Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,488
- 3,568
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (Tanganyika Law Society -TLS), utakaofanyika Agosti 2, 2024, Wakili Msomi Peter Kibatala ametishia kususia Uchaguzi huo ikiwa Wakili Boniface Mwambukusi hatarudishwa kwenye orodha ya Wagombea
Soma; Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi imemuengua Boniface Mwabukusi kugombea nafasi ya Rais wa TLS
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wakili Kibatala amesema “Ukweli ni kwamba nisingempigia kura Mwabukusi. Ningempigia kura Wakili Paul Revocatus Kaunda, lakini kama jina la Wakili Mwabukusi halitarejeshwa kihalali katika orodha ya Wagombea wa Urais, nitasusia mchakato wa Uchaguzi wa TLS, na Mkutano. Huu hautakuwa utovu wa nidhamu; ni uamuzi wa kibinafsi. Nitalipa ada zangu, lakini nitasusia mkutano.”
Ameongeza “Itakuwa pia mpango binafsi kwa yeyote ninayeketi naye kuwashawishi kufuata nyayo zangu. Wakati huo huo; 1. Nitaungana na Mwabukusi katika hatua zozote za kisheria anazoweza kufuata. Hakuna Uchaguzi halali wa Urais wa TLS unaoweza kufanyika katika mazingira haya.”
Pia soma; Mwabukusi afungua kesi kupinga maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya TLS kumuengua kugombea Urais wa TLS
Aidha, amemalizia kuwa “Waachwe wanachama wachague: sisi ni WANASHERIA. Sisi ni ngome ya mwisho. Hapana.”