Walimu walipwe kama maofisa wa BoT na TRA, tatizo la walimu litakoma mara moja!

mbona BOT na TRA wako hadi leo? ulipwe mshahara mzuri halafu uukimbie? sio kweli. tena wakilipwa vzr wataanzisha na biashara nje ya kazi na ualimu ukaendelea. Walimu wanasahaulika wakuu
Unajua status? Status ya kazi ya bot na ya uaskari zinafanana?
Hivi wewe ni askari unalinda benki kila siku hulali na unalipwa milioni nne kwa mwezi.. Utafanua hio kazi kwa miaka mingapi
 
Mbona umemchagua anayelinda bank wapo ma ACP,commissioners,kuna mkubwa IGP kama umemchagua askari mlinda bank jua tu analipwa vizuri kuliko teller wa bank au coin counter wa B.O.T ukipanda rank na rank ya polisi pia inapanda acha mawazo ya jeshi la kipindi hicho.
 
Wengi wanakimbilia ajira BOT na TRA. Wengine TAKUKURU na JWTZ, kinachowapeleka kwa wingi ni mishahara minono.

Leo taifa linakabiliwa na uchache wa walimu hasa wa masomo ya Hisabati na Sayansi. Najiuliza kama kuna nia ya dhati ya kumaliza tatizo hili, maana tiba yake ni rahisi kuongeza mishahara iwe kama ya taasisi nilizozitaja hapo juu.
Ndugu yangu mimi bado sijakuelewa.
Soko kwa walimu wazuri[waliobobea kwenye masomo wanayofundisha] mbona ni zuri sana?
Kuna mwl kijana ambaye mara nyingi hupenda kumchokoza kuhusu malalamiko ya waalim. Aliniambia kuwa soko ni zuri sana kwenye shule binafsi kwa wale waliobobea kwenye masomo fundisha. Aliniambia alivutwa kwenye shule moja [secondary] kwa kuambiwa kuwa kwa kila kichwa 1 cha div anakula 50k na kwa kila kichwa cha div2 anakula 20k
alininiambia walichacharika isivyo kawaida na kufanikiwa kupata motisha nzuri sana na juu ya hivyo akaibiwa na shule nyingine ambayo nayo ina motisha zaidi.
Kwa maoni yangu ni kwamba wengi walioingia ualimu waliingia hivyo kwa sababu ya kutafuta nafasi ya kwenda chuo kikuu lakini ari ya ufundishaji haipo. Hivi mnaweza kuamini mwalimu anafundisha kiingereza lakini mwenyewe hawezi hata kujieleza kwa lugha hiyo????
 
issue ni wito sio mshahara mnono
Tupo karne 21 hii wito ni kazi za kanisani tuu. Mwalimu ni binadamu nae ana mahitaji binafsi, anahitaji aishi vizuri, avae vizuri, asomeshe watoto wake pia. Halafu kumbuka walimu ndio wanaotegemewa sana na familia zao kwa sababu wametoka katika familia duni. Hiyoo ni sababu ya kinyonyaji ambayo haina tija. Imefika wakati walimu wanufaike kupitia taaluma yao na muache kuwadharau.
 
Walimu wazuri ni wangapi? wangapi ni walimu wa shule za binafsi? shule ngapi za serikali hazina hao walimu wazuri au walau wa kutosha? hapa hatuzungumzii hao wachache wanaolipwa pesa nyingi, tunawaxungumzia wengi walio na mishahara duni. ingekuea wengi wanaliowa vizuri kusingekuwa na shida ya walimu leo.
 
Tupo karne 21 hii wito ni kazi za kanisani tuu. Mwalimu ni binadamu nae ana mahitaji binafsi, anahitaji aishi vizuri, avae vizuri, asomeshe watoto wake pia. Halafu kumbuka walimu ndio wanaotegemewa sana na familia zao kwa sababu wametoka katika familia duni. Hiyoo ni sababu ya kinyonyaji ambayo haina tija. Imefika wakati walimu wanufaike kupitia taaluma yao na muache kuwadharau.
hoja imeshiba!
 
Tatizo ni walimu wa sayansi na hisabati kama hawatatoa motivation kwa walimu wa sayansi na hisabati kuwaongezea mshahara kidogo kulinganisha na wa sanaa uwe juu ya wa sanaa,basi wanasayansi wataenda kwenye kada nyingine zenye green pasture na siyo education hailipi unalipwa kama mwalimu wa saana.yeye hana practical.
 
Mbona umemchagua anayelinda bank wapo ma ACP,commissioners,kuna mkubwa IGP kama umemchagua askari mlinda bank jua tu analipwa vizuri kuliko teller wa bank au coin counter wa B.O.T ukipanda rank na rank ya polisi pia inapanda acha mawazo ya jeshi la kipindi hicho.
??????????
Unajua tunacho kiongelea lakini? Sijakuelewa kabisa
 
Wanazungumziwa walimu ila nataka kukudeal wewe uliokuja na status...na umefanya comparison kwa polisi na wafanyakazi wa bank,B.O.T vs Polisi....sasa wewe unataka kuniambia kuwa askari wote wanalipwa sawa? Na nenda kawaulize mateller wanalipwa sawa na manager or wamiliki au coincounter wa BOT analipwa sawa na Governer....kuna madaraja tofauti tofauti nawafahamu PT kibao wanaishi kama mungu tz hiihii huwezi kumcopare na mfanyakazi wa bank.
 
umemjibu vema
 
wage
Tupo karne 21 hii wito ni kazi za kanisani tuu. Mwalimu ni binadamu nae ana mahitaji binafsi, anahitaji aishi vizuri, avae vizuri, asomeshe watoto wake pia. Halafu kumbuka walimu ndio wanaotegemewa sana na familia zao kwa sababu wametoka katika familia duni. Hiyoo ni sababu ya kinyonyaji ambayo haina tija. Imefika wakati walimu wanufaike kupitia taaluma yao na muache kuwadharau.
wage theory mkuu
 
Kun kazi zingine kutokana na mazingira yake ukiongeza tu mshahara watu wataacha hio kazi baada ya mwaka au miaka miwili , wataenda kufanya biashaa zao .. Kama ualimu na uaskari...
Kaka hujasoma economics ee?
kweli aiseee inatakiwa mishahara yao isiwatoshe ili kila siku wawepo
 
Back
Top Bottom