Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
- Thread starter
- #21
Ni watu wachache sana wanaojua na kutumia Kiswahili ipasavyo, hata hiyo Tanzania yenu. Au unafikiria ule uharo nyie huandika ndio Kiswahili. Mtu anapokua muwazi na kukuambia hakifahamu Kiswahili vizuri unamchukulia kuwa mjinga, ilhali huo ndio ukweli.
Kiswahili chenyewe bado hakieleweki, maneno mengi yanaendelea kubuniwa kila siku maana hakijaiva. Juzi tu ndio mumejua maana ya 'makinikia', miaka yote wakati mlikua mnaliwa, mlikua mnaita mchanga wa madini.
Binafsi nimejikuta kwenye huu upumbavu wa nyie kutuona wajinga kisa tumesekiri kutokujua Kiswahili ipasavyo, ipo siku nilitaka tafsiri ya Kiswahili ya maneno kwa mfano kama 'source code', 'software' n.k. Niliishia kuhangaika maana hata wenyewe hamjui.
Sheria zenu zenyewe mumeshindwa kuziandika kwa Kiswahili, na pia hata stakabadhi muhimu. Juzi hapo kuna zabuni imetangazwa ya kiserikali halafu nikakumbana na maneno kama 'Proposal must be written in English'. Wenyewe mnajua mapungufu ya hii lugha lakini kutwa huwa mnajifanya jeuri, hamna kitu cha ovyo kama maskini jeuri asiyetaka ushauri au kuambiwa.
Leo hii nenda hapo kwenye mgahawa Tanzania na uagize 'sharubati' uone jinsi watakushangaa, hadi pale utaagiza 'juisi' ndio utaeleweka.
Haujaelewa ninachokiongelea, ni kweli kwamba Watanzania wengi wana matatizo na Lugha ya Kiswahili kama vile ilivyo sehemu yoyote ile Dunia hii, hata USA kuna wengi wana matatizo na English language, Uingereza, Uchina hivyo hivyo kuna Wachina wana matatizo na Mandarin, ila tofauti ni kwamba hakuna Mtanzania ambaye anajivunia kutokufahamu Kiswahili, kwetu sisi nia aibu kutokujua Kiswahili, wakati Kenya kutokujua au kujifanya haujui Kiswahili ni sifa, yaani watu wanajivunia kutokujua Kiswahili, wkt mtu huyo huyo ukimwambia hajui Kiingereza mnaweza mkagombana, na hiki ndicho ninachokiongelea!
Girlfriend wangu Mkenya aliniambia Kenya kuna Gazeti la Kiswahili na Wakenya wengi hulisoma kwa kujificha kwa kuogopa stigma kwamba kwa nini anasoma Gazeti la Kiswahili, ndicho ninachomaanisha!
Kwamba kuna tofauti ya kutokujua lugha vizuri na kujivunia kutokuijua lugha wkt ukweli ni kwamba Wakenya wengi wanajua Kiswahili tena vizuri sana tu, kwani sijawahi kupata shida ya kuwasiliana nikiwa huko, ila nimewahi kukejeliwa sana kwamba najua Kiswahili kizuri!