Wananchi wa Rungwe mkoani Mbeya wakataa madawati baada ya kubaini yametolewa na mtu wa CCM

Hao ndio wanamkwamisha Magufuli, kwa kudhani kila Jambo ni siasa!
 
Hii nchi maajabu hayaishi! Tangu uchaguzi uishe ni mwendo wa vibweka na vibwanga! Sioni miaka kumi ijayo Tanzania tukiwa wamoja tena.
 
Aslimia kubwa ya shule za mby hakuna upungufu wa madawati na hata wananchi wakiamua kuchagishana kwao ni kitu kidogo sana tofauti na mikoa mingine
Acha uongo wewe, kwa nini wanafunzi wanakaa chini? si wangekuwa wamechangishana siku nyingi?
 
Madawati ni mali ya shule sio ya kijiji.Hao viongozi wa kijiji si waajiriwa wa shule wala wizara ya elimu.Hawana nguvu ya kisheria kuyakubali au kuyakataa madawati yanayopelekwa kwenye shule.Wakamatwe wote tia ndani .Fungulia kesi ya uhaini na uhujumu uchumi kwa mpigo na wafunguliwe kesi za kupora madawati kutoka eneo halali la shule na kuyapeleka kusikojulikana

Kama ile ya kifaru
 
Siasa za watu wasio jua kufikiri vizuri maendeleo hayana Chama hata kidogo
 
Madawati ni mali ya shule sio ya kijiji.Hao viongozi wa kijiji si waajiriwa wa shule wala wizara ya elimu.Hawana nguvu ya kisheria kuyakubali au kuyakataa madawati yanayopelekwa kwenye shule.Wakamatwe wote tia ndani .Fungulia kesi ya uhaini na uhujumu uchumi kwa mpigo na wafunguliwe kesi za kupora madawati kutoka eneo halali la shule na kuyapeleka kusikojulikana
Sawa kabsa na wale waliokataa misaada ya hospital ya mbunge wa chadema bukoba mjini hao vipi
 
Wananchi na viongozi wa kijiji cha Kifunda huko Rungwe mkoani Mbeya wamekataa madawati yaliyokabidhiwa na mkurugenzi wa halmashauri Busekelo wialaya ya Rungwe wakisema kuwa hawahitaji msaada huku wanafunzi wa kijiji hicho wakikaa chini.
Mwenyekiti na Afisa mtendaji wa kijiji hicho wamesema wananchi wameyarudisha baada ya kugundua kuwa madawati hayo yametengenezwa na diwani wa CCM.
Diwani wa kata hiyo huyo amesema kuwa hayupo kuwafurahisha wananchi ila anatekeleza sera ya serikali

Yaani pamoja na mikwara na mbwembwe zote za Magu lakini bado wananchi wanaikataa CCM na maagizo ya serikali yake.

CCM ni sikio la kufa hata aje Malaika itakataliwa tu
 
Wananchi na viongozi wa kijiji cha Kifunda huko Rungwe mkoani Mbeya wamekataa madawati yaliyokabidhiwa na mkurugenzi wa halmashauri Busekelo wialaya ya Rungwe wakisema kuwa hawahitaji msaada huku wanafunzi wa kijiji hicho wakikaa chini.
Mwenyekiti na Afisa mtendaji wa kijiji hicho wamesema wananchi wameyarudisha baada ya kugundua kuwa madawati hayo yametengenezwa na diwani wa CCM.
Diwani wa kata hiyo huyo amesema kuwa hayupo kuwafurahisha wananchi ila anatekeleza sera ya serikali

NI UWONGO ULIOKUBUHU MADAWATI ANAKABIDHIWA. MKUU WA SHULE KAMA WALIKABIDHIWA WANANCHI WANA HAKI YA.KUYAKATAA KWAVILE WAO SIO WALENGWA
 
Aslimia kubwa ya shule za mby hakuna upungufu wa madawati na hata wananchi wakiamua kuchagishana kwao ni kitu kidogo sana tofauti na mikoa mingine
Mhhh, unafurahisha sana, sasa kama hakuna upungufu wa madawati imekuwaje wamepelekewa hivyo viti?
 
Sawa kabsa na wale waliokataa misaada ya hospital ya mbunge wa chadema bukoba mjini hao vipi

Waliokataa hiyo misaada ni wanakijiji ilipo hiyo hospitali au ni madaktari?
Madawati yamekataliwa na wanakijiji sio walimu.Ingekuwa ni walimu hilo ni swala jingine lakini wanakijiji! Wao si walimu na si waajiriwa wa hiyo shule.Madawati yalikuwa ya shule sio ya kijiji
 
Wananchi na viongozi wa kijiji cha Kifunda huko Rungwe mkoani Mbeya wamekataa madawati yaliyokabidhiwa na mkurugenzi wa halmashauri Busekelo wialaya ya Rungwe wakisema kuwa hawahitaji msaada huku wanafunzi wa kijiji hicho wakikaa chini.
Mwenyekiti na Afisa mtendaji wa kijiji hicho wamesema wananchi wameyarudisha baada ya kugundua kuwa madawati hayo yametengenezwa na diwani wa CCM.
Diwani wa kata hiyo huyo amesema kuwa hayupo kuwafurahisha wananchi ila anatekeleza sera ya serikali

KWA HIYO NI BORA WATOTO WAO WAKAE CHINI?????? Basi wasilalamike kwa 'bora elimu' watakayopata watoto wao. Ukweli kwa hili sina tafsiri bora zaidi ya Ujinga uliokithiri
 
Back
Top Bottom