dumejm
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,179
- 848
Hivi karibuni (takribani miezi mitatu sasa) nimeshuhudi baadhi ya watu huko mitaani wakijihusisha na uwekezaji katika jukwaa linalofahamika kama FIC (wenyewe wanawaita Football investment Charity) huku wakimwaga sifa kwamba mabwana hawa (FIC) wanalipa na ni mchongo legit kwa sasa.
Kutokana na maelezo yao ,unaambiwa watu wanatengeneza mamilioni ya fedha kwa kuweka mkeka mmoja wa kubashiri mechi za mpira wa miguu kila siku ambao unaongeza mtaji wako kwa asilimia 2.5 kila siku ambapo kwa maelezo yao initial investment inajizalisha mara mbili kila mwezi.
Siyo mtaalamu wa masuala uwekezaji lakini baada ya kusikia tetesi na kuona namna watu wanavyousifia uwekezaji huu ikabidi niingie kufanya utafiti kodgo kuchimba taarifa zao. Baada ya utafiti mdogo niliyoufanya haya ndiyo baadhi ya mambo ambayo nimeyagundua
1. Hii ni ponzi scheme, SCAMMERS (mwisho wake hautakuwa mzuri)
2. Hakuna taarifa za tovuti yao kwenye search engine ya google, Hakuna review yoyote iliyowahi kundikiwa bofore katika kipindi hicho cha miaka 2 ambacho wanaclaim wameanza.
2. Kwa Tanzania washiriki wengi watakuambia "kwa hapa bongo mchongo huu una miaka miwili sasa" lakini ukifanya utafiti utagundua shughuli zao kwenye mitandao ya kijamii zimeanzia rasmi mwezi julai mwaka huu.
4. Washiriki wengi watakuambia mchongo huu umeanzia UK lakini hakuna taarifa zozote za uwepo wao huko UK
5. Mazingira ya mtaji kujidouble kila mwezi huo ni mtego(nyavu), hii inakuvuta kuendelea kuacha fedha zako kwenye system yao (unambiwa ukianza na 10k baada ya mwaka mmoja utakuwa na takribani 90M)
6.Mchakato wa kutoa fedha hauko automated, inaweza kukuchukua kuanzia dakika 30 hadi masaa matatu kupata fedha zako baada ya kuomba kutoa.
7.Wameanza kujishughulisha na shughuli za kusaidia jamii(hii triki yao kuiaminisha jamii ili waonekane ni legit)
8.Ukifuatilia chats zao kwenye mitandao ya kijamii hao wanaojiita viongozi utagundua kuwa siyo wabongo na hawajui kiswahili kabisa, machapisho yao mengi wanayoandika ni AI generated au AI generated transalated( hii maana yake hao wanaorun hiyo platform hawajui lugha ya kiswahili kabisa, wanaandika kwa lugha zao na kutransate kwa ajili ya wabongo kupitia AI (Chat GPT) (possibly hawa watu ni Nigerians))
9. Unaambiwa ukitaka kutoa fedha nyingi lazima upitie mchakato wa KYC verification, utaambiwa utume ID yako support for verification purpose
10.Sijajua kama Serikali (BOT, Gaming Board Of Tanzania na Capital Markets and Securities Authority (CMSA) ) wanatambua uwepo wao hawa FIC, kwa aina yao ya uwekezaji kwa maana inasemekana wana ofisi kadhaa hapa Bongoland.
11. Mazingira ya kamisheni za kualika watu, kwamba unavyoalika zaidi unajiongezea kamisheni za kualika watu ambayo ni asilimka fulani ya mapato yao kila wiki. Ukiangalia vizuri hii ndio mechanism yao ya kuvuta kijiji ili waje kusepa nacho mwisho wa siku.
Watu wengi waliongia kwenye mtego huu hawana ufahamu wowote wa namna mambo haya yanafanya kazi na wameshajikomiti wakiwa na matarajio ya hali ya juu kwamba baada ya mwaka mmoja wanakwenda kuwa mamilionea
WATAALAMU SAIDIENI JAMII KUPITIA MAONI YENU WATU WAAMKE WAPATE UELEWA MAPEMA KABLA MAMBO HAYAJA HARIBIKA.
NAWASILISHA.