Wananchi wa Uturuki wamegoma kuingizwa mkenge kama wa Libya

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,788
39,141
Wanaukumbi.










"Waasi' 6,000 wamekamatwa Uturuki.

Utawala nchini Uturuki umevamia kambi za kijeshi kote nchini kuwatafuta wanajeshi wanaoshukiwa kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyozimwa siku ya Ijumaa.Kambi za kijeshi zimevamiwa na kusakwa.

Katika oparesheni kwenye mji ulio magharibi wa Denizli saa chacha zilizopita kamanda mmoja wa kikosi cha jeshi na zaidi ya wanajeshi 50 walikamatwa.

Maelfu ya wanajeshi wamekamatwa.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu serikalini amesema kuwa jeshi limerejesha udhibiti katika asilimia kubwa ya kambi za kijeshi japo kuna baadhi ambazo zipochini ya usimamizi ya wale walionga mkono mapinduzi.

Majaji takriban 3000 ambao wanatuhumiwa kupinga serikali ya rais Reccep Teyyip Erdogan wamesimamishwa kazi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema kuwa bunge litaamua ikiwa litabuni sheria ya hukumu ya kifo.

Wale waliokamatwa wanatajwa kuwa wafuasi wa kiongozi wa kidini raia wa Uturuki anayeishi nchini Marekani Fethullah Gulen ambaye analaumiwa kwa kupamnga mapinduzi hayo.

Source: Turkey coup attempt: Some 6,000 people detained, says minister - BBC News
 

Attachments

  • 160716071806_turkey_army_624x351_reuters.jpeg
    11.8 KB · Views: 94
Raia wa kawaida ndio wenye nguvu na ndio walio muweka rais wao hapo.

Duhh ukweli waarabu wanapenda sana vita vya wenyewe kwa wenyewe .
Mwarabu kama hafurahii kitu ni kunyanyua mtutu
Au atatumia nguvu na hasari kutatua tatizo.

Hakuna ile tukae chini tusuluhishe
P.S Sio waarabu wote bali asilimia kubwa.
 
Njama... njama Njama nyekundu ilipangwa na MATAIFA manne (4 ) makubwa !!!
na mbili ktk hizo ni SupuPawa !! nafikir mtanielewa...............

Ritz
 
Wangeingia choo cha kike kama Libya vile , Syria bado ipo hali ya mpito. Sasa kama mwamerika amechukua mda Kutoa tangazo kumuunga mkono " rafiki yake Uturuki", alikuwa anasubiri nini ? Haiyumkini kuwa anamhifafhi yule anaetajwa kuwa ni kiongozi wa mapinduzi ambae anaishi huko marekani.
 
Jaribu kufunua vitabu usome upya nadhani ufahamu vita vya wenyewe kwa wenyewe Ulaya vimetokea sana zaidi ya hizo nchi za kiarabu.
 
Na we peleka pumba zako huko.
Hii mada inahusu nchi za Ulaya au Uturuki.

Na wapi nimeseme kwamba nchi za ulaya hazikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Usilete porojo zako.
Sasa wewe na mimi nani ana porojo kwani Uturuki ipo wapi?

Halafu unaposema waraabu wanapenda kuawana wenyewe kwa wenyewe uje na ushahidi.

Siyo kweli hata wazungu wanauwana wenyewe kwa wenyewe soma history.
 


si waarabu , hao ni waturuki .

Hata hivyo anza kuwajua wazungu nini wanafanya huku kwenu Afrika

Gonga hapa

The French African Connection
 
idara ya usalama wa taifa ya Uturuki ilikuwa wapi kuona intelejensia ya mapinduzi hayo..?
 

Waziri mmoja wa Serikali ya Uturuki ameituhumu Marekani kwamba ndiyo ilihusika kusuka mipango ya kutaka kuipindua Serikali halali ya Ukuruki!!! John Kerry amekanusha vikari tuhuma hizo.

Swali ni ,je, uhusiano wa Uturuki na NATO specifically the USA utakuwa wa kiwango gani - kuna cha kuaminiana tena hapo au Uturuki italazimaka kuwa karibu zaidi na Urusi na kuacha kutumiwa na US kuihujumu Syria.
 
Sasa wewe na mimi nani ana porojo kwani Uturuki ipo wapi?

Halafu unaposema waraabu wanapenda kuawana wenyewe kwa wenyewe uje na ushahidi.

Siyo kweli hata wazungu wanauwana wenyewe kwa wenyewe soma history.
Hivi hii topic inawahusu wazungu au Uturuki.

Kujibu swali lako ndio historia inasema wazungu walipigana.

Nchi ambazo ziko Middle East na North Africa wanapigana sasa kwa sasa na maanisha miaka hii ya elfu mbili.

Uturuki iko wapi unaweza ku Google usipende kutafuniwa kila kitu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…