saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 5,091
- 7,510
Kuna habari iliandikwa humu JF jana na mdau wa huu mtandao kuhusu wanafunzi kusahihisha mitihani ya wanafunzi wenzao. Habari ilihusu shule ya msingi Kimandafu.
Kwanza naipongeza serikali yetu kwani kwa kweli ni sikivu sana, hongera serikali ya Samia Suluhu Hassan. Leo Asubuhi walifika wakaguzi kutoka wilayani, tunapongeza. Tatizo inavyoonesha wale wakaguzi aidha walimpa taarifa mwl. Mkuu kabla kuwa awaweke wanafunzi wake vizuri, maana mapema asubuhi walimu walipita kila darasa kuwaeleza wanafunzi ya kuwa mkiulizwa na wakaguzi kuwa mitihani yenu mnasahihishwagwa na wanafunzi mkatae waambieni ni walimu ndio wanatusahihishia.
Ni kwamba wale wakaguzi hawajui mbinu ya kufanya kazi yao, hawajui intelejensia au walifanya makusudi baada ya kuhongwa. Tukisema wakaguzi ndio wachawi wa elimu yetu tunakosea?
Pili, walivyopelekwa kunywa chai walimu walirudi tena madarasani kuwakanya wanafunzi kuwa mkiombwa makararasi yenu ya test muwaambie kuwa tumeacha nyumbani, wakaguzi hawakuwa na mbinu yoyote kupata ukweli?
Sasa hawa wana-qualify kuitwa wakaguzi? Au ni rushwa? Huu ni udhaifu, uzembe, dalili za rushwa kwa upande wa ukaguzi. Ila kwa ujumla tunaishukuru serikali yetu message sent and successfully delivered, maana wamewaahidi wanafunzi ya kuwa hakuna mwanafunzi atarudia kusahihisha tena mtihani wa mwenzake, haya ni mafanikio makubwa.
Ieleweke kuwa hakuna mtu ana muda wala sababu ya kuzusha uwongo humu mtandaoni, serikali ijue ya kuwa yanayoandikwa humu ni ya kweli kuhusu uhuni na uhalifu unaofanyika kwenye utumishi wa umma. Najua wameandika taarifa ya uwongo kwa mabosi waliowatuma.
Kama mnataka ukweli kusanyeni karatasi za majibu kutoka kwa wanafunzi maana usahihishaji wa mwanafunzi na mwalimu ni tofauti sana, kwanza unakuta wanafunzi wamefanya makosa katika kusahihisha na katika kujumlisha maksi. Tuheshimu majukumu yetu na kupiga vita uvivu na uzembe. Uzembe mkubwa uko kwa walimu wakuu, wamejisahau mno.