Walimu wenzangu: Hivi ukiwa mwalimu ni lazima uvae manguo yasiyoeleweka, oversize na malonya?

Kumbe wewe ni
Habari za jioni Jf........

Asilimia kubwa sana ya walimu nguo tunazovaa kwakweli kuna muda ukikaa kumtizama mtu unacheka kimoyo moyo, mwalimu wa kike unakuta kavaa gauni panaaa linaishia katikati ya miguu sio fupi sio refu, kama ni sketi basi sehemu ya hips imezidi inakua kama nguo ya kuazima, chini sandals, koti oversize, wengine hadi na nywele twende kilioni......vivyo hivo walimu wa kiume shati bongee la shati mkono unashindwa kujua ni la mikono mifupi au mirefu, suruali buga (bwanga) mkanda haujulikani rangi, mkanda mrefu unazungushwa kama kanga... Hii ni kwa ufupi ila tuna mengi mno.

Walimu kwanini tunavaa hivi? Tumeshindwa kutofautisha kati ya haiba na kuwa smart?? Haiba ni kuvaa nguo oversize au lonya? Au ni akili tu tumezitune manguo ya ajabu ajabu ndo yetu? Sijui wanafunzi huwa wanawatuwazia nini...

Cha ajabu hata walimu wanafunzi nao wanakuja field nguo wanazovaa mmh, naishia kuwaza nnavowajua Wanachuo vivazi vyao wakiwa chuo, very smart wanakuja field utadhani ni watu wametoka vijijini, sketi imeungwa vipande saba yani ipo kama kabeji
Tujirekebishe jamani haiba sio kuvaa malonya
Kumbe wewe ni mwalimu!
 
Walimu wako desperate kuolewa, hamna subra, ulishaolewa? Halafu mbona Dar walimu hawavai kama ulivyosema?
Acha chai, wapo desparate kuolewa?????
Walimu ni wife materials, soko la walimu kwenye ndoa ni kubwa mno :D wanafata manesi
 
Nilipanda daladala nikamuona mwalimu anatoa kitambulisho asilipe nauli kwa amri ya Mheshimiwa. Ajabu mwanafunzi analipa 200/=
 
Naiona shida kubwa sana. Both kiuchumi (mtawanyo wa pesa kwenye JamiI, daladala), na kijamiii, heshima ya mwl inashuka.
***Boreshha maslahi yao na mengine yatajiset
Kwani heshima ya walimu ilikua lini juu?
Wanajeshi wanavopanda bure na wao heshima imeshuka?
Mtuache jamani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom