Wamiliki wa Magari Adimu (brand tofauti na TOYOTA, Magari yenye changamoto ya upatikanaji wa Spare Parts) Tukutane Hapa

Inategemea RAV 4 ya mwaka gani kama hizi za 2006 kwenda mbele spare bei ni zile zile tu mkuu...
Yes mkuu hata mm nilikuwa na Carina ti yaani spare zake huumizi kichwa.
Sasa hivi nikipata pesa nataka ninunue rav 4 nione Kama itakuwa vzr kwenye gharama za spares.
 
Huyu jamaa nimemkubali sana, nilikuwa natafuta spare ya nissan bluebird hapa dar naambiwa 360,000 ila nilipomcheki yeye kaniagizia nje nadhani nairobi kwa 140,000 ndani ya siku mbili mzigo nikaupata na sasa nadunda mtaani.
Embu ona sasa,tofauti ya laki nzima!
 
Nissan Elgrande imekaaje wakuu. Naona bei imepoa na chombo kina space ya kutosha
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,sisi wamiliki wa magari ambayo ni brand tofauti na TOYOTA tunapata changamoto nyingi sana ambazo zinapelekea wengine kushindwa kuyahudumia magari yao na mwisho kuachana nayo au kuyatelekeza kwenye magereji au kuyauza kwa bei ya HASARA kitu kinachopelekea magari haya kuonekana hayafai na watu wengi kusita na kuogopa kuyanunua.

Sasa basi Uzi huu ukawe msaada wa kupeana habari,taarifa,na huduma ambazo zitapelekea kusaidia kupunguza adha ya kuhudumia magari yetu kuanzia kwenye upatikanaji wa spare parts kwa bei reasonable na mafundi wenye ujuzi wa kuzielewa hizi gari.

Mimi binafsi nimeshakutana na changamoto nyingi kwa kumiliki ka gari kangu kadogo aina ya VW POLO,nimevumilia matatizo mengi ya mafundi na bei kubwa za spare tangu nimeanza kukamiliki lakini kilichonitokea juzi juzi hapa ndicho kilichopelekea mimi kuleta huu mjadala humu jukwaani ili tuweze kusaidiana na mwishowe magari haya yaonekane ya kawaida na isiwe adhabu kuyamiliki.

Gari yangu ilikuwa na tatizo la fuel pump la muda mrefu kidogo baada ya kuwekewa mafuta machafu,kwahiyo ilikuwa na tatizo la kuchangaya,ilikuwa naweza kusimama kwenye mataa taa zikiruhusu gari inakosa nguvu ya kwenda kabisa kiasi kwamba magari ya nyuma yangu yananipigia honi,fundi akaniambia hiyo itakuwa tatizo ni fuel pump,ikabidi niingie mtandaoni nikakutana na jamaa anauza spare za magari mbalimbali sitamtaja humu basi fuel pump bila housing yake ilinitoka 250,000/= pamoja na kubembeleza nipunguziwe bei haikusaidia ilinibidi ninunue tu kwasababu gari ndio ninayoitumia kwa mizunguko yangu mjini lakini iliniuma sana kwasababu najua online aliexpress fuel pump hiyo isingezidi 70,000 mpaka kuipata lakini ingenibidi nisubiri wiki tatu au zaidi na hiyo ndio ilikuwa changamoto

Na hiyo sio mara ya kwanza kununua spare kwa bei mbaya kuizidi hii,changamoto ni nyingi sana kwahiyo wale wamiliki wenzangu wa magari haya adimu,mafundi,wauzaji spare tukutane hapa tuelezee changamoto tunazokutana nazo ili tuweze kuona ni namna gani tunaweza kusaidiana.

Nawasilisha.
NATAFUTA MLANGO STARLET WA ABIRIA KUSHOTO NYUMA
Kama kichwa cha habari kilivyo ,natafuta mlango wa kushoto wa nyuma haraka sana,
Tafadhali kwa yeyote aliyenao tuwasiliane kwa PM au hata hapa hapa.
 
Mkuu ulikuwa sahihi ukiona mtu anajibu pumba kwahuu uzi uliouleta ujuwe huyo anamiliki baiskel achana naye mimi nimemiliki mazda imenitesa kwenye spea najuta kwenye Toyota kifaa cha 125000 mazda utapata kwa 400,000 wakati huo spea nishida kuzipata, kwa ushauli mfuko ukituna gari yakununua ni Toyota
Pole mkuu sasa umeiuza nini au umepata suluhisho la spea zake.
 
Hii kitu naikubali sana japo 4600cc ila wasiwasi spea
 

Attachments

  • BG314443_c00e04.jpg
    BG314443_c00e04.jpg
    29.5 KB · Views: 63
Namiliki Nissan FUGA timing belt tu ilikatika ikanitoka 110,000
Hiyo ni bei ya kawaida mkuu. Hasa ukinunua OEM parts. Mie nimenunua ya Toyota Tsh 120,000. Sema za Toyota mara nyingi kuna kuwa na copies nyingi mtaani ndio maana zinaonekana cheap.

Ila kama unanunua original parts za Toyota, hazipishani saana bei na zile za European cars. Tofauti ni kwamba, most Japanese cars are very realiable. Hata zikiwa na zimetembea saana.
 
Back
Top Bottom