Wakwe zangu wachunguzwe afya ya Akili zao.

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,380
Ndugu wanajf ninyi ndio jamii kubwa yakutoa ushauri mzuri hapa Tanzania, mimi nimebahatika kupata takribani watoto 4 na kila mtoto na mama yake kulingana na mazingira ya kiafrika. Lakini cha kushangaza wakwe zangu wamegeuka kuwa wajuvi wa mambo, yaani wao basi kila kitu wakiuliza kuhusu mimi wao wanatoa taarifa yaani taarifa za Uongo mwanzo mwisho.

Hivi mwanamke ukizaa naye ndio anakuwa ameshakujua maisha yako yote....,tena sio mkeo, hivi mwanamke ukimuoa hata mambo yako mengi hajayajua na ukamuacha ndio kishawajua mpaka marafiki zako ambao hata hujawahi kumtambulisha......,

Mimi nashangaa imefikia hatua wakwe zangu wameunganishwa na wanasiasa ili wanivuruge wakitoa taarifa za uongo kila wakati. Yaani hawana hata uelewa wa Ukoo wangu wala maisha yangu wala elimu yangu wala mapito yangu, lakini taarifa wanazotoa kwa jamii ni za kushangaza sana, mpaka nabaki na shangaa sana, tena wakwe wenyewe hata siwajui hata kwa sura ila kwa kaumarufu kangu wao wanalazimika kunijua.

Ndugu zangu hata michepuko nayo inatoa taarifa za kubumba bumba, hivi sisi Watanzania tunatabia gani....mbona kila kipya kinyemi kinakuwa gumzo...kuoa familia zetu hizi za uswahilini yataka MOYO.

Mfano mkuu kuna mmjomba mkwe mmoja anafanya kazi pale njia ya kuelekea magogoni hana hata ABC zangu lakini anavyopotosha juu yangu na kuwalazimisha jamii inayonizunguuka waniwekee vikwazo (mwipae nilisha achana naye na ameolewa). Majangaaaaaaaaaaa

Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa chama tarajiwa cha ACA.

NAOMBENI USHAURI.
 
Mkuu ungekua na hela kiasi ningekushauri uchukue likizo uende mbali kabisa ikiwezekana hata nje ya nchi, u-refresh mind, huko usifungue JF wala facebook, wala usiwaze kabisa kuhusu CCM na walivyokufanyia,
Ukikaa kama mwezi hivi utarudi ukiwa OK, lasivyo unaelekea kubaya kwa kweli
 
Deo kila nikisoma mabandiko yako huwa ninabaki mdomo wazi. Kuna tatizo kubwa linalokukabili.
Kuhusiana na hili la wakwe kupimwa akili, ninakushauri kwa moyo wa dhati kabisa usindikizane nao mpatiwe huduma wote.
Ukiona wanachelewa, bora wewe uwahi.
 
Wewe Deo unamatatizo makubwa sana Psychological nakushauri utembelee wataalam wakushauri otherwise naona kila unachoandika kinamadhara kwenye future yako, kwa kifupi unastress kubwa sana
Na kama hii kwako ni Tabia basi hutaweza kuishi na mwanamke wa aina yeyote maana unaweza kubishana jambo dogo wewe ukaliandika facebook.
 
Wakwe zako akina nani..?
Wewe Deo wewe, si huna mke..!
 
Pole mkuu sio wa kukutania ila wafate watalaamu wakushauri maana kila unachoandika mimi sijawahi kukuelewa zaidi ya kukuonea imani tuu na kuomba kesho tujaaliwa uje vizuri..
 
Pole sana Mkuu bado hujachelewa kupata msaada. Kila la heri Mkuu.

 
mwajiri wako ana haki ya kukufukuza kazi na sababu ni ugmawa wa akili sasa ndugu ukifukuzwa kazi sh1 utaokota makopo hapo tu hauko sawa kichwani
 
Deo fanya kama Makufuli anavyofanya kwenye suala la Bashite
ZIBA MASIKIO USIMSIKILIZE MTU
Songa mbele uanzishe chama,watanyooka tuu
 
Huyu chalii sijawahi kumwelewa aiseee embu pitia mirembe kwanza basi kabla hujaja kutuchosha humu samahani lakini sikuelewagi kabisa sijui kwanini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…