Tanzania ! Tanzania ! Tanzania !
Habari za leo vijana wasomi.
Naomba kutoa wazo hapa hasa kwa Serikali dhidi ya Vijana wa elimu ngazi ya Shahada.
1. Serikali tunaweza anzisha "VIJANA SECURITY FUND". Hii ikawa maalumu sana kwa vijana wa taifa letu umri kuanzia miaka 18 mpaka 44. Huu uwe mfuko wa vijana utakaowasaidia vijana nchi nzima kujipatia mitaji kwa ajili ya kujitengenezea ajira kwao na kutupatia faida nchi kupitia KODI.
a) Hii taasisi itapendeza ikisimamiwa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam hasa wale idara ya Ujasiriamali.
b) Vyuo vyote kuanzia vyuo vya chini, kati na juu ndio vitumike kwenye kuwasajili wanafunzi kwenye mfuko huo hasa waliohitimu.
c) Vyuo vitumike kubuni na kuwasaidia vijana wake mawazo ya Biashara, Viwanda na Ajira (kwa wale wasio na mawazo imara). Hapa kila chuo kiwe na tovuti ya wahitimu (GRADUATE PORTAL) wahitimu watajisajiri humo na kupeana taratibu humo humo.
2. Serikali tuanzishe "LOCAL INVESTMENT HUB" . Hii iwe platform kwa vijana wote (iwe ni lazima kwa kila kijana milele) iwe wamepata elimu iliyorasmi na wale wasio na elimu rasmi. Hapa pawe na uwekezaji hasa uwekezaji wa kikanda, kitaifa na kimataifa. Hii hao iwe na uono wa fursa za uwekezaji hapa Bongo, East Africa na Africa nzima. Wenye mitaji wanaweza wekeza mitaji yao na kuvuna faida; wasio na mitaji watapewa mitaji na usimamizi ili wakuze mitaji yao na walipe madeni ya LOCAL INVESTMENT HUB.
3. Serikali tuanzishe Idara maalumu ya Uwekezaji (Hii idara ishuke chini mpaka ngazi ya Kata na itasimamiwa na vijana wenyewe wa eneo husika) mpaka kwenye ngazi ya Taifa.
N.B
Kuna aina nyingi za uwekezaji, fursa na kukuza maendeleo katika taifa letu. Tatizo hapa ni mitaji kwa vijana.
Tanzania ina uhaba na fursa nyingi yaani kila sekta inauhaba sana zaidi ya inavyodhaniwa na kuzungumzwa.
Karibu.