Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Jan 26, 2019
3,067
6,180
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Watanzania tumelelewa katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano. Hii ni mizizi iliyoasisiwa na wapigania uhuru wa nchi hii na tumeweza kudumu katika misingi hiyo kwa miongo kadhaa sasa.

Anapotokea mtu, awe kiongozi ama yoyote yule, akafanya dhihaka, kukashifu, kubeza na kuingilia imani za dini fulani basi bila shaka anapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Serikali ya Rais Mama Samia ni serikali sikivu na yenye weledi inayosimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hakupaswa kuzua taharuki kwenye vyombo vya habari kwa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane msikitini, ambayo Waislamu wameitafsiri kama uvamizi dhidi ya msikiti huko Kisarawe na kuamuru kituo cha kuhifadhisha Quran kifungiwe huku akiita kuwa ni udhalilishaji.

Pia, alidai kuwa misikiti ni sehemu ya watu kuswali na kuondoka tu huku akitumia kauli za kebehi na dharau kwamba watoto wanalala kama nyanya, wamepangwa kama tofali za block, hata nguruwe hawezi kulala katika mazingira hayo. Mara aseme watoto hao walipaswa wachapwe viboko wote na wazazi wao wawekwe gerezani kwa kuwa wameshindwa kuwalea! Hizi ni dharau kwa wazazi wa Kiislamu! Mzazi anayempeleka mwanae kuisoma dini yake ili awe na maadili mema katika jamii yake aonekane ameshindwa kumlea mwanae!

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Waislamu nchini Tanzania wana taasisi yao ya BAKWATA, ambayo inashirikiana na taasisi nyingine ndogondogo kusimamia masuala ya Waislamu kwa ujumla. Petro Magoti alishindwa nini kuongea na uongozi wa BAKWATA unaoongozwa na Mufti Abubakar bin Zuber kuwa waboreshe kituo hicho cha msikiti wa Kiluvya ili kuweka mazingira rafiki ya vijana wa Kiislamu kuisoma dini yao na jambo hilo lisifike kwenye mitandao na kuzua sintofahamu kama alivyofanya yeye?

Msimamizi wa kituo cha msikiti wa Kiluvya alionekana akimueleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wanafunzi wanaishi katika hali hiyo kwa dharura tu huku jitihada mbalimbali za kuanzisha ujenzi wa mabweni zikiendelea. Nondo, mchanga, cement na matofali tayari vimeshakusanywa na jitihada za kuomba vibali vya ujenzi zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha wanafunzi wanaishi katika mazingira rafiki.

Wito wangu kwa Rais ni kuhakikisha kuwa wateule wake kama Petro Magoti hawaingilii masuala ya kidini moja kwa moja kwa sababu ni eneo nyeti linaloweza kuvunja amani ya nchi hii kwa haraka sana. Awashauri wateule wake wawe na busara katika masuala ya utawala.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.

Video ya Sheikh akitoa mapendekezo kwa serikali nini kilipaswa kufanyika.


Pia soma:Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe ameonekana akizua taharuki na sintofahamu kwa waislam wa wilaya ya kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Huku
Huwa hamtaki kuambiwa ukweli na hamuachi kulialia.

DC yeye ameplay part yale, amesimama kwenye jukumu lake...haiwezekani aone watoto wa miaka mitatu kwa mitano wanaopaswa kuwepo nyumbani kwa wazazi wao wakisoma shuleni eti wanalala nje ya manyumbani kwao na kujipikilisha huko

Haiwezekani Asilani

Cry more !!!
 
Huwa hamtaki kuambiwa ukweli na hamuachi kulialia.

DC yeye ameplay part yale, amesimama kwenye jukumu lake...haiwezekani aone watoto wa miaka mitatu kwa mitano wanaopaswa kuwepo nyumbani kwa wazazi wao wakisoma shuleni eti wanalala nje ya manyumbani kwao na kujipikilisha huko

Haiwezekani Asilani

Cry more !!!
Mwalimu alihojiwa na kusema kuwa hakuna mtoto wa miaka 3 hapo msikitini kiluvya na watoto wote wameletwa kwa ridhaa ya wazazi wao.
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe ameonekana akizua taharuki na sintofahamu kwa waislam wa wilaya ya k

Mkuu wa wilaya Ni Kada wa CCM na kateuliwa na Mh Rais Samia ambaye ni muislamu pia, hapo naona Petro Magoti ameshinda mtanange huu kwani amefuata Sheria za afya na ustawi wa jamii zilizowekwa kihalali bila kujali dini yoyote
 
Mkuu wa wilaya Ni Kada wa CCM na kateuliwa na Mh Rais Samia ambaye ni muislamu pia, hapo naona Petro Magoti ameshinda mtanange huu kwani amefuata Sheria za afya na ustawi wa jamii zilizowekwa kihalali bila kujali dini yoyote
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
 
Watangulizi wa Petro Magoti mbona hawakuleta taharuki hizi.

Wamepita ma DC, Mh Jokate mwegelo na Nikki wa pili wameishi vizuri tu na wana Kisarawe ila yeye toka aje Kisarawe amekuwa ni mtu wa kuzua taharuki.

Kwanza kaanza kwa kutoa matamko kuwa mabinti wa kizaramo wasichezwe, pikipiki zisitumike kubeba mkaa pikipiki ikikamatwa anaitaifisha , hajakaa vizuri kaja na haya
 
Watangulizi wa Petro Magoti mbona hawakuleta taharuki hizi.

Wamepita ma DC, Mh Jokate mwegelo na Nikki wa pili wameishi vizuri tu na wana kisarawe ila yeye toka aje kisarawe amekuwa ni mtu wa kuzua taharuki.

Kwanza kaanza kwa kutoa matamko kuwa mabinti wa kizaramo wasichezwe, pikipiki zisitumike kubeba mkaa pikipiki ikikamatwa anaitaifisha , hajakaa vizuri kaja na haya
utakuwa wa dini ile for such reasoning
 
Hizi ndio chokochoko mnazoleta ili kuvuruga amani ya nchi hii?

Serikali kupitia idara zake za usalama wa taifa isijue kama kuna mafunzo ya ugaidi uje kujua wewe chiriku unayelala sebuleni kwa dada yako?
analala seuleni sawa, lakini anachokisema kiko sawa? This is the point to consider!

Ni kweli, si tunayaona, tuna watoto wa ndugu zetu waislamu tunaishi nao. Wanafundishwa kuona wengine ambao siyo dini yao ni makafiri, siyo wenzetu. Ujinga mtupu
 
Back
Top Bottom