Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 299,204
- 751,865
Mwanaume alikuwa na kawaida ya kumpa ombaomba mmoja Shilingi milion moja kila mwezi.
Mtu huyo aliendelea kufanya hivyo kwa muda Sana.. Sasa Siku moja, akampa ombaomba shilingi laki saba na nusu pekee. Ombaomba yule alishangazwa na hilo, lakini akajisemea, 750,000 ni bora kuliko kukosa kabisa.. Akaondoka.
Baada ya mwezi mmoja yule mtu alimpa yule Ombaomba 500,000 pekee. Ombaomba akashangaa! Ikabidi sasa amuulize yule mtu, “ Mbona zaman iUlikuwa ukinipa 1,000,000 kisha zikapungua na kuwa 750,000 Sasa Unanipa 500, 000 tuu kwa nini?" Je Naweza kujua sababu?
Yule msamaria akamjibu, “Zamani watoto wangu wote walikuwa wadogo na mimi nilikuwa na hali nzuri Kifedha, ndio maana nilikuwa nakupa 1,000,000. Lakini binti yangu akakua na kuingia chuo kikuu, na gharama za chuo kikuu zilikuwa kubwa, kwa hiyo nilianza kukupa 750,000. Sasa, mwanangu wa pili anaingia chuo kikuu, na gharama zinaongezeka, hivyo ndio maana nakupq 500,000 tuu.”
Yule ombaomba akamuuliza, "Una watoto wangapi?" Msamaria akamjibu, "ninao wanne." Yule ombaomba akamu uliza, “Na utawasomesha wote kwa gharama yangu?!”
Wakati mwingine, wengine huchukulia wema na matendo mema kuwa ni haki yao na sio ukarimu kutoka kwako.🤔🙇🏿♂😪