Waliotumbuliwa wadai wana siri nzito

Tunataka kujua hizo siri nzito walizo nazo kwa manufaa ya Taifa, naomba mahakama ziwape ushirikiano wa kutosha
 
Wazitoe
Naona nao wanaharufu ya unafiki, mbona hizo siri hawakuzitoa mapema kwa maslahi ya taifa? Kwa sababu Ngosha kawanyima ugali ndo wanaanza kutishia
Kila kitu na mwanzo na sababu pia,hawakusema mwanzo Ila sasa wamepata sababu,wacha watoe hizo siri kama wanazo kweli.
 
Siri Nzito? hahaha, nacheka kwa dharau tu, yaan mnatishia nyau, hivi mnajua maana ya serikali?

Kwanza mshukuruni JPM tu maana hatoi sababu za kutumbua mbali na ile ya Kitwanga ambayo ilikuwa ni lazima aiseme, na ile ya Board ya TRA, wengine hajasema.

Mkapa kipindi chake alikuwa anasema hivi....

"Rais amemstaafisha *** kwa manufaa ya Umma" hayo manufaa ya Umma nani aliyewahi kuyahoji?

Rais kumteua mtu ni discretion yake, na kumuondoa ni discretion yake, sasa unahoji nini mahakamani? unahoji kutenguliwa kwa nafasi yako au stahiki zako baada ya kutenguliwa?

Kwanza, Rais akiamua kutuma team ikuchunguze toka umeanza kazi katika Taasisi husika hadi unatenguliwa uliyokuwa unayafanya au uliyofanya, na maendeleo yako na kipato chako, na kama kulikuwa na matumizi mabaya ya ofisi au madaraka, ndugu yangu umekwisha, tena kwa hawa Watanzania waliokuwa wanakula cake enzi za JK. utawakamata wengi sana, waambieni watulie tu, wajiajili tu, wadau stahiki zao tu wapewe. ..


Hii ndio Afrika Bwana, kama huamini hii ni Afrika, Nyanyua kichwa chako kwa watawala uone....
 
View attachment 454059

Wasema wataiburuza serikali makamani.

Wadai serikali inawaonea na wapo na siri nzito na wako tayari kuzitoa mahakamani.
Shauli yao bora watulie tu lasivyo watageuziwa kibao sasa hivi kwa kufunguliwa mashataka ama ya uzembe au matumizi mabaya ya madaraka.
Wanatishia kujamba wakati wanaumwa tumbo la kuharisha, Teh! Teh! Teh!.
 
ahha ahaha, walikuwa wanatwambia vijana mkajiajili
Mkuu kijiajiri kwa mdomo ni rahisi wajiajiri sasa tuone mfano na sie tujiajiri.Kuna yule Doctor wa Morogoro aliomba msamaha bila kosa kisa kaachwa kwenye uteuzi.
 
View attachment 454059

Wasema wataiburuza serikali makamani.

Wadai serikali inawaonea na wapo na siri nzito na wako tayari kuzitoa mahakamani.
Hii ni sawa na kutongoza msichana,
akakutolea nnje!

Baadae unaanza kumponda [kumkashifu] mara ooh! Kwanza hauna uzuri wowote!

Unaringa miguu yenywe kama chupa ya konyagi!
Nk.
 
i wanna dance for you eeh ... kwa nini wakae na masiri mazito? kwa maana hiyo wangeendelea kukaa kwenye nafasi zao siri ingeendelea kuwa siri basi sawa mimi nimeelewa
 
Bila shaka na mama yangu Anne Kilango atakuwepo kwenye huo msafara wa kumshitaki JPM!;)
 
Mtu mzima hatishiwi Nyau; mahakamani hakuna kiingilio wala kibali, waende hata jana! Ebho
 
na wao wachapukie fursa sasa!!si walikuwa wanasema vijana wajiajiri..na wao wakajiajiri sasa!
 
Wakili wao ni Tundu lissu na hiyo habari imetolewa na Tanzania Daima.
 
Wakajiajiri tu hakuna namna maana waliimba vijana wajiajiri sasa wao cjui kama wameanza,tena wana bahati sana wametimuliwa kipindi wamachinga hawasumbuliwi kabisa so waende kariakoo nafasi zipo waache ubabaishaji,vp kama wangesema hizo siri mapema
 
Back
Top Bottom