Chiwaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 5,726
- 3,762
Hivi hii kitu hutumika pia na jangwan?Leo nimesikia redio kuna taasisi hapa Tanzania itakuwa inakagua/inapima moshi wa magari kujua kama uko sawa kwa mazingira yetu, yaani vehicle emission standard.
Kwa nilivyosikia redioni hawa wapimaji wakiona gari lako halijafaulu viwango vyao wanatoa number plate na kukwambia ukarekebishe, gari halitaruhusiwa kutembea mpaka lirekebishwe.
Sasa nina maswali kwa wahusika natumaini masali yangu yatasaidia wengi.
1.What is the vehicle emission standard kwa Tanzania?
2.Huko tunakoagiza magari huwa mnawapa emission standard zetu ili magari yakija yakidhi hizo standard?
3.Emission standard zinatofautiana nchi na nchi na Tanzania tunanunua magari kutoka nchi mbalimbali je watawezaje kupambana na hio changamoto?
4.Magari mengi ya zamani (<2005 ) hayafikii emission standard za >2010 na wenzetu huko wana phase out taratibu hizo gari nyinyi hapa mtafanyaje na gari nyingi hapa Tanzania ni za miaka 10 au zaidi iliopita.
Mfano kuna magari yana catalytic converter na mengine hayana hasa hasa ya Japan kuanzia 2005 kushuka hili mnalichukulia vipi?
5.Gari zilizojaa 'showrooms' mmezipima kabla ya kuuziwa sisi ili tukinunua msije kuzikamata na kutoa number plate?
Wakaguzi wa haya magari naomba mjibu maswali haya natumaini mtatusaidia maanake tunakoelekea mtatoa number plates za magari mengi sana na yatabaki ya serikali yale mapya tu!
Emission standard - Wikipedia