Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,032
- 4,736
Ninavyoelewa mimi madai uandaliwa na anayedai na kuwasilisha pamoja na vielelezo Kwa mdaiwa. Kama ndivyo naamini kampuni iliyotengeneza ndege zetu ndiyo iliyowasilisha madai ya kiasi wanachoidai serikali. Kama pia tunakubaliana hapo maana yake aliyepandisha bei ya ndege ikawa mara mbili NI kamapuni iliyotengeneza ndege siyo mtumishi WA umma.
Tukiendelea kukubaliana Hadi hapo tutabaini kwamba wanaopokea invoice kwenye taasisi nyingi ni watu wa uhasibu au finance na Kwa maana nyingine hakuna invoice inayopokelewa kwenye taasisi private au public Bila kupitia Kwa wakurugenzi (private sector) au Katibu Mkuu WA sekta husika Kwa upande wa serikali.
Tutazidi kukubaliana kwamba Afisa masuuri WA serikali katika sekta ni Katibu Mkuu WA sekta au wizara husika, Kwa makampuni Afisa masuuri ni Mkurugenzi mtendaji au mtendaji mkuu. Kama tunakubaliana basi hapa aliyepokea invoice siyo junior officer Bali ni top managerial officer ambaye lazima Kwa upande wa serikali kimuundo ni Katibu Mkuu wa Wizara aidha ya fedha au Uchukuzi, mkurugenzi WA Fedha WA Wizara husika na Kwa shirika la ndege atakuwa mtendaji mkuu WA shirika la ndege nchini au mtendaji mkuu WA mamlaka au wakala WA ndege za serikali.
Baada ya kupokea invoice Kwa ukubwa fedha zilizoombwa na mtengeneza ndege walishauri au walipitisha Kwa malipo. Nimeeleza haya baada yakuona kuna upotoshaji unaendelea bungeni kuhusu hii hoja kama ifuatavyo;
Tumeambiwa kuna hatua za kinidhamu zimechukuliwa au zitachukuliwa lakini hakuna Katibu Mkuu, mtendaji mkuu au mkurugenzi aliyetumbuliwa wala kuwajibishwa Hadi sasa.
Serikali haiwezi kulipa fedha nyingi kiasi hiki Bila waziri kujua; hakuna waziri aliyewajibishwa. Hivyo pamoja na watumishi WA umma kupitisha maana yake hata waziri alikubaliana na malipo husika ndiyo maana akaruhusu imfikie Mhe. Rais ambaye alibaini madudu.
Maombi ya malipo yalioombwa na kampuni iliyotengeneza ndege; Hadi sasa hakuna sehemu kampuni hii yenye source documents za kuomba malipo imejadiliwa au kusemwa vibaya. Nasema hivi kumaanisha kwamba kama fedha zingelipwa maana yake zingelipwa kwenye akaunti ya kampuni na hivyo Kwa wizi wowote ule lazima syndicate inahusisha watumishi WA kampuni inayotengeneza ndege. Sijamsikia anayelalamikia kampuni tunawalalamikia Watanzania ambao wao siyo watengeneza invoice Bali waliletewa Tu.
Mwisho; naomba pia kufundishwa, spika anashindwa kumpigia Mhe. Rais apate ufafanuzi? Mhe waziri anashindwa kumpigia Rais apate ufafanuzi? Kwanini wakose KUELEWANA wakati wanatambua fika kwamba uongo na ukweli watakaozungumza unawiza kuathiri nafasi ya Mhe. Rais? Wanapata wapi muda wakujadili kauli ya Mhe. Rais kwakujichanganya? Wanataka Mh. Rais atoke kufafanua? Siyo vyema