa kuwa ni Askari wa Jeshi Polisi mkoa wa Dodoma wamefanya upekuzi katika nyumba ya mwanachama na kigogo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Honesty Msacky nyumbani kwake Nzuguni B kwa madai ya kuwa anamiliki silaha kinyume na taratibu za nchi.

Akizungumza baada ya upekuzi huo nyumbani kwake Msacky amesema watu walifika nyumbani kwake saa 12:00 na kuanza kugonga geti huku wakimuita jina la Baba Glory ambalo halifahamu.


"Baada ya kuingia getini wakalazimisha nimuite balozi hali ambayo niliwagomea na kuwaambia sina balozi kwani yeye ni mwanachama wa Chadema hivyo baada ya hapo wakaingia ndani na kuanza upekuzi usio na ustarabu," amesema Honesty.

Soma pia: Jeshi la Polisi wamefika nyumbani kwa Boniface, hapa Msakuzi kwa ajili ya upekuzi

Hata hivyo Msacky amesema anaamini kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa zipo hujuma mbalimbali za kisiasa za kuchafuana ili chama chake kisifanye vizuri huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Anania Amo akisema hana taarifa na tukio hilo.

Chanzo: EATV
masikini ccm bado wanatumia mbinu za kizamani sana ku deal na chadema
 
Huyu atakuwa gaidi ndiyo maana wamemshtukia aache uhuni atoe ushirikiano yaani yeye hana balozi anaishije kwenye mtaa wenye balozi huyo aiyepo ndyo balzi wake
Wewe utakuwa mwendawazimu. Balozi siyo kiongozi wa serikali mtaani. Huyo ni kiongozi wa CCM. Ni sawa uende kwa muislam halafu umwambie, amwite kiongozi wake wa jumuia ndogo ndogo.
 
Back
Top Bottom