The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 746
- 2,095
Hii ni picha ya bango la mradi wa ujenzi na ukarabati wa kilomita mbili (2) Goba kwa Awadhi ambayo imesambaa kwa kwenye mitandao ya kijamii.
Mradi huu ni wa ukarabati na ujenzi wa mitaro ambapo unatokana na nguvu za wakazi wa eneo hilo.
Inaelezwa wakazi hao wamekubaliana kujenga mitaro kwa kutumia zege na makadirio ya bajeti ni Shilingi milioni 40 kutoka kwa wakazi 95 ambao wameahidi kuchangia. Hadi sasa, zaidi ya Shilingi milioni 16 zimekusanywa, na ujenzi umeshaanza.
Sema tofauti na mabango mengine ambayo mara nyingi yamekuwa na ujumbe uliozoeleka kwamba UKIMWI unaua, bango hili limehitimishwa na ujumbe wa “Tuchange wote kujenga barabara yetu”.
Pia inasemekana kuwa mjadala huo umewaibua viongozi wa mtaa ambao waliwashawishi wananchi kuliondoa bango hili bila mafaniko. Wananchi wanasema kuwa endapo watalitoa, basi viongozi waitishe mkutano kuelezea barabara hiyo itatengenezwa lini.
Uamuzi wa wananchi wa Goba wa kujikomboa kwa kujenga barabara yao wenyewe ni ishara ya ujasiri na kujitolea katika kuleta mabadiliko katika jamii yao. Hii ni hatua ya kipekee ambayo inaonyesha nguvu ya umoja na dhamira ya kuboresha maeneo yetu.
Je, mtaani kwenu mnachukua hatua gani kama barabara inazingua?