Wako Wapi Vitukuu vya Nabii Nuhu?

Zulu Man Tz

Member
Sep 23, 2020
73
99
Historia Fupi ya Vitukuu vya Nabii Nuhu
Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu ya Biblia Mwanzo 10:1-32 Biblia imeonyesha uzao wa watoto wa Nuhu ambao ni Shemu, Hamu na Jafeti uzao ni kama ifuatavyo Wana wa Japheti ni Gomeri, Magogu, Madai, Javani, Tubali, Mesheki, na Tirasi. Wana wa Hamu ni Kushi (Absyinia kwa sasa Ethiopia), Kemet (Misri ikimaanisha "black ancestry"), Puti na Kanaani. Wana wa Shemu ni Elamu, Ashuru, Arpakshadi, Ludi na Aramu. Biblia inaongelea zaidi uzao wa Shemu ambako kupitia mtoto wake Arpakshadi ndiko Chimbuko la Baba yetu WA Imani kwa dini ya kiyahudi (Judaism), Wakristo na Waislamu.

Wahebrania ndani ya Afrika
Mnamo karne ya 17 Absyinia (Ethiopia) ilikuwa katika mitikisiko ya kisiasa na machafuko ya kutisha dhidi ya nguvu ya kikanda ya wanaogombea udhibiti na ushwawishi juu ya mamlaka ya kifalme nchini humo. Moja ya machafuko nchini humo ni kipindi Cha Zemene Mesafint ambayo inamaanisha "the age of the princes🤴" hii conflict ilikuwa ni takribani ya miaka 150 kwa makadirio ilianza katikati ya karne ya 17 mpaka mwanzoni mwa karne 19. Machafuko hayo yenye mvutano wa pande mbili yaani viongozi wa kikanda(Regional Rulers) na mabwana wa kimwinyi (feudal lords) waliofahamika kama "princes".

Katika kipindi hicho utawala wa kifalme wa Ethiopia ulidhoofishwa na Regional princes wakapata nguvu ya ushwawishi na utawala dhidi ya kiti Cha ufalme nchini humo na kucontrol mipaka ya nchi iyo. Cha kuongezea ni kwamba Zemene Mesafint walikuwa pia na conflict na nchi jirani zao hasa utawala wa Ottoman ambao walifanya jaribio la kuivamia na kuichukua Ethiopia mwishoni mwa Karne ya 16 na mwanzoni mwa Karne ya 17.
Kipindi Cha Karne ya 17 vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ethiopia kugombania ufalme ilipelekea baa kubwa la njaa nchini humo na amani haikupata kutulia kama mwanzo. Kutokana na njaa kali ikapelekea uhamaji wa wananchi kutoka Absyinia kwenda nchi za Afrika ya Mashariki apa ndipo tunapata"Oromo Migration" kutoka pembe ya Afrika, the expansion of the Luo people in the Great Lakes region, and the movement of the Maasai people into Kenya and Tanzania.

Ingawaje hii historia imehifadhiwa zaidi kwa masimulizi ambayo inarithishwa vizazi hadi vizazi kuna mkanganyiko na wabobezi wa historia ulmwenguni kuhusiana na Migration ya watu kutoka Ethiopia na kuhamia Afrika ya Mashariki. Ya kwanza ni Nilo-Hamitic Migration ambao hawa wanaamini watu wenye asili ya Ethiopia walihamia East africa kipindi Cha miaka 3000 K.K, na wengine wanaamini kuwa watu kutoka kundi la wanaoongea Afro-Asiatic ambao ni watu wa kushi na Semitic asili yao ni Absyinia (Ethiopia) na walihamia Africa ya Mashariki baadae. Kwa mujibu wa historia za masimulizi ya kiafrika tunaamini kuwa Karne ya 17 ndio uhamaji wa watu ulifanyika toka Absyinia ya Kale to East Africa ya sasa.

1. Oromo Migration
A. Kabila la Wanyaturu

 Kama nilivotangulia kusema baadhi ya watu wa kabila la Oromo walihama toka Ethiopia to East Africa katika Karne ya 17. Warimi ambao ndio baadae waliitwa wanyaturu, ni kama makabila mengine waliokuja nao kutoka Absyinia na kuingia kaskazin mwa Tanzania kupitia mipaka ya Kenya na Uganda.

Warimi baada ya kuingia Mwanza walifanya maskani yao Uzinza-Mwanza na baadae walihamia sehemu ya Pasiansi hapo hapo Mwanza.

 Wasukuma wakiwafukuza wanyaturu na wakakimbilia Ntunzu uko Mashariki mwa pasiansi, baadhi ya wanyaturu wakaendelea na safari kuelekea Mashariki mpaka walipofika mkoani Singida na baadhi yao waliendelea kuishi hapo Ntunzu walipoona panawafaa.

Kutokana na masimulizi ya kinyaturu (Oral Traditional) Mtemi maarufu wa kabila ilo ambaye ni Kimweri Ye Nyaturu ambaye inasadikika kuwa wazazi wake walitokea kando kando ya Ziwa Victoria ambao ni kati ya waliobakia Ntunzu uko usukumani na wakaamua kuwafuata ndugu zao Singida mnamo Karne ya 18.
 Kimweri Ye Nyaturu alizaliwa mwaka 1860 uko katikati mwa Tanzania na alikuwa mtoto wa Mtemi.

Kimweri Ye Nyaturu alikuwa kiongozi wa Kabila la wanyaturu kipindi Cha nwisho wa karne ya 19 mpaka mwanzoni mwa karne ya 20, aliishi katika kipindi Cha ukoloni wa wajerumani na alijulikana kwa kupinga ukoloni wao na kulinda mipaka yake. Baada ya utawala wa wajerumani kimweri ye Nyaturu alipata umaarufu Mkubwa kwa kuwapinga wajerumani na ukoloni wao. Kimweri Ye Nyaturu alifariki mnamo mwaka 1927 lakini legacy yake tunaikumbuka daima.

B. Kabila la wadatoga (Wamang'ati)
Watu jamii ya wadatoga asili yao pia ni Nilotic origins ambao walitokea ziwani Eyasi huko Sudani ya kusini na Nyanda za juu Magharibi mwa Nyanda za juu za Absyinia. Kuhamia kwao kutoka izo sehemu baadhi yao waliamua kukaa Nchini Kenya hapo ndio tunawapata kabila la Kalenjin na wengine wakaja kuingia kaskazin mwa Tanzania na kuunda kabila la wasandawe au wadatoga.

2. Expansion of Luo People in the Great Lakes Region.
Kutoka Karne ya 15-20 makabila mbalimbali yenye uhusiano na Nilo-semitic group kutoka Nchi ya Misri, Ethiopia na Sudan ya kusini walihama kutoka kwnye nchi zao na kuelekea nchi za Uganda- kaskazin, Mashariki mwa Nchi ya Kongo, magharibi mwa Kenya na mwishowe kuingia kaskazin mwa Tanzania ( Mara, Shinyanga na Mwanza).

Makabila ya watu wa asili ya Luo Sudani ya kusini ni Shilluk, Anuak, Pari, Acholi, Balanda, Boor, Thuri na Luwo. Nchini Uganda makabila hayo ni Acholi, Alur, Jonam na Padhola. Nchini Kongo Mashariki tunawapata kwny kabila la Alur. Nchini Ethiopia luo people ni kabila la Anuak ambalo kwa majina mengne wanajulikana Kama Anyuak, Agnwak, na Anywaa huko Kusini Magharibi mwa Ethiopia kando kando ya mito. Nchini Misri makabila ya Luo ni (Tekidi), Kush and Meroe. Nchini Tanzania na Kenya tunawapata kwny makabila ya wajaluo, wakalenjin, wajita na uko Chad kuna kabila la Maban lenye asili ya luo people.

3. Movement of Maasai People and their relatives.
Wamaasai na watu wa jamii zake wanaofanana nao kama vile Turkana, Samburu, Kalenjin,na waarusha, inaaminika kwamba asili yao ni kutoka Ethiopia na Sudan ya kusini kando kando ya bonde la Mto Nile sehemu ijulikanapo kama"Dapash" kipindi Cha Karne ya 15. Jamii zote hizo zinapatikana Tanzania na Kenya.

Soma kwa makini izi scenario zikufumbue macho muafrika mwenzangu.
Makabila yote niliyokwisha kuyataja hapo juu yana uhashiria mkubwa Lugha zake zinafanana na lugha ya kihebrania Cha kale waliongea Mababu zetu wa kiimani za ukristo na uislamu Abrahamu,Isaka na Yakobo na hata Nabii Musa huko Kemet(Misri ya sasa). Mfano. Kimisri Cha zamani-Kaka, kihebrania-kaka, kiswahili(kibantu)-Kaka. Kihebrania-nakah, kimisri-Nakah, kikongo-Nioka, Kiswahili-Nyoka. Neno Nile jina lake halisi ni "Nahar" kwa kihebrania uo ni Mto Nile ilo jina lilipewa na ukoo wa wa Shemu ambako ndiko alipozaliwa Arpakshadi ambaye ndio Chimbuko la Babu wa Imani wa dini zote Abrahamu.

Maana ya Jina Musa kwa kijita ni aliyeotoka majini "Msa" na kihebrania ni "Masha" maana yake ni aliyetolewa majini ukirejea biblia utaelewa Kitabu Cha Kutoka 2:10. Pia Misri sio jina la Kiarabu ni jina la mjukuu wa Nuhu aitwae" Mitsraim" hawa wote walikuwa weusi na sio wazungu. Baada ya Misri kutawaliwa sana na Waarabu ndio ikawa mwisho wa ukuu wa mtu mweusi apo Kemet ya Kale.

Bara la Afrika zamani liliitwa "Alkebulan" hiki ni kibantu maana yake ni mama wa watu au bustani ya Edeni. Mto Kongo au Mto Zaire ndio ulikuwa Mto Yordani.

Mfalme Suleiman alipoanza kujenga hekalu takatifu la Bwana alitafuta watu wenye taaruma ya ujenzi ambao ni watu kutoka Absyinia na Kemet yaani Ethiopia ya Kale na Misri.

Na uko ndiko ilikotoka dhahabu kwa wingi ya kupamba hekalu uko Ofiri ambayo inasadikika ni Sudan ya kusini au pwani mkabala ya Somalia na Arabia (1 Wafalme 9:26-28). Na pia uko Ofiri ilitoka miti ya misandali iliyojenga Nguzo kuu za hekalu la Bwana, vinubi na vinanda(1 Wafalme 10:11-12).

Kihebrania "Mayim" na kiswahili/kibantu tunaita "Maji" strong positive correlation ❤️🙏
Mwaka 1776 Mmsionari Abbe alishangaa akiona wakongo wakiongea lugha iliyofanana sana na kihebrania Cha kale ila wakongo wenyewe hawafahamu wamerithishwa kwa masimulizi tuu. Hio ndio iliyofanya Pope Francis wa kanisa Katoliki kutembelea Kongo na Kisha Kubusu viatu vya raisi wa Kongo na kisha kwenda uko Sudani ya kusini kutokana na machafuko ya kivita nchini humo.

Naambatanisha iyo picha ya Pope Francis na Ramani ya Alkebulan (Afrika ya Kale) kwny picha kabla hawajaja hawa wakoloni, wamisionari na wapelelezi wao na kugawana Afrika yetu Kama Chapati kwa kigezo Cha Dini zao.

Screenshot_20230207-215826.png
map-africa-1763-A66YYF.jpg
Asanteni kwa kusoma Nakala Yangu, Mwenyezi Mungu mwenye Rehema awe nanyi.🙏❤️
 
Kutokana na masimulizi ya kinyaturu (Oral Traditional) Mtemi maarufu wa kabila ilo ambaye ni Kimweri Ye Nyaturu ambaye inasadikika kuwa wazazi wake walitokea kando kando ya Ziwa Victoria ambao ni kati ya waliobakia Ntunzu uko usukumani na wakaamua kuwafuata ndugu zao Singida mnamo Karne ya 18.
 Kimweri Ye Nyaturu alizaliwa mwaka 1860 uko katikati mwa Tanzania na alikuwa mtoto wa Mtemi.
 
Shida iliyopo ni kuwa hatuna huo ujanja sasa wa kusema sijui tulikuwa na maendeleo kuliko wazungu aka wakoloni.
 
Kutokana na masimulizi ya kinyaturu (Oral Traditional) Mtemi maarufu wa kabila ilo ambaye ni Kimweri Ye Nyaturu ambaye inasadikika kuwa wazazi wake walitokea kando kando ya Ziwa Victoria ambao ni kati ya waliobakia Ntunzu uko usukumani na wakaamua kuwafuata ndugu zao Singida mnamo Karne ya 18.
 Kimweri Ye Nyaturu alizaliwa mwaka 1860 uko katikati mwa Tanzania na alikuwa mtoto wa Mtemi.
mshana anzisheni uzi wa historia ya kweli ya afrika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom