ni kweli, mienasubiliutekelezaji wa mita 60, ndio watakuwa wamefungua hizo fukwe kwa wote, ila sasa mh!
Mimi sidhani kama ni hivyo...hutozwi kuogelea unatozwa kutumia huduma za hoteli hiyo. Kwa mfano ukiweza kupaa angani ukatua baharini usawa na hiyo hoteli ya whitesands na kuendelea na mambo yako na baada ya hapo ukapaa ukaondoka zako hakuna mtu anayetakiwa kukuchaji. Ukitumia huduma nyingine zozote zilizowekwa na hoteli hiyo ni lazima ugharamie.
Mfano hai: Kule kigamboni kuna beach kama tatu zinafuatana..Kipepeo, Sunrise na South Beach..ukiweza kupita vichochoroni ukaingia baharini ukaogelea hadi usawa wa South beach hakuna mtu atakudai..na kwa kuwa zinapakana waweza kuendelea kuogelea usawa wa hoteli yoyote hapo.
Utakapotoka majini na kwenda kukaa umbali wa hizo mita 60 nje ya bahari (kisheria) au kutumia viti au chochote ambacho kiliwekwa na hoteli hiyo kwa ajili ya watu wake ni lazima utadaiwa.
Huo ni mtazamo wangu!
http://![]()
Wamiliki wa Hotel za kitalii zilizoko katika fukwe mbalimbali nchini wamepigwa marufuku kutoza wananchi kiingilio wanapoenda kupumzika na kuogelea katika fukwe hizo.
Marufuku hiyo imetolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, fukwe zote ni mali ya umma hivyo hakuna anayepaswa kuzitumia kwa biashara akiwatoza fedha wananchi.
“Fukwe zote ni mali ya umma kwa sababu kuna mipaka yake, hivyo kitendo cha kuwatoza wananchi fedha kuingia katika fukwe hizo ni kosa kisheria na wanaofanya hivo wanapaswa kuacha mara moja,” alisema Heche.
Baadhi ya hotel zilizoko katika fukwe hususan jijini Dar es Salaam zimekuwa zikitoza wananchi kiingilio cha kati ya shilingi 10,000 na 40,000 kwa kutembelea fukwe hizo kupunga upepo na kuogelea.
Katika hatua nyingine, Heche aliwataka wawekezaji wote waliojenga katika fukwe za bahari kuhakikisha wako umbali wa mita 60 kutoka Baharini, kinyume cha hapo nyumba na hotel zao zilizo chini ya umbali huo zitabomolewa.
Chanzo: Dar24