WanaJF mliochangia uzi wangu kuhusu Ujenzi wa Coco Beach, Rais Magufuli amekisikia kilio chenu kuhusu Sh. 14 Bilioni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
95,470
167,287
Kwanza kabisa namshukuru mh Rais Magufuli kwa usikivu wake, uwazi pamoja na ufuatiliaji wa hoja mbalimbali za maendeleo.

Pili nawashukuru wanaJf kwa umakini wenu katika kuhoji na kufuatilia mambo.

Juzikati nilishusha uzi hapa jamvini nikiwataarifu juu ya meya wa manispaa ya Kinondoni kumkabidhi mkandarasi mradi wa ujenzi hapo Coco beach wenye thamani ya sh 14 bilioni.

80% ya wachangiaji mlihoji hizo fedha zote 14b zinajenga nini pale ufukweni.

Na wengi mkaonyesha wasiwasi wenu kuwa huenda kuna ufisadi mkubwa umepangwa kufanyika.

Baada ya kupitia comments zenu na kuona uzito wake nikashusha uzi mwingine nikimshauri Rais Magufuli ampe usimamizi wa miradi ya Coco beach na Machinjio ya vingunguti mh Jaffo kwa kuwa uadilifu wake tumeona kwenye ujenzi wa Zahanati zaidi ya 350.

Itoshe tu kusema swala la Coco beach mh Rais Magufuli leo amelisemea na kukemea hata kitendo cha kutaka kuifunga beach na kuwaacha wajasiriamali hawana pa kwenda.

Ahsanteni nyote
Maendeleo hayana vyama!
 
Unajipa kik
Huku unajipenyeza
Mwisho wa uzi wako huo ungeweka namba yko ya Sim

Ova
 
Kwanini atumbuliwe?!
Kwani Wa morogoro alitumbuliwa kwa sababu ipi? Makonda, Mkuu Wa wilaya ya ilala na kinondoni pamoja na wakurugenzi wao na ma- DSO wanatakiwa ama kuondolewa au kuhamishwa na kushushwa cheo kwa uhusika wao Wa kadhia ya coco na machinjio ya vingunguti!
Awe fair kwa wote kwani Wa morogoro na wasaidizi wake na RPC wamemwagwa!
 
Sawa umesikika mkuu!
 
Hapo ndo nawaza kwakutumia njaa
 
Back
Top Bottom