Waingereza wairudishia Tanzania zaidi ya bilioni 14

Hii kesi ya kina Kitilya ni litmus test ya TAKUKURU na DPP katika kupambana na kesi zenye makucha ya political movers and shakers wa Tanzania

Nani katika serikali alishirikiana na kina Kitilya? why hafikishwi mahakamani?

Nani alipata Mgao wa hizo dola milioni 6.....Na mnajua wapo kutoka serikali ya CCM...why hawawajibishwi?

Again.....Nchi inaendeshwa kwa Katiba,Sheria na Kanuni...Na si vinginevyo.....Kucheza na maisha ya watu katika kamera ilihali mnashindwa kuchukua hatua kwa Rushwa kubwa serikalini ni jambo ambalo linawaumiza watanzania.....
 
Mh.Raisi bila kigugumizi Anamkubali Zito Kabwe kama Mwanasiasa mahiri Anaetanguliza Maslahi ya Nchi na Maendeleo yake Mfia Nchi Rejea hoja zake zote zenye Mashiko.Ni Hazina kwa Taifa letu Isitoshe ni Kijana Mwenye Maono na ndiye Chachu ya Vijana wengi Nchini Kujitosa kwenye Siasa.Kama Binadamu ye yote ameumbwa na Mapungufu.Ila Basi Tumtie Moyo siku zote BRAVO ZITO
 
Serikali ya Uingereza jana imeirudishia Tanzania kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 14 kama malipo ya faini kutoka kwa Benki ya Standard kutokana na kushindwa kuzuia rushwa.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose wakati wa maongezi maalum kuhusu mafanikio ya Mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu kupambana na rushwa ambao ulishirikisha Viongozi kutoka mataifa tofauti ambao walikutana mjini London.

Malipo ya faini ya kiasi cha dola milioni 6 yalilipwa kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu nchini Uingereza mwezi wa Novemba mwaka jana kuhusu rushwa kwenye hati fungati.

Fedha hizo zinarejeshwa kwa Tanzania baada ya benki ya Stanbic Tanzania kupitia kampuni ya EGMA kuongeza asilimia moja ya riba baada ya serikali kukopa dola milioni mia sita kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo mwaka 2012 na 2013 na kutakiwa kuzilipa katika kipindi cha miaka 7 kwa riba ya aslimia 1 nukta nne na badala yake ikatozwa asilimia mbili nukta nne ya mkopo wote hali iliyotokana na benki kuu kubaini baadhi ya matatizo.

Kutokana na kugundulika kwa rushwa hiyo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifanya uchunguzi na tarehe 1/4/2016 iliwafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon.

Washtakiwa wote walishtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Serikali ya Uingereza imeisifu serikali ya awamu ya Tano kwa kupambana na rushwa huku ikisisitiza kuhusu furaha yake kwa Rais Magufuli kutuma Wawakilishi walioongozwa na Waziri Mkuu, Majaliwa kwenye Mkutano huo wa kimataifa kuhusu kupambana na rushwa.

‘’Tumefarijika na dhamira ya serikali na pia hotuba ya Waziri Mkuu, Majaliwa iliyoonyesha hatua zinazochukuliwa katika kupambana na rushwa. Alisisitiza kuwa utashi wa kisiasa ni muhimu sana vikiunganishwa kwa sheria imara na hatua imara za kiutawala’’ alisema Ms Melrose.

kwa kweli ni aibu kwa nchi yetu makosa yanatokea kwetu sisi tunakaa kimya wenzetu wanaangalia kwa upande wao wanachukua hatua alafu ndio tunajisifu.

kashfa ya rada waliturudishia chenji lakini kwetu ni kina nani walituingiza kwenye kashfa hiyo na walichukuliwa hatua gani ? tulibaki kuzungumzia chenji ya lada ambayo hatukurejeshewa fedha bali bidhaa zenye thamani.

sasa hili wao wamechukua hatua lakini kwetu tushaanza mara huyu anasema hawa wana hatia yule anasema hakuna ushahidi.!

ni lini system ya uongozi ya tanzania itakuwa serious? yaani kila mmoja kwa nafasi yake yuko serious na kumtetea mwananchi? inavyoona tunagwanyika katika vipande wakati wote huyu akiwa serious yule yuko bize na interesti zake na mwisho system haina good results.
 
kashfa ya rada waliturudishia chenji lakini kwetu ni kina nani walituingiza kwenye kashfa hiyo na walichukuliwa hatua gani ? tulibaki kuzungumzia chenji ya lada ambayo hatukurejeshewa fedha bali bidhaa zenye thamani

Ni mheshimiwa Mzee wa Vijisenti,Mbunge wa CCM na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
zitto kabwe alilipigia kelele hili suala hatimae pesa yetu imerudi.
#BravoZittoKabwe

Kubwa_Lao Mh Zitto anataka deni lote lisamehewe maana kisheria ya kimataifa benki ikihusika Kwa njia moja Au nyingine juu ya rushwa deni linasamehewa sio $6M Ni $600M
 
Issues kama hizi zenye maslahi ya taifa huwezi kuwaona kina Lema au Msigwa wao wanakomaa na bunge liwe live tu.

Big up Zitto
 
Kubwa_Lao Mh Zitto anataka deni lote lisamehewe maana kisheria ya kimataifa benki ikihusika Kwa njia moja Au nyingine juu ya rushwa deni linasamehewa sio $6M Ni $600M
ni kwel linasameheka, ila tatzo, hajatilia maanani kama hawana 10% basi serikal itakuwa kunakitu inakitafuta
 
Japo mimi siyo mwanasheria, kesi hii ni kama haipo kwani washtakiwa muhimu hawapo mahakamani na hata sababu hatuambiwi. Walioshtakiwa ni madalali so, ingekuwa na maana inayotarajiwa na kunadiwa mbele za kamera za kupambana na rushwa kama wahusika halisi wa serikali wangepandishwa kizimbani. Na hapa ndipo dpp anapotuchanganya tusiokuwa lawyers ili mwisho wa siku wahusika wahalalishwe kutokuwa na hatia na fidia watalipwa.
 
Japo mimi siyo mwanasheria, kesi hii ni kama haipo kwani washtakiwa muhimu hawapo mahakamani na hata sababu hatuambiwi. Walioshtakiwa ni madalali so, ingekuwa na maana inayotarajiwa na kunadiwa mbele za kamera za kupambana na rushwa kama wahusika halisi wa serikali wangepandishwa kizimbani. Na hapa ndipo dpp anapotuchanganya tusiokuwa lawyers ili mwisho wa siku wahusika wahalalishwe kutokuwa na hatia na fidia watalipwa.
Kama nilivyosema, hawa madalali itabidi wawaseme waliowadalalia. Huu ni muda mwafaka wa kujua mbivu na mbichi.

Nitawashangaa kama wataamua kwenda kaburini peke yao.
 
Pesa zinazotakiwa kurudishwa au kutolipwa ni zile dola milioni 600 ambazo ni zaidi ya trilioni.

Sasa hao Waingereza wamerudisha change tu na lile Deni la dola milioni 600 za kitapeli liko pale pale na riba yake tunaendelea kulipa.

Waingereza ambao hazikuwa pesa zao wamelamba zaidi ya bilioni 40, nyie mnafurahia hiyo bilioni 14.

Mkopo Mzima ni batili na Deni lote lifutwe. Wale waliopitisha pia upande wa serikali wakamatwe.
 
Tatizo hizo hela zitapigwa tu kama ile chenji ya rada ambayo matumizi yake kwenye vifaa vya elimi ni utata mtupu. Ndani ya CCM hata malaika hugeuka sheitwani
Mkuu ivi bado unadhani hizi ni enzi za akina lowassssa na sumayiiii walipokuwa madarakani? Mambo ya rushwa kwa namna yanavyoshughulikiwa sahz wala haihitaji hasira. Kama kuna ndugu,jamaa, rafiki au umpendaye kisiasa anaguswa kwa namna moja au nyingine usiwe na hasira maana waweza kujikuta unazimia na hata vinginevyo zaidi ya kuzimia.
 
Hiyo pesa kurudishwa nchini,ni ushahidi tosha kuwa kosa limitendeka.
Inaweza kuwaweka kwenye hali mbaya sana Mzee kitilya na wenzake
Alafu bado utaja sikia kuwa watuhumiwa wameachiwa huru kwa kukosa ushahidi wa kutosha.
 
Watanzania kweli elimu, elimu, elimu. Mtu anakuibia trilioni1.3 kisha anarudisha bilioni 14 unashangilia?
Tunataka zile dola milioni 600 zote zirudi au Deni lifutwe.
Riba tu ya hizo pesa kwa mwaka ni zaidi ya hizo bilioni 14 mnazoshangilia.

Bila kukamata viongozi wa serikali na wale wa bank ya Uingereza walioidhinisha hili sisi tumelizwa tu. Tutabaki kuhangaika na madalali.
 
Ushauri wangu kwa ZITO ZUBERI KABWE Usitoke Nje Kutetea na Kusemea yale yaliyo na faida ya Nchi.Epuka kundi la Wanaporojo na Publicity.Siku zote Umejitanabaisha Kuifia Nchi .Songa Mbele Usikatishwe na Wale wenye Chuki Binafsi.Wewe Ukweli Usofichika na Hazina ya Taifa.Komalia na Mengineo hasa uwakilishaji wako wa Hoja si kwa Kubeza ila kwa kuelezea Ukweli pasina shaka Na Matokeo ya Hoja zako Watanzania Tunaziona.Upinzani Ndo huu wakueleza Serikali Hoja zenye Mashiko si Kubeza kila Kitu Serikali Ima Raisi anachokifanya kwani Wengine wanachokisema kwa Wananchi Utadhani hawa ni Wake Wenza.BRAVO ZITO LET THEM SEE WHAT IS BLACK AND WHAT IS WHITE
 
Hii kesi ya kina Kitilya na mkwe wa Edward Lowassa ni litmus test ya TAKUKURU na DPP katika kupambana na kesi zenye makucha ya political movers and shakers wa Tanzania.

Ninafahamu Katiba ya Tanzania 1977 katika Ibara ya 54(5) inalinda kisihojiwe sehemu yoyote kilichojadiliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri lakini ingekuwa ni vizuri tukafahamu yaliyokuwa yanajiri katika vikao kuhusu hili sakata.

Katiba ya Tanzania inasema;
54(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika mahakama yoyote.

Cha msingi ni kusikia utetezi wa washitakiwa kwa sababu ninaamini kuwa wengine bado wako mitaani lakini wanatakiwa wawe washitakiwa au mashahidi katika kesi hii.

Watu kama Bashir Awale ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Stanbic lazima wahusishwe katika kesi hii. Waziri wa fedha wa wakati huo lazima ahusishwe katika kesi hii. Gavana wa BOT na Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha wa wakati huo lazima wawepo kwa njia moja au nyingine.

Hawa kina Kitilya ni chambo tu cha kuwanasa samaki ambao ninaamini bado wako majini wanaelea.

Ninaisubiri kwa shauku hii kesi!
kesi hio itaisha juu kwa juu,kwani wakiikomalia kuna watu wako serikali itawazoa!
 
Watanzania kweli elimu, elimu, elimu. Mtu anakuibia trilioni1.3 kisha anarudisha bilioni 14 unashangilia?
Tunataka zile dola milioni 600 zote zirudi au Deni lifutwe.
Riba tu ya hizo pesa kwa mwaka ni zaidi ya hizo bilioni 14 mnazoshangilia.

Bila kukamata viongozi wa serikali na wale wa bank ya Uingereza walioidhinisha hili sisi tumelizwa tu. Tutabaki kuhangaika na madalali.
Tatizo lako unachokiandika nadhani hujui hata maana yake!

Unataka dola milioni 600 zirudi wapi wakati serikali ya Tanzania ndiyo imekopeshwa na inatakiwa kulipa baada ya miaka saba.

Ninyi Tanzania ndiyo mnatakiwa mzirudishe kwa waliowakopesha!

Kuna baadhi ya watu mnafurahisha sana.
 
Back
Top Bottom