Wakati wa mahusiano kasema ana mtoto1, baada ya kuishi pamoja kumbe ana 3

Awakubali tu kwani shida nini jamani si watoto wa mkeo hao,ni wako pia wapokee haina maana ya kufanya maamuzi mengine we wapokee hao watoto.
 
Heshima kwenu wakuu.
Nina kaka yangu ana mke na huyu wifi yangu ni mke mzuri kwa kweli kila mtu wa familia anampenda ikiwemo mimi binfsi kutokana na tabia zake njema na zisizokera.
Kaka yangu huyu wakati anatafuta mke alitamani apate mke mwenye mtoto anagalau mmoja kwa sababu yeye ana watoto watatu tayari.
Issue hapa ni kwamba wakati anafahamiana na wifi yangu huyu.Waliulizana habari za watoto wifi akasema anae mtoto mmoja.(Na kaka aliamini kitokana na wifi alivyo decent)Walipoanza kuishi pamoja miaka 2 imepita now na wifi akajifungua mtoto mwingine wa kaka.
Sasa kupitia ndugu zake ndo kaka amegundua kuwa wifi ana watoto 3 na sio mmoja kama alivyosema awali.Kumuuliza mkewe kasema ni kweli ila alishindwa kusema mwanzo kwa sababu aliogopa kuachwa.Hao watoto 2 wakubwa wa Sekondari.Na huyu anaeishi nae ni wa shule ya msingi.
Wote wanaishi dar.Kaka anashindwa afanyeje ameniomba nimshauri kabla hajaweka wazi kwa wanafamilia wengine.Nimemwambia hii kwangu ni mpya nikamuomba nipost jamii forums amekubali.Yeye sio member humu ila ushauri atasoma.
Kwa wenye uzoefu hii issue imekaeje ushauri wenu ni muhimu sana.
piga ua ww hujaoa na miaka yako haijatimia 25.
ushauri wangu usiingilie mapenzi ya watu,utaumbuka
 
Hao watoto wanamgharimu chochote?(in terms of pesa), kama jibu ni ndiyo nitashauri...la kama siyo aendelee na mkewe
 
piga ua ww hujaoa na miaka yako haijatimia 25.
ushauri wangu usiingilie mapenzi ya watu,utaumbuka
Hamna kuingilia bana.Hili jukwaa limewekwa kwa ajili ya kusaidiana mambo kama haya.Ni issue ya kushuriana ili kujenga hii familia na bro asimuumize mkewe baas
 
Back
Top Bottom