Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 180,977
- 1,094,426
Asante mkuu. Nilifikiri utakasirika.Asante sana mkuu wa clarification umeelezea vizuri sana japo naona bado kuna dosari kidogo ngoja niiweke sawa.
Neno "tombina" kwa tafsiri yake ya kiujumla bila kujalisha ni kwa wasukuma wa wapi(general meaning)lina maana ya "mzinzi na mpuuzi mkubwa"
Na sio lazima muda wote linatumika zima zima kama lilivyoo, Sasa inategemea na neno hilo unalitumia wapi na kwa nani.
Kama unalitumia kwa mtu mneheshimiana naye mfano mjomba au mzazi wako ukimwambia "tombina" anapaswa kuchukua hiyo tafsiri ya "mpuuzi mkubwa tu" na akaacha hiyo ya "mzinzi"
Ndio maana unaweza kuta mama mtu mzima anamwambia mtoto wake mdogo wa miaka 5 "ole na masabu? tombina"
Kwa akili ya kawaida tu hapo hauwezi kusema huyo mama ana maanisha mtoto wake mdogo wa miaka 5 ni "mzinzi" so obvious atakuwa anamaanisha hicho kipande kingine cha tafsiri ambacho ni "mshenzi mkubwa"
Asante kwa kunidokeza lahaja za kinyantuzu... Katika lugha zote za kibantu naona hili lugha letu huwa tamu sana. Msamiati mmoja una maana kama milioni utafikiri ile lugha ya dunia bwana.
Wabeja sana nkohi.
Lugha hai ni tata mno; na matumizi yake mara nyingi hutegemea muktadha, mahali, mahusiano ya wazungumzaji na vigezo vingine vingi. Ndiyo maana mara nyingi tafsiri huwa zinapwaya sana.
Ukiwakuta masela wapo kijiweni wanaambiana "we msenge sana" kwako mpita njia unaweza kukunja uso na hata kusikitika. Lakini kwao, kulingana na mahusiano waliyonayo, mahali walipo na muktadha wa wakati huo, neno msenge hapa laweza hata lisiwe tusi kivile.
Nafurahi kuwa hili limeeleweka na mmeweza kuombana msamaha ilipobidi. Huo ndiyo ubinadamu na utu.
Blessings. Wabeja namhala.
Tombina bebe !!!