mbatombato
JF-Expert Member
- Jun 25, 2016
- 441
- 245
Nchi hii kukaa chini haikuwepo wakati wa awamu ya kwanza ya uongozi Ila idadi ya wanafunzi ilikuwa ndogo either! Awamu ya kwanza shule ilikuwa eneo utakatifu, maana miongoni mwa majengo mazuri ktk miji, shule nazo zilikuwemo! Kwa wale wa mjini watakumbuka viti na meza za chuma vilivyokuwa vikichukuliwa na wauza karanga toka mashuleni, in fact madawati yalikuwa mengi kuliko idadi ya wanafunzi!
Awamu ya pili ndio ilianza kuonja joto la idadi kubwa ya wanafunzi na mzee mwingi alitoa fomu maalum za kuchangia madawati, na Harambee kadhaa ingawa shida haikupungua ilizidi kuongezeka! Mkapa na Kikwete walilikuza tatizo, si kwa nia mbaya bali ni kwa wema tu, baada ya kuongeza shule za umma zilizocreate more demands za madawati!
Anyway, anastahili sifa raisi na viongozi wenzake, lkn tusibeze kila juhudi za watangulizi, mfano ukimuona mnunua madawati ni shujaa na kubeza wengine waliojenga shule (Lowasa including) itakuwa sio fair!
Umesema kweli kabisa..