Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,038
- 22,714
Mzee wa Upako amenikera hata mimi.Ni kweli ulio wazi kwamba Mzee wa Upako anajihusisha na ulevi.Hii ina maana kwamba anawadanganya wafuasi wake kwa kuwa hakuna mtumishi wa Mungu wa kweli anayetumia kileo .Hili ndilo linalo waudhi walio wengi.Kwa nini adanganye watu kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu na kumbe sio?Lakini hata hivyo,mbona magazeti pia yamemuandika sana?Huyo ni mfa maji!Jana 'nilibahatika' kusikiliza mahubiri ya Mzee wa Upako kupitia Channel Ten!
Kwa kweli katika kuhitimisha mahubiri yake, mzee wa upako alionesha kuumizwa sana na maneno yanayoandikwa juu yake hapa JF na akasema amewakosea nini? Yani kufundisha maneno ya Mungu ndio imekuwa kosa.
Kwa kweli alionekana inside he is a broken man hadi nikamuonea huruma. Sasa kwa heshima na taadhima, ninawaomba wana JF tumpumzishe mzee wa upako angalau tusije kusika kajitia kitanzi kutokana na maneno na michango yetu juu yake...
Tumpumzishe kama tulivyompumzisha PM Majaliwa, maana naye alivyokuja speed na swala la Faru John likamtoa nduki mpaka sasa katulia tulii kama maji mtungini...