Waliokamatwa kwa tuhuma za kununua Makahaba Ubungo kumburuza mahakamani Mkuu wa Wilaya kwa kudhalilishwa! Wadai walifuatwa Guest!

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,755
43,120
Wasalaam!

Baada ya Mkuu wa wilaya ya ubungo kuendesha zoezi la kukamata watu wanojiuza na wanao daiwa kununua makahaba wilayani humo!

Baadhi yao wamedai kufatwa nyumba za kulala wageni na kwenye vyumba vyao na kukamatwa wakituhumiwa kufanya biashara ya ukahaba uku wakidai kuwa wamesingiziwa na kudhalilishwa kwani walikuwa wamelala na wengine walikuwa na wapenzi wao wamepumzika!

Wameeleza kuwa wanajipanga wiki hii kufungua Mashitaka dhidi ya Mkuu wa wilaya binafsi na sio ofisi ya Mkuu wa wilaya kwani wao wanadai kuwa Mkuu wa wilaya ndio alikuwa ana washurutisha jeshi la polisi kuwadhalilisha na waandishi kuwapiga picha na wao hawakupewa nafasi ya kujieleza bali waliunganishwa na makahaba kwenye karandiga!

Wengine wamedai kuwa walikuwa wamelala ili kesho warudi kwa familia zao mikaoni wanashangaa kudhalilishwa na kufedheshwa na Bwana Yahaya aliyejitambulisha kama mkuu wa wilaya!

Wamesema wamesha waambia mawakili wao kumuandikia barua ya kumtaka mkuu wa wilaya kuwasafisha mbele ya jamii kama alivyo wadhalilisha na baada ya siku saba watafungua kesi ya madai dhidi ya Bwana Yahaya na baadhi ya polisi waliokuwa kwenye lile tukio!

NB: Mh. Rais alishasema kama mkuu wa wilaya au mkoa akitumia madaraka vibaya yatakayomkuta yanamuhusu yeye sio serikali!

===

Update juu ya hili soma: Ubungo: Wanawake 36 wanaodai kukamatwa na kudhalilishwa kuwa "Dada Poa" kumfikisha mahakamani DC Hassan Bomboko na kumdai Fidia ya Tsh. Bilioni 36!

===

Pia soma: Mkuu wa Wilaya ya Ubungo adhamiria kutokomeza biashara ya ukahaba
 
Wasalaam!
Baada ya Mkuu wa wilaya ya ubungo kuendesha zoezi la kukamata watu wanojiuza na wanao daiwa kununua makahaba wilayani humo!

Baadhi yao wamedai kufatwa nyumba za kulala wageni na kwenye vyumba vyao na kukamatwa wakituhumiwa kufanya biashara ya ukahaba uku wakidai kuwa wamesingiziwa na kudhalilishwa kwani walikuwa wamelala na wengine walikuwa na wapenzi wao wamepumzika!

Wameeleza kuwa wanajipanga wiki hii kufungua Mashitaka dhidi ya Mkuu wa wilaya binafsi na sio ofisi ya Mkuu wa wilaya kwani wao wanadai kuwa Mkuu wa wilaya ndio alikuwa ana washurutisha jeshi la polisi kuwadhalilisha na waandishi kuwapiga picha na wao hawakupewa nafasi ya kujieleza bali waliunganishwa na makahaba kwenye karandiga!

Wengine wamedai kuwa walikuwa wamelala ili kesho warudi kwa familia zao mikaoni wanashangaa kudhalilishwa na kufedheshwa na Bwana Yahaya aliyejitambulisha kama mkuu wa wilaya!

Wamesema wamesha waambia mawakili wao kumuandikia barua ya kumtaka mkuu wa wilaya kuwasafisha mbele ya jamii kama alivyo wadhalilisha na baada ya siku saba watafungua kesi ya madai dhidi ya Bwana Yahaya na baadhi ya polisi waliokuwa kwenye lile tukio!

N:B Mh Rais alishasema kama mkuu wa wilaya au mkoa akitumia madaraka vibaya yatakayomkuta yanamuhusu yeye sio serikali!
Kuna Ma RC na Ma DC bado ni Wababe- Samia
 
Kufuata watu gesti ndio job description yake??

Humo ofisini kwake hakuna hata file moja alishughulikie akaona kuvamia watu wakikulana ndio dili.

Yule aliyekula mwanafunzi alivaa kapelo, huyu nae anayechungulia watu usiku kavaa kapelo.
 
Kutofuata Sheria ni ugonjwa kwa watanzania wengi mpaka viongozi.

Unaanzishaje operation bila kufanya impact na legal analysis?

Makahaba hawana chapa, katiba inalinda faragha ya mtu, yeye na askari wake waligunduaje kuwa wale ndani ya gest house au lodge walikuwa makahaba na siyo wapenzi?
 
Imagine uliipanga Pisi ije ukaitumia nauli.. ww ukatangulia huko GESTI..

Pisi yenyewe haikuja.. Nauli imeliwa bado na hao jamaa wakakubebelea kwenda kituoni😅.

Nendeni sehem za maana hzi Gesti za buku buku ndio shida yake hii.
Bado ni kosa kumfata mtu guest au kwenye chumba hata ukimkuta na mwanamke atakuwa amefanya kosa gani? Naona wanakosea sana
 
Back
Top Bottom